Mazungumzo ya duru la pili ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa yatakayofanyika kwa wiki mbili yalianza tarehe 2 huko Bonn, Ujerumani, wajumbe zaidi ya 2,400 kutoka nchi na sehemu 172 wanashiriki kwenye mazungumzo hayo, wajumbe wa mkutano watajadili zaidi utekelezaji wa "mpango wa Bali" uliopitishwa kwenye mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana huko Bali, Indonesia, na kufanya maandalizi ya uidhinishaji wa mkataba wa kulinda hali ya hewa ya dunia wa baada ya mwaka 2012, ambao utapitishwa kwenye mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwaka kesho katika mji wa Copenhagen, Denmark.
"Mpango wa Bali" unaagiza pande zote husika zimalize mazungumzo kuhusu utaratibu utakaofuatwa wa hifadhi ya hali ya hewa baada ya "Makubaliano ya Kyoto" kufikia muda wake mwaka 2012. Mazungumzo ya duru la kwanza yalifanyika nchini Thailand kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu. Kuhusu mazungumzo ya safari hii, ofisa husika wa wizara ya mazingira ya Shirikisho la Ujerumani alisema, anatarajia kuwa mazungumzo hayo yatakuwa muhimu sana katika mchakato wa "mpango wa Bali", mkataba wa kuhifadhi hali ya hewa wa baadaye unatakiwa kuthibitisha mwelekeo wa kupata maendeleo ya uchumi, lakini hewa ya Carbon dioxide inayotolewa ni sharti iwe kidogo zaidi. Na nchi za viwanda pia zinawajibika kuhusu kuongezeka kwa joto duniani, na zinatakiwa kuchukua nafasi ya kuongoza.
Kwa kuwa hadi hivi sasa Marekani bado haijasaini "Makubaliano ya Kyoto", nchi zinazoendelea pia zinatarajia kuwa mazungumzo kuhusu hifadhi ya hali ya hewa yatafanyika chini ya kanuni za mapatano kuhusu hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa, kwa hiyo, mazungumzo ya safari hii yatafanyika katika vikundi viwili. Kwa upande mmoja, nchi zilizosaini "Makubaliano ya Kyoto" ziwe katika kikundi kimoja, na kujadili wajibu wa nchi za viwanda wa kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani, ikiwa ni pamoja na lengo la kupunguza utoaji wa hewa za aina hiyo kwa 25% hadi 40% kuliko ule wa mwaka 1990. Kwa upande mwingine, nchi ambazo hazijasaini "Makubaliano ya Kyoto", zifanye majadiliano katika kundi lingine zijadili zaidi kuhusu hatua za kupunguza utoaji wa hewa za aina hiyo kwa nchi za kikundi hicho, hususan Marekani, ili kutoa mchango kama unaotolewa na nchi zinazoendelea kwa utaratibu wa hifadhi ya hali ya hewa katika siku za baadaye. Ajenda ya mazungumzo iwe ni pamoja na hatua mwafaka kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, teknolojia ya kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani na uwekezaji kwenye hifadhi ya mazingira. Licha ya hayo, kutokea tarehe 4 hadi tarehe 13, miundo mwili iliyoko chini ya mikataba miwili ya "Makubaliano ya kanuni ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa" na "Makubaliano ya Kyoto" inajadili kuhusu ubunifu wa mpango wa utekelezaji, uhamishaji wa teknolojia na kuweka akiba ya makaa ya mawe katika utaratibu wa maendeleo wa hifadhi ya mazingira.
Katika mazungumzo hayo ya Bonn, hadhi za nchi zinazoendelea katika hifadhi ya hali ya hewa ya dunia zinafuatiliwa na watu. Uungaji mkono wa kifedha na hatua zinazochukuliwa dhidi mabadiliko ya hali ya hewa na hali mbaya inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani kwa jitihada ya kuzisaidia nchi maskini, ni masuala muhimu yatakayojadiliwa mkutanoni. Kiongozi wa sekretarieti ya "Makubaliano ya kanuni ya mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa", Bw. Yvo de Boer alisema, lengo la kulinda hali ya hewa halitaweza kutimizwa kwa kutegemea nchi za viwanda peke yake bila kushirikisha nchi zinazoendelea. Alitoa wito wa kutaka nchi za viwanda zitoe msaada wa fedha za kutosha kwa nchi zinazoendelea na kuzipatia teknolojia ya kukabiliana na kuongezeka joto duniani.
|