Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-04 19:21:17    
Mapishi ya vipande vya samaki mkunga

cri

Mahitaji

Samaki mkunga gramu 200, uyoga gramu 20, mizizi ya mianzi gramu 15, vipande vya vitunguu maji gramu 5, pilipili hoho gramu 5, vipande vya vitunguu saumu na tangawizi gramu 5, chembechembe za pilipili manga gramu 2, chumvi gramu 2, mvinyo wa kupikia gramu 2.

Njia

1. kata samaki mkunga awe vipande, koroga pamoja na chumvi, mvinyo wa kupikia, chembechembe za pilipili manga na vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi.

2. washa moto mimina mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya samaki mkunga kwenye sufuria, korogakoroga halafu vipakue. Washa moto tena, halafu tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, pilipili hoho, korogakoroga, tia vipande vya mizizi ya mianzi, uyoga, mimina mvinyo wa kupikia, korogakoroga tia vipande vya mkunga, mimina maji na mchuzi wa sosi, baada ya kuchemka, punguza moto, mwisho weka pilipili hoho na chumvi, korogakoroga ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.