Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-11 16:36:59    
Mapishi ya supu ya uyoga, mboga na nyama ya paja la nguruwe

cri

Mahitaji: Mboga ya majani gramu 50, uyoga gramu 100, nyama ya paja la nguruwe gramu 50, nyanya ndogo gramu 20, vitunguu maji gramu 5, tangawizi gramu 2, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja

Njia:

1. chemsha maji, tia vipande vya tangawizi.

2. tia vipande vya uyoga, mimina mvinyo wa kupikia.

3. tia nyanya ndogo na nyama ya paja la nguruwe halafu koroga.

4. tia mboga, chumvi, mimina mafuta ya ufuta, tia vipande vya vitunguu maji. Acha ichemka kwa muda, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.