Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-18 20:44:19    
Mapishi ya maharagwe na kamba-mwakaje

cri

Mahitaji

Kamba-mwakaje gramu 200, maharagwe gramu 50, yai moja, chumvi kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, vipande vya vitunguu maji gramu 5 na tangawizi gramu 5

Njia

1. washa moto chemsha maji, baada ya kuchemka, tia maharagwe na chumvi, baada ya dadika 5 yaipue na uyapakue.

2. koroga kamba-mwakaje pamoja na ute wa yai.

3. weka sufuria jikoni, mimina mafuta mpaka yawe nyuzi joto 60, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga, tia kamba mwakaje, korogakoroga, tia mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia, chumvi, korogakoroga, mwisho tia maharagwe korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.