Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-12 19:06:39    
Balozi Sun Zhenyu achambua sera za biashara za Marekani

cri

Shirika la biashara duniani, WTO, tarehe 11 lilimaliza majadiliano ya siku mbili kuhusu sera za biashara za Marekani.

Marekani ikiwa nchi inayochukua nafasi ya kwanza katika shughuli za kiuchumi na kibiashara duniani, sera zake za biashara zina athari kubwa kuhusu mazingira ya biashara ya dunia. Taarifa iliyotolewa tarehe 11 na WTO inasema, karibu nchi na sehemu zote wanachama zinafuatilia kuzorota kwa uchumi na biashara za Marekani. Balozi wa China katika WTO, Bw. Sun Zhenyu alisema, katika majadiliano hayo sera za sarafu za Marekani zilikosolewa. Alisema,

"Katika majadiliano, China, Umoja wa Ulaya, Japan, Brazil, Thailand, Norway na Uswisi zilifuatilia na kukosoa sera za biashara, hususan sera za sarafu za Marekani. Kupanda kwa bei za mafuta na chakula kutokana na kupungua haraka kwa thamani ya dola za kimarekani, kuleta hasara kubwa kwa nchi na sehemu nyingi wanachama wa shirika hilo zinazoendelea, kwani dola ya kimarekani ni sarafu muhimu duniani, na nchi nyingi zinaweka akiba za fedha za kigeni za dola za kimarekani na kuichukulia dola ya kimarekani kuwa ni sarafu katika kufanya urari wa mahesabu ya fedha, kupungua kwa thamani ya dola za kimarekani kumesababisha mfumuko wa bei za vitu."

Kutokana na kanuni husika za WTO, nchi au makundi ya kiuchumi yanayochukua nafasi 4 za mbele duniani, zinakutana kufanya majadiliano kila baada ya miaka 2 kuhusu sera za biashara, ambapo nchi na sehemu wanachama zinatoa masuala yanayofuatiliwa nazo, nchi na sehemu zinazokaguliwa zinawajibika kutoa maelezo ili kuimarisha maelewano na kupunguza mikwaruzano ya kibiashara. Majadiliano hayo ni ya 9 kwa Marekani kukaguliwa katika WTO, katika majadiliano ya siku mbili, nchi na sehemu wanachama zilitoa masuali zaidi ya 800.

Tarehe 11, ujumbe wa Umoja wa Ulaya katika WTO, ulitoa taarifa ikisema, mwelekeo wa kuweka vizuizi vya kibiashara kwa Marekani ni "ishara moja inayotia watu wasiwasi", kwa mfano hivi karibuni Marekani ikitumia kisingizio cha "kupambana na ugaidi na kulinda maslahi ya usalama wa taifa", inataka makontena yote yanayowekwa bidhaa kutoka nchi za nje yakaguliwe kwa mionzi ya elektroniki, njia ambayo imeongeza gharama ya bidhaa zinazoagizwa na Marekani, na ni kitendo kisichoambatana na kanuni za WTO. Bw. Sun Zhenyu alisema, kitendo cha kuweka vizuizi vya kibiashara cha Marekani kinaonekana kwa udhahiri zaidi katika biashara kati ya China na Marekani. Alisema,

"Wagombea urais wawili kutoka chama cha Democrats cha Marekani hivi karibuni walisema mara kwa mara kuimarisha vizuizi vya biashara dhidi ya China, mambo yanayohusu China yanayoshughulikiwa na bunge la taifa la Marekani yamezidi 40, na mengi kati ya hayo hayahusiani na mambo ya biashara. Marekani katika baadhi ya nyakati inatekeleza sera za kupinga kutoa ruzuku kwa bidhaa za China zinazoingia Marekani, na katika baadhi ya nyakati inatekeleza sera za kupinga kuuza bidhaa kwa bei za chini kupita kiasi, na katika baadhi ya nyakati nyingine sera hizo mbili zinatekelezwa kwa pamoja, vitendo vyote hivyo vimeathiri uhusiano wa biashara ya pande mbili za China na Marekani."

Ili kuboresha mazingira ya biashara duniani na kujenga kanuni za haki za biashara na kuzinufaisha nchi zinazoendelea katika utaratibu wa biashara ya pande nyingi, toka mwaka 2001 WTO ilizindua mazungumzo ya duru la Doha. Hivi sasa mazungumzo ya duru la Doha yalikwama tokea miaka miwili iliyopita, na sasa ni wakati muhimu wa kukwamua mazungumzo hayo. Balozi Sun alisema,

"Tunaihimiza Marekani ioneshe unyumbufu zaidi, kutangulia kupunguza ruzuku ya kilimo na kufungua masoko yake kwa nchi zinazoendelea."