Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-11 11:17:30    
Nairobi-Mawaziri wawili wa Kenya wafa katika ajali ya ndege

cri

Polisi ya Kenya tarehe 10 Juni ilisema, ndege ndogo ilianguka kwenye sehemu ya magharibi nchini humo, watu wanne waliokuwa kwenye ndege hiyo walikufa, wakiwemo waziri wa barabara wa Kenya Bw. Kipkalya Kones na naibu waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Bw. Lorna Laboso.

Habari zinasema, ndege hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Nairobi kwenda wilaya ya Kericho mkoani Bonde la Ufa, na ilianguka kwenye sehemu ya magharibi mkoani humo.

Hadi sasa, chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana. Rais Mwai Kibabi wa Kenya tarehe 10 alitoa taarifa akitoa rambirambi kutokana na watu waliokufa kwenye maafa hayo, na kutangaza kuwa bendera nchini Kenya zitapepea kwa nusu nlingoti ili kuwaomboleza.