Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-19 16:42:56    
Maisha ya Bw. Nuttavudh Photisaro mjini Guangzhou

cri

Bw. Photisaro ni konsela wa Thailand mjini Guangzhou, China, zamani aliwahi kuwa konsela wa Thailand nchini Cambodia. Muda wake wa kufanya kazi hapa China haujatimia mwaka mmoja, lakini ameupenda mji huo mzuri.

Guangzhou ni mji mkuu wa mkoa wa Guangdong, China. Hali ya biashara mjini Guangzhou ni motomoto. Bw. Photisaro anaona kuwa, shughuli za biashara mjini humo haziko nyuma ikilinganishwa na miji mingine yote duniani. Alisema,

"Watu wanaoishi mjini Guangzhou, wanakuwa na pilikapilika na wanachapa kazi kila dakika hata kila sekunde. Wafanyabiashara wanaonekana kila mahali, na mambo wanayozungumzia yote yanahusu biashara."

Bw. Photisaro alifahamisha kuwa, kwa kuwa mkoa wa Guangdong uko karibu na Thailand, hivyo una mawasiliano ya karibu na Thailand, na ni mwenzi muhimu wa biashara wa Thailand. Aliona kuwa ongezeko kasi la uchumi wa Guangdong kunahimiza kidhahiri maendeleo ya uchumi na biashara za Thailand. Alisema,

"Mkoa wa Guangdong uko karibu na Thailand, Wa-thailand wengi wenye asili ya China wanatoka miji ya Shantou, Chaozhou ya mkoa wa Guangdong na mji wa Wenchang wa mkoa wa Hainan. Mawasiliano ya uchumi na biashara kati ya mkoa wa Guangdong na Thailand ni ya karibu sana kuliko yale ya miji mingine na Thailand."

Baada ya kwenda Guangdong, Bw. Photisaro alitembelea miji ya Shenzhen, Dongwan, na viwanda vilivyoendelea na viwanda vyenye sayansi na teknolojia ya hali ya juu vya huko vilimshangaza sana. Alisema kuwa ni vigumu kufikiria kuwa miongo kadhaa iliyopita, sehemu hizo bado zilikuwa vijiji vilivyoko nyuma kimaendeleo. Alisema mkoa wa Guangdong unafanikiwa kubadili mfumo wa uchumi wa mpango kuwa mfumo wa uchumi wa soko huria, kuna mambo mengi Thailand inastahili kujifunza. Bw. Photisaro aliona kuwa anapaswa kujulisha uzoefu huo mzuri kwa Thailand, ili kutoa mchango kwa maendeleo ya uchumi wa Thailand.

Licha ya uzoefu wa maendeleo ya uchumi, kitu kingine Bw. Photisaro anataka kuwajulisha watu wa Thailand ni vitoweo. Vyakula vya Guangdong vinaitwa vyakula vya mapishi ya kiguangdong, ni moja ya vyakula vya mapishi manne maarufu ya China. Bw. Photisaro alisema, alipokuwa nchini Thailand alikwenda kwenye mikahawa ya kichina mara kwa mara, na anavyopenda kabisa ni vitoweo vya kiguangdong. Baada ya kuishi mjini Guangzhou kwa muda mrefu, Bw. Photisaro anafurahia utamaduni wenye umaalum wa Guangdong, anapenda kusikiliza muziki za kihongkong na kitaiwan, na kutazama opera ya kiguangdong, vilevile alianza kupenda kukusanya vyombo vya kaure.

Mara moja, serikali ya mji wa Foshan wa Guangdong iliwaalika makonsela wa nchi mbalimbali mjini Guangzhou kutembelea tanuri la kuchoma vyombo vya kaure la Nanfeng lenye historia ya miaka 500, ambalo ni tanuri kale kabisa duniani na linalohifadhiwa vizuri zaidi hata kutumika hadi sasa. Wakati Bw. Photisaro alipoona vyombo vya kaure vilivyotengenezwa kwenye tanuri hilo, alivutiwa sana. Baada ya hapo, Bw. Photisaro anatembelea mara kwa mara viwanda vya utengenezaji wa sanaa za kaure na jumba la makumbusho ya vyombo vya kaure, na kuanza kukusanya vyombo vya kaure.

Bw. Photisaro alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, ingawa haujatimiza mwaka mmoja tangu aanze kufanya kazi hapa China, lakini ameifuatilia China kwa muda mrefu. Kwa kuwa athari ya China katika dunia inaongezeka siku hadi siku, na watu wa Thailand wanaifuatilia China siku hadi siku.

"Katika miaka ya karibuni, vyombo vya habari vya Thailand vimekuwa vinaifuatilia China siku hadi siku, vinafuatilia mabadiliko ya China, kwani mabadiliko ya China yanaiathiri dunia na Thailand."

Bw. Photisaro alisema, zamani Thailand ilinukuu habari za China kutoka kwa shirika la habari la Associated Press, shirika la habari la Reuters au shirika la habari la AFP. Sasa habari kuhusu China zinazotolewa na Thailand ni nyingi. Baadhi ya vyombo vya habari vya Thailand kwa ajili ya kutoa habari zaidi kuhusu China, vinaajiri waandishi wengi wa habari wanaofahamu lugha ya Kichina.

Tatizo kubwa alilokuta nalo Bw. Photisaro wakati alipokuja China ni kutojua lugha ya Kichina. Aliona kuwa akitaka kuwasiliana na Wachina, na kufahamu zaidi China, si rahisi kama hawezi kuongea lugha ya Kichina. Hivyo kutokana na uhimizaji wake, mwezi Agosti mwaka jana, ofisi ya ubalozi mdogo wa Thailand mjini Guangzhou pamoja na Chuo Kikuu cha uchumi na biashara cha lugha za kigeni cha Guangzhou ziliwaalika walimu karibu 100 wa vyuo vikuu wa nchi hizo mbili kujadili utoaji wa mafunzo ya lugha ya Kichina. Hata alipendekeza kuwa, wanafunzi wa Thailand lazima wachukue lugha ya Kichina kuwa somo la lazima.

Bw. Photisaro anasoma magazeti ya lugha ya Kichina, kama anakuta sehemu asiyoelewa, anamwomba katibu wake atafsiri kwa lugha ya Kithailand. Pia anasikiliza na kutazama vipindi vya redio na televisheni vya huko, ili kuifahamu China kwa pande zote. Bw. Photisaro alisema, China inaendelezwa kwa kasi, hasa ni maendeleo ya sayansi na teknolojia. Aliona kuwa, urushaji wa satilaiti ya "Chang'e No.1" ni fahari kwa watu wote wa Asia. Alisema,

"China ni nchi kubwa, iko katika zama mpya za kuelekea kujiunga na nchi nyingine duniani. Naona kuwa, China kurusha 'Chang'e No.1' sio tu ni mafanikio ya China, bali pia ni fahari kwa watu wa Asia. China imekuwa nchi yenye teknolojia ya hali ya juu katika safari za anga ya juu na safari za ndege, na Thailand inataka kunufaika na matokeo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia ya China."

Bw. Photisaro alisema, ili kutekeleza wazo la kujiendeleza kwa njia ya kisayansi, China inatekeleza sera ya kubana matumizi na kupunguza utoaji wa uchafuzi nchini humo, na Thailand inakabiliwa na masuala ya raslimali na mazingira yanayofanana na China katika maendeleo yake. Alieleza matumaini yake kuwa, Thailand na China zitaimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta hizo, ili kutimiza kwa pamoja maendeleo endelevu ya uchumi na jamii.


Idhaa ya kiswahili 2008-06-19