Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-09 20:10:22    
Shughuli za utalii mkoani Hunan zarejeshwa katika hali ya kawaida

cri

Maafa ya baridi kali na theluji yaliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu yalisababisha hasara kubwa kwa uchumi wa mkoa wa Hunan, China, na pia kwa shughuli za utalii ya huko. Kutokana na takwimu zisizokamilika, hasara iliyosababishwa na maafa hayo kwenye shughuli za utalii mkoani Hunan ilifikia Yuan milioni 600.

Maafa ya theluji yalikatisha mawasiliano na zana za umeme za sehemu zenye mandhari nzuri za mkoa wa Hunan. Habari zinasema maafa ya theluji yalisababisha kukatika kwa matawi ya miti na kupasuka kwa mianzi, eneo lililokumbwa na maafa hayo lilifikia hekta milioni kadhaa.

Baada ya kutokea kwa maafa hayo, idara ya utalii ya mkoa wa Hunan ilishughulika haraka kupunguza athari zinazoletwa na maafa ikiwa ni pamoja na kupanda miti kwa njia mbalimbali na kukarabati mandhari ya sehemu za misitu. Licha ya hayo, serikali kuu pia ilichukua hatua kuzisaidia sehemu zilizokumbwa na maafa mkoani Hunan kustawisha upya shughuli za utalii. Tokea mwishoni mwa mwezi Januari, idara kuu ya utalii ya China ilitoa misaada ya dharura ya Yuan milioni 3.9 kuusaidia mkoa wa Hunan kukarabati mandhari na zana za miundo-mbinu zikiwemo barabara, vibao vya maelezo, vyoo na vituo vya utoaji huduma kwa watalii. Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya mkoa wa Hunan, Bw. Liu Zhiming alisema, hivi sasa shughuli za utalii za mkoa wa Hunan zimeanza kustawi upya. Alisema

"Baada ya maafa ya theluji kwisha, milima na mito ya mkoa wa Hunan itaonekana kuwa na sura mpya na nzuri zaidi. Idara za utalii za mkoa wa Hunan pia zitatoa huduma nzuri zaidi kwa watalii wanaotembelea mkoa wa Hunan."

Mwezi Februari mwaka huu, ambapo theluji na barafu ziliyeyuka, bustani ya misitu ya taifa ya Zhangjiajie iliyoko mkoani Hunan, ilianzisha shughuli za utalii zenye kauli-mbiu ya "Kando mbili za mlango wa bahari wa Taiwan, na sehemu tatu za Taiwan, Hong Kong na Macau zinashikana mkono na Zhangjiajie" na utalii wa michezo ya Olimpiki mkoani Hunan, na kutoa mwaliko kwa marafiki wa sehemu mbalimbali za duniani, na kuwaeleza kuwa soko la utalii mkoani Hunan limeanzishwa upya baada ya maafa ya baridi kali na theluji, sasa watalii wa nchini na wa nchi za nje wanaweza kutalii mkoani Hunan bila wasiwasi.

Shughuli hizo zilifanyika kwenye sehemu yenye mandhari nzuri ya Wulingyuan, mabingwa wengi wa michezo Olimpiki pamoja na watalii wa nchini na wa nchi za nje karibu 1,000 walishiriki kwenye shughuli hizo. Naibu mkuu wa mkoa wa Hunan anayeshughulikia mambo ya utalii, Bw. Gan Lin alipanga shughuli hizo na kujitahidi kufanya matangazo kuhusu sehemu hiyo yenye mandhari nzuri. Anaona kuwa mandhari nzuri ya Zhangjiajie, ambayo ni moja ya sehemu nzuri kabisa duniani, inaanza kufufuka. Alisema,

"Marafiki mliotoka sehemu mbalimbali duniani, ninataka kuwauliza maswali mawili, Je, mandhari ya Zhangjiajie ni nzuri ua la?

Watalii walijibu: ni nzuri!

Bw. Gan aliuliza: mnaonaje?

Watalii walijibu: Nzuri!

Bw. Gan alisema, ninawatakia furaha kwenye matembezi!"

Mbali na kufufuka kwa haraka kwa miundo mbinu ya utalii, sehemu zenye mandhari nzuri za utalii na vivutio mkoani Hunan, masoko ya utalii pamoja na imani ya watalii pia zinaendelea kufufuka. Idara ya utalii ya mkoa wa Hunan inaona, njia nzuri ya kupunguza athari zinazoletwa na maafa kwa wao wenyewe ni kuvutia watalii wengi zaidi waende kutembelea mkoa wa Hunan.

Tokea mwezi Februari, idara ya utalii ya mkoa wa Huanan iliitisha mikutano mingi, na kuweka mpango kamili kuhusu namna ya kuzindua soko la utalii na kupunguza athari zinazoletwa na maafa mkoani Hunan, ilieleza wazi kuwa mkazo unatakiwa kuwekwa kwenye kuendeleza soko la utalii la watu wenye asili ya China wa nchi za Asia ya kusini mashariki, soko la watalii wa ngazi ya juu wa Korea ya Kusini, pamoja na masoko ya Umoja wa Ulaya na Japan, tena watumwe wafanyakazi wake kwenda kwenye sehemu mbalimbali za nchini na za nchi za nje kufanya matangazo ya kuvutia watu, idara ya utalii inatarajia kuonesha sura mpya ya utalii wa mkoa wa Hunan kwa kutumia fursa hizo. Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii wa mkoa wa Hunan, Bw. Liu Zhiming alisema,

"Maafa ya baridi kali na theluji yaliyotokea mkoani Hunan yalifuatiliwa na nchi mbalimbali pamoja na marafiki wengi, na yameongeza sifa za mkoa wa Hunan kutoka kwa upande mwingine. Baada ya maafa hayo, hali ya kufufuka kwa haraka kwa shughuli zetu za utalii imeinua zaidi sifa yetu. Kwa hiyo, ninasema shughuli zetu za utalii itakuwa na nguvu kubwa ya kuwavutia, tuna imani kubwa ya kufufua shughuli zetu za utalii baada ya kukumbwa na maafa."

Hivi sasa hali ya sekta ya utalii ya mkoa wa Hunan inaendelea kufufuka, makundi ya watalii pamoja na watalii binafsi wanamiminikia mkoani Hunan. Tunatoa mfano wa sehemu yenye mandhari nzuri ya Wulinyuan iliyoko Zhangjiajie, tokea katikati ya mwezi Februari hadi katikati ya mwezi Machi, sehemu hiyo ilipokea watalii zaidi ya laki 2.8, kiasi hicho ni zaidi ya maradufu kuliko idadi ya watalii walioitembelea sehemu hiyo tokea katikati ya mwezi Januari hadi katikati ya mwezi Februari. Sehemu nyingi maarufu zenye mandhari nzuri pamoja na vivutio vingi vya mkoani Hunan vinavutia idadi kubwa ya watalii wa nchini na wa nchi za nje.