Waziri mkuu wa Iraq Bw. Nouri al-Maliki tarehe 8 alipokuwa na mazungumzo na rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alisisitiza kuwa, Iraq yenye hali tulivu itachangia kuwepo kwa usalama wa sehemu hiyo na hata wa dunia nzima. Bw. Maliki aliiahidi Iran kuwa, Iraq haitatoa nafasi ya kuiathiri Iran. Wachambuzi wanaona kuwa ziara hiyo ya Bw Maliki inahusiana sana na "mkataba kuhusu hadhi ya jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq" ambao unajadiliwa katika mazungumzo. Hivi karibuni Marekani ilitoa "mkataba kuhusu hadhi ya jeshi la Marekani lililoko nchini Iraq" kwa Iraq, jambo ambalo limesababisha wasiwasi na upinzani mkubwa kutoka kwa Iran, lengo la ziara hiyo ya Bw. Maliki ni kuiondoa wasiwasi wa Iran.
Madaraka liliyokabiwa jeshi na Marekani na Umoja wa Mataifa yatafikia mwisho wa muda wake mwishoni mwa mwaka huu. Na kuanzia mwezi Machi mwaka huu, Marekani na Iraq zilianza mazungumzo kuhusu uhusiano wa muda mrefu likiwemo suala la kuwepo kwa jeshi la Marekani nchini Iraq katika siku za baadaye. Pande mbili zilinuia kufikia makubaliano kabla ya mwishoni mwa mwezi Julai, ili kuhalalisha kuwepo kwa jeshi la Marekani nchini Iraq kwa muda mrefu. Lakini Iran ambayo ni nchi jirani ya Iraq, inalalamika kuhusu mkataba huo. Kwa kufikiria usalama wake, ni dhahiri kuwa Iran haipendi kuona Marekani, ambayo ni "Adui mkubwa" inaweka askari zaidi ya laki 1 karibu na mpaka wake. Mara tu baada ya mkataba huo kutangazwa, ulisababisha upinzani mkubwa kutoka kwa Iran. Rais wa zamani wa Iran Bw. Akbar Hashemi Rafsanjani alisema, Iraq na watu wa sehemu hiyo hawawezi kuiruhusu serikali na Iraq kusaini mkataba huo na Marekani, mkataba huo utatimiza "ukaliaji wa kudumu" wa jeshi la Marekani nchini Iraq, "hali halisi ya mkataba huo ni kuwafanya watu wa Iraq kuwa watumwa wa Wamarekani". Kutokana na mazingira hayo, Bw. Maliki aliongoza ujumbe wake na kuwasili Tehran tarehe 7 alasiri na kuanza ziara ya siku 2 nchini Iran, hii ni ziara yake ya pili nchini Iran katika mwaka huu.
Katika usiku wa siku hiyo, Bw. Maliki alikuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Iran na aliahidi kuwa, Iraq haitatoa nafasi ya kuiathiri Iran. Tena Bw Maliki alisisitiza kuwa huenda Iraq itasaini "mkataba wa hadhi ya jeshi la Marekani nchini Iraq" na Marekani, lakini mkataba huo hautaathiri maslahi ya Iran. Wachambuzi wanasema ni dhahiri kuwa lengo la ziara hiyo ya Bw Maliki ni kuleta ulingano katika mambo ya kidiplomasia na kuifariji Iran. Iraq inataka kuituliza Iran, ili kutuliza mazingira ya usalama ya sehemu hiyo.
Wachambuzi wanasema endapo Iraq itafanya uamuzi wa kusaini mkataba huo, bila shaka itaathiri uhusiano wa nchi hizo mbili. kwanza, Iraq haitaki kuiudhi Iran kutokana na suala hilo, kwani bado ni muhimu sana kupata uungaji mkono wa Iran, ambayo ni nchi ya jirani yake inayoongozwa na madhehebu la Shia kwa serikali ya sasa ya Iraq yenye viongozi wengi wa waislam wa madhehebu ya Shia na Wakurd. Pili Iraq hayo pia haitaki Iran kuendelea kukabiliana na Marekani kwa kuitumia Iraq kwa kutoa uungaji mkono kwa jeshi la madhehebu ya Shia nchini Iraq kutokana na Iran kuathiriwa na mkataba huo. Ni dhahiri kuwa lengo la ziara ya Bw Maliki ni kutaka kuondoa wasiwasi na malalamiko ya Iran, ili kuhakikisha kuendelea kupata uungaji mkono wa Iran kuhusu serikali ya sasa ya Iraq, tena bila ya kuiudhi Marekani.
Jambo muhimu ni kuwa "faraja" ya Bw Maliki siyo ombi tupu, Iraq pia ina hali nzuri ya kufanya mazungumzo na Iran. Bw Maliki anatarajia kuzungumzia ushahidi iliopata Iraq kuhusu uingiliaji wa Iran dhidi Iraq wakati watakapojadili uhusiano kati ya pande hizo mbili. Lakini hata hivyo si rahisi kwa Iran kukubali usuluhisho, na nchi hizo mbili zitaendelea kuvutana kuhusu suala hilo.
|