Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-13 20:08:20    
Tumechukua hatua ya kutoa msaada kwa Afrika

cri

Ili kutoa misaada ya kifedha kwa wanafunzi wa Afrika, serikali ya China na vyuo vikuu mbalimbali vya China vilianzisha udhamini maalumu wa masomo kwa wanafunzi kutoka nchi za Afrika. Hivi sasa China inaongeza zaidi idadi ya wanafunzi wanaopewa udhamini wa masomo, ili kuwavutia vijana wengi zaidi kutoka nchi za Afrika kuja kusoma nchini China.

Mwaka 2007 wanafunzi 2,733 wa Afrika walipewa udhamini wa masomo nchini China, na serikali ya China pia itaongeza idadi ya wanafunzi wa Afrika watakaopewa udhamini wa masomo nchini China kufikia elfu nne. Licha ya kuwavutia wanafunzi wa Afrika kusoma nchini China, wizara ya elimu ya China na vyuo vikuu husika pia vinatafuta mfumo wa ushirikiano wa kutuma walimu barani Afrika, na kuanzisha kituo cha msingi cha ushirikiano wa elimu. Mkurugenzi wa ofisi ya Asia na Afrika ya idara ya kimataifa ya wizara ya elimu ya China Bw. Xue Yanqing alisema,

"Mwelekeo wa maendeleo ya ushirikiano kwenye mambo ya elimu kati ya China na Afrika ni namna ya kuisaida kihalisi Afrika katika mambo ya elimu. Kwa mfano kuwa tulianzisha chuo cha ufundi nchini Ethiopia, na nchi nyingine za Afrika mashariki pia zinaweza kujifunza uzoefu kama huo. Tunataka kuhimiza kazi yetu kwa kupitia mfano fulani"

Chuo cha walimu wa uhandisi cha Tianjin ni moja kati ya vyuo vikuu vilivyowekwa hapo awali na wizara ya elimu ya China, chuo hicho kimekuwa kituo cha kutoa msaada wa elimu kwa Afrika, pia ni chuo kilichoanzisha kazi yake mapema barani Afrika. Hadi sasa chuo hicho kilituma walimu 120 kwa jumla nchini Ethiopia na Tanzania, na kutoa mafunzo kwa wanafunzi elfu 10 wa Afrika. Ili kukamilisha mradi wa ushirikiano kati ya China na Afrika, chuo hicho na walimu wake wameshinda matatizo mengi. Mkuu wa chuo hicho Bw. Meng Qingguo alisema,

"Tumechukua hatua ya kutoa msaada kwa Afrika, na wala siyo kutaka kujipatia maslahi. Chuo chetu kimebeba majukumu ya kufanya ushirikiano kwenye mambo ya elimu na nchi za Afrika, maendeleo ya nchi za Afrika yanahitaji watu wenye ujuzi maalumu. Ingawa fedha zetu za msaada si za kutosha, lakini hatutapunguza kazi yetu kutokana na upungufu wa fedha, tutatafuta fedha zaidi kutokana na mahitaji halisi ya msaada kwa ajili ya Afrika."

Mkurugenzi wa ofisi ya mawasiliano ya kimataifa ya chuo cha walimu wa uhandisi cha Tianjin Bw. Xie Chao alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, walimu waliotumwa na chuo hicho barani Afrika wote wana kiwango kizuri cha taaluma, na wanakaribishwa na vyuo vya huko na wanafunzi wa huko. Walimu hao pia wana moyo wa uvumilia wakati wanapokabaliwa na matatizo. Bw. Xie Chao alisema,

"Walimu wetu waligundua mashine kadhaa hazikuweza kufanya kazi, waliyatengeneza hatua kwa hatua. Kutokana na uchafuzi wa maji, walimu wetu waliumwa na miguu, na tulituma dawa barani Afrika."

Juhudi zilizofanywa na serikali ya China na sekta ya elimu, na mafanikio yaliyopatikana katika ushirikiano kwenye mambo ya elimu kati ya China na Afrika yanasifiwa. Hivi sasa serikali ya China, watu wa sekta ya elimu, na wataalamu wa masuala ya uhusiano kati ya China na Afrika, wote wanafanya utafiti na kutafuta njia ya namna ya kuufanya ushirikiano huo uwe na ufanisi zaidi katika siku za baadaye. Naibu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa historia ya Afrika ya China, ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa Afrika katika chuo kikuu cha ualimu cha Shanghai Bw. Shu Yunguo alisema,

"Kwanza, tunapaswa kuongeza ufanisi wa ushirikiano wa elimu kati ya China na Afrika, na kufanya mawasiliano zaidi na upande wa Afrika. Tunapaswa kurekebisha kwa ufanisi mafunzo kutokana na hali halisi. Pili, kila kituo cha msaada kwa Afrika kinapaswa kuonesha sifa na umaalumu wake. Vile vile utafiti wa mambo kuhusu Afrika unapaswa kuendelezwa zaidi, na kuifanya kazi ya utafiti iunge mkono ushirikiano huo."

Imefahamika kuwa wizara ya elimu ya China itaendelea kushikilia sera ya kuwapokea wanafunzi kutoka Afrika kusoma nchini China, na kutuma walimu barani Afrika, pia itafanya makongamano na semina zinazolenga mahitaji halisi ya maendeleo ya Afrika, hatua hizo zitatoa mchango katika kuhimiza maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi mbalimbali barani Afrika.

Wasikilizaji wapendwa mlikuwa mnasikiliza maelezo kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye mambo ya elimu. Kipindi hiki cha Daraja la Urafiki kati ya China na Afrika kwa leo kinaishia hapa. kwaherini!