Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-11 17:23:10    
Kikundi cha madaktari wa Russia chatoa misaada ya matibabu kwenye sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi mkoani Sichuan

cri

Kikundi cha utoaji wa msaada wa matibabu cha Russia kilichoundwa na madaktari na wauguzi 67 ni kikundi cha kwanza cha matibabu cha kimataifa kilichofika kwenye sehemu zilizokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi huko Wenchuan mkoani Sichuan. Tarehe 21 Mei baada ya kufika huko Pengzhou ambayo ni sehemu iliyoathiriwa vibaya katika maafa hayo, kikundi hicho kilijenga mara moja hospitali ya muda ya matibabu ya dharura na kuanza kazi za kutoa matibabu kwa majeruhi.

Mara baada ya kikundi cha matibabu cha Russia kukamilisha ujenzi wa hospitali ya muda, kundi la kwanza la majeruhi walipelekwa kwenye hospitali hiyo. Bi. Yang Yixu mwenye umri wa miaka 80 alikuwa ni mmoja kati ya majeruhi hao. Wakati tetemeko la ardhi lilipotokea tarehe 12 Mei, alianguka na uti wa mgongo wake ulivunjika. Kutokana na kuwa hospitali za huko ziliharibiwa vibaya, hivyo waokoaji walimpeleka Bi. Yang Yixu kwenye hospitali hiyo.

Bi. Yang Yixu alifanyiwa upasuaji ndani ya saa moja baada ya kufika kwenye hospitali hiyo. Mkuu wa kikundi cha matibabu cha Russia Bw. Aleksander Ivanus alisema, kikundi hicho kinaweza kutoa matibabu kwa ufanisi namna hii, kunatokana na kuwa hospitali hiyo ya muda ina vifaa vya kisasa. Bw. Aleksander Ivanus alisema:

"vifaa vyote vya hospitali hiyo vinaweza kutenganishwa na kuundwa pamoja kwa haraka, hivyo ni rahisi kusafirisha vifaa hivyo. Si kama tu vinaweza kusafirishwa kwa magari, pia vinaweza kusafirishwa kwa helikopta au kudondoshwa kutoka angani. Kwa hiyo hospitali hiyo inaitwa "hospitali inayohamahama ya angani". Hospitali hiyo inatoa huduma za aina 16 zikiwemo uokoaji, matibabu na misaada ya uhandisi."

Bw. Aleksander Ivanus alisema, hospitali hiyo kila siku inaweza kutoa matibabu kwa watu 200 waliojeruhiwa vibaya, na pia inaweza kufanya upasuaji kwa majeruhi 5 hadi 10 kwa wakati mmoja. Aidha madaktari na wauguzi wa kikundi cha utoaji misaada ya matibabu cha Russia wote wana uzoefu mwingi wa kutoa misaada ya matibabu katika matukio ya dharura. Kikundi hicho kiliwahi kutoa misaada katika sehemu zilizokumbwa na maafa makubwa duniani ikiwemo Tsunami iliyotokea kwenye bahari ya Hindi.

Bw. Aleksander Ivanus alisema, ingawa kwa sasa kazi za uokoaji ni ngumu, lakini alifurahi kuona kuwa kazi za uokoaji, kuwapanga wakazi walioathiriwa na maafa hayo na kuzuia maambukizi ya maradhi kwenye sehemu hizo zinaendelea kwa utaratibu. Bw. Aleksander Ivanus alisema:

"tetemeko hilo la ardhi lilitokea kwenye sehemu za milimani na kusababisha uharibifu mkubwa, barabara ziliharibiwa vibaya. Hakuna nchi yoyote duniani yenye uwezo mkubwa wa kutosha wa usafirishaji wa anga kwa kuhamisha haraka wakazi walioathiriwa na maafa hayo kutoka kwenye sehemu hizo. Lakini kwa kukabiliwa na maafa makubwa namna hii, serikali ya China inaweza kuendesha kazi za uokoaji na kukabiliana na maafa kwa utaratibu namna hii, inanishangaza sana."

Mbali na kutoa matibabu kwa majeruhi, madaktari wa Russia pia waliwajibika kutoa misaada ya kisaikolojia kwa wakazi wa huko. Katika hospitali hiyo, mwandishi wetu wa habari aliona Daktari Bi. Olia Makarova alitoa msaada wa kisaikolojia kwa msichana mmoja mwenye umri wa miaka 3 hivi. Imefahamika kuwa wazazi wa mtoto huyo wote walijeruhiwa vibaya katika tetemeko la ardhi, na msichana huyo alishitushwa sana. Bi. Makarova alisema, anataka kumsaidia mtoto huyo kuondokana na kivuli cha kisaikolojia kwa njia ya matibabu ya kisayansi. Bi. Makarova alisema,

"baada ya tetemeko hilo la ardhi kutokea, watu waliingiwa na hisia za woga na hofu, ikiwemo huzuni kutokana na kufiwa na jamaa, na wanahofia majengo kubomoka tena, au kuogopa matetemeko madogo madogo yanayofuatia. Tunalopaswa kufanya ni kuzungumza nao, ili kuwasaidia kujitoa kutoka katika hisia hizo. Kama ni watoto, pia tunaweza kuchora pamoja nao, ili kuwasaidia kueleza hisia zao za hofu na wasiwasi na kuwawezesha kuona matumaini."

Ingawa Bi. Makarova alishindwa kuelewana na watoto hao kwa lugha, lakini alijitahidi kuwasiliana na watoto kwa vitendo. Bi. Makarova alisema:

Kabla ya kumalizika kwa mahojiano hayo, hatimaye tabasamu ilionekana usoni mwa mtoto huyo. Bi. Makarova alisema ana matumaini kuwa watu wote waliojeruhiwa katika tetemeko hilo la ardhi wataweza kuwa na tabasamu tena usoni baada ya muda mfupi.