Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-23 18:04:59    
"Mahekalu manane ya sehemu ya nje" ya mji wa Chengde

cri

Hekalu la Puning lililoko mji Chengde, mkoani Hebei, China ni hekalu maarufu ya dini ya kibudha ya kitibet kwenye sehemu ya kaskazini ya China. Hekalu hilo lilijengwa kwenye utawala wa Qianlong wa enzi ya Qing katika karne ya 18. Kwenye sehemu za pembezoni mwake kuna mahekalu mengine 11 yenye mitindo mbalimbali. Mahakelu 8 kati yake yalisimamiwa moja kwa moja na serikali ya Qing katika wakati ule, tena mahekalu hayo yote yako katika sehemu ya nje ya Gubeikou, hivyo yanaitwa "mahekalu manane ya sehemu ya nje". Mwezi Desemba mwaka 1994, "Mahekalu manane ya sehemu ya nje" yaliorodheshwa kuwa mabaki ya utamaduni duniani.

Mahekalu yaliyojengwa mapema zaidi kati ya "Mahekalu manane ya sehemu ya nje" ni hekalu la Furen na hekalu la Fushan, ambayo yalijengwa mwaka 1713. Ofisa wa idara ya usimamizi ya mahekalu hayo ya mji wa Chengde, Bw. Peng Junpo alieleza historia ya mahekalu hayo mawili. Alisema,

"Wakati ule kulikuwa na sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka 60 tangu azaliwe mfalme Kangxi, mabudha hai kutoka mkoa wa Mongolia ya ndani na nchi ya Mongolia walishiriki kwenye sherehe hiyo. Ili kuonesha moyo wake, mfalme Kangxi alijenga mahekalu hayo mawili ya ukoo wa kifalme kwenye sehemu ya Rehe."

Mfalme Kangxi alijenga mahekalu hayo mawili mwaka ule kutokana na mazingira maalumu ya kihistoria na kisiasa. Mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa hekalu la Puning, Bw. Wang Hui alieleza mazingira ya historia ya wakati ule ya umoja wa makabila mbalimbali ya China. Alisema

"Baada ya serikali ya Qing kutawala China, iliona njia nzuri kabisa ya kuimarisha utawala wake ni kuwa na umoja wa makabila. Kwa kuwa sehemu ya Chengde ilikuwa ni sehemu ya malisho kwa wakati ule, na ilikuwa ni sehemu ya kati, kati ya China na sehemu ya makazi ya makabila madogo madogo, ambapo kuna uhusiano mkubwa na mgongano kati ya makabila mbalimbali. Wakati ule watu wa kabila la Wamongolia na kabila la Watibei wote waliamini dini ya kibudha ya kitibet, kwa kuheshimu dini yao na kufuata wazo la dini ya kibudha ya kitibet, mfalme Kangxi alijenga hekalu la Furen na hekalu la Fushan kwa nyakati tofauti."

Baada ya Qianlong kuwa mfalme, aliendelea kufuata utaratibu wa mfalme Kangxi, tena alijenga mahekalu 10 yenye mitindo mbalimbali kwenye sehemu ya Chengde. Hekalu la kwanza kati ya mahekalu 10 yaliyojengwa na mfalme Qianlong ni hekalu la Puning. Hekalu hilo lilijengwa kwa ajili ya kuadhimisha tukio moja kubwa katika historia ya umoja wa makabila ya China. Mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa hekalu la Puning, Bw. Wang Hui alisema,

"hekalu la Puning lilijengwa kwa ajili ya kuadhimisha ushindi wa kutuliza uasi wa Zhungeer, kujenga hekalu ni kama kuweka rekodi ya historia, na pia ni onyo kwa siku za baadaye. Alitarajia kuleta utulivu wa jamii na kuwa salama na tulivu milele baada ya tukio hilo."

Kutulizwa lwa uasi wa Zhungeer aliousema mkurugenzi Wang, ni serikali ya enzi ya Qing kwa nyakati tofauti ilituliza uasi uliofanywa na mtemi wa sehemu ya Zhungeer Mongolia ya Distress Lu Te Dawagi na Aamor Sana kati ya mwaka 1755 na mwaka 1757, na ililinda umoja wa taifa na ukamilifu wa ardhi.

Kutokana na kuwa serikali ya enzi ya Qing iliheshimu dini za makabila madogo madogo na kuweka mbele umoja wa makabila, hekalu la Puning lilikuwa mahali muhimu pa kufanya mawasiliano ya kisiasa na kidini ya moja kwa moja kati ya sehemu mbalimbali za Tibet na Mongolia, pamoja na serikali ya enzi ya Qing. Hekalu la Puning ni lenye mtindo wa kipekee katika usanii wa majengo. Bw. Wang Hui alisema,

"Hekalu la Pungning limegawanyika katika sehemu mbili, sehemu yake ya mbele ilifuata kabisa mpango wa majengo ya mahekalu ya kabila la Wahan, yaani lenye kumbi 7 za Jialan. Lakini kutokea ngazi ya 42 na juu ya ukuta wa King Kong ni Mandala, yaani ni mtindo wa majengo wa dini ya kibudha ya kitibet, na iliunganisha barabara utamaduni wa aina mbili."

Hivi sasa, hekalu la Puning lina watawa 80, kila siku wanajifunza na kusoma vitabu vya dini kwa kufuata ratiba iliyowekwa, wote walipata elimu nzuri ya lugha za Kitibet, Kihan na Kiingereza, tena wanaishi kwa kufuata mila na desturi za makabila yao. Naibu mkuu wa hekalu, mwalimu wa ngazi ya juu wa King Kong, Morigen mwenye umri wa miaka 39 mwaka huu, anasimamia masomo na maisha ya watawa. Alisema,

"Serikali inatuunga mkono sana. Tunafanya kila kitu kwa kufuata utaratibu wa dini ya kibudha. Chakula na makazi yetu ni mazuri kuliko mahekalu mengine. Ingawa hekalu letu hilo ni la dini ya kibudha ya kitibet, lakini pia ni kwa ajili ya umoja wa taifa, mtawa mkuu wa dini ya kibudha ya kihan pia anaalikwa kuja kufanya shughuli za kidini."

Kati ya mahekalu manane ya sehemu ya nje, licha ya hekalu la Puning, kuna mahekalu mawili yanayoonesha umoja wa makabila ya Wahan na Watibet, pamoja na uunganishaji wa usanii wa majengo za kabila la Wahan na kabila la Watibet, hayo ndiyo hekalu la Putuozongcheng na hekalu la Xumifushou. Mfanyakazi wa idara ya usimamizi wa mahekalu manane ya mji wa Chengde, Bw. Li Ran alieleza maana ya majina ya mahekalu hayo mawili, akisema,

"Putuozongcheng ni tafsiri ya kasri ya Potala kwa maneno ya Kihan, hekalu hilo lilijengwa mwaka 1771 kwa ajili ya Dalai Lama, hekalu hilo lilijengwa kwa kuiga mtindo wa kasri ya Potala. Na hekalu la Xumifushou ni tafsiri ya hekalu la Zhashilunbu kwa maneno ya Kihan, hekalu hilo lilijengwa kwa kufuata mtindo wa hekalu la Zhashilunbu la Rikece, Tibet, hekalu hilo ni hekalu la kifalme lililojengwa na mfalme Qian Long kwa ajili ya Panchen Lama."

Hekalu la Putuozongcheng lilijengwa na mfalme Qian Long kwa ajili ya Dalai Lama, ambaye alitarajia kwenda kumwona mfalme, ingawa hatimaye Dalai Lama hakuenda, lakini hekalu hilo limekuwa shahidi wa tukio lingine kubwa katika historia ya umoja wa taifa la China, yaani mwaka 1771 watu wa ukoo wa Torguts wa kabila la Wamongolia wa China waliohamia sehemu ya mtiririko wa chini wa mto Volga, walishindwa kuvumilia ukandamizaji na unyanyasaji wa Urusi ya mfalme Czar, walisafiri umbali mrefu na kukwepa vizuizi vya jeshi la mfalme Czar, na kurejea kwenye maskani ya China.

Hekalu la Xumifushou lilijengwa kwa ajili ya Panchen Lama aliyetarajia kwenda kumwona mfalme Qian Long.

Idhaa ya kiswahili 2008-06-23