Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-23 18:07:50    
Bustani ya utamaduni wa kabila la Wahui mkoani Ningxia

cri

Katika mkoa wa Ningxia, kuna bustani moja maarufu ya kuonesha utamaduni wa kabila la Wahui. Bustani hiyo ilianzishwa mwezi Septemba mwaka 2005, na ni bustani ya pekee nchini China ya kuonesha utamaduni na deturi za kabila la Wahui. Mkuu wa bustani hiyo Bw. Lei Runze alipozungumzia madhumuni ya kuanzisha bustani hiyo, alisema,

"Mkoa wa Ningxia ni sehemu watu wa kabila la Wahui wanayoishi. Idadi ya watu wa kabila la Wahui nchini China ni karibu milioni 10, na kati yao milioni 2.1 wanaishi mkoani Ningxia. Kwa muda mrefu hakukuwa na sehemu ya kuonesha historia na utamaduni wa kabila hilo nchini China, hivyo serikali ya mkoa wa Ningxia ilitenga fedha na kujenga bustani ya kuonesha utamaduni wa kabila la Wahui na jumba la maonesho kwa kabila hilo."

Kutokana na umuhimu wa bustani hiyo, serikali ya mkoa wa Ningxia inetilia maanani sana. Bw. Lei Runze alisema,

"China ni nchi yenye makabila mengi, na miongoni mwa makabila madogo madogo nchini China, kabila la Wahu ni moja kati ya makabila yenye maendeleo zaidi ya uchumi. Chanzo cha utamaduni wa kabila hilo ni utamaduni wa kiislamu na wa enzi ya Han na Tang katika historia ya China. Hivyo kuanzisha bustani ya kuonesha utamaduni huo kunaweza kukidhi mahitaji ya kuelewa utamaduni wa kabila la Wahui."

Bustani ya kuonesha utamaduni wa kabila la Wahui lina eneo la hekta 20, ndani ya bustani hiyo, kuna jumba la makumbusho ya kabila la Wahui, kasri ya uadilifu, kijiji cha kuonesha mila na desturi za kabila hilo, mikahawa na kituo cha maonesho. Jumba la makumbusho ya kabila la Wahui lina umbo la maandishi ya neno la Hui la kichina, na katika jumba hilo, watu wanaweza kuona maelfu ya nyaraka, picha na vitu vingine vinavyohifadhiwa vya kuonesha historia ya kabila la Wahui na utamaduni wa kabila hilo. Katika jumba hilo, kuna vyumba vitano vinavyoonesha mada tano ya asili ya historia na utamaduni wa kabila la Wahui, maendeleo ya utamaduni wa kiislamu, utamaduni na desturi maalumu za kabila la Wahui, michango iliyotolewa na kabila hilo katika historia ya China, kuanzishwa kwa sehemu ya kabila la Wahui la Ningxia na maendeleo na mabadiliko ya sehemu hiyo.

Vitu vingi vya historia vinavyohifadhiwa katika jumba hilo pia ni nyaraka zenye thamani kubwa kwa kuelewa utamaduni wa kiislamu. Mfanyakazi wa jumba hilo kutoka kabila la Wahui Bw. Xu Wei alisema,

"Jumba la makumbusho ya kabila la Wahui linafanya ushirikiano na Shirikisho la Dini la Kiislamu na taasisi za zaburi za dini la Kiislamu. Hivi karibuni, taasisi ya zaburi ya Ningxia iliipa jumba hilo heshima ya kituo cha kuwafundisha wazalendo wa kiislamu, na kuwapeleka masufii wao kulitembelea, ili kuelewa elimu ya utamaduni wa kiislamu.

Jumba la makumbusho ya kabila la Wahui linahifadhi vitu vya aina mbalimbali ya mabaki ya kale ya utamaduni, kitu kidogo ni kama vile kurani yenye ukubwa wa ukucha, na kikubwa ni kama vile njuga kubwa ya kale yenye urefu wa karibu mita miwili. Kati ya vitu hivyo vingi, viwili ni muhimu zaidi, kimoja ni kitabu cha kurani kilichochapishwa enezi wa Ming kuanzia mwaka 1368 hadi mwaka 1683, na hii ni kurani yenye historia ndefu zaidi na iliyohifadhiwa vizuri zaidi mkoani Ningxia, kingine ni modi mbili ya meli za kale za kiarabu na nguo 12 za kiislamu zilizozawadiwa mwaka 2007 na waziri wa sheria, mfuko wa dini na mambo ya kiislamu wa Kuwait Bw. Abdullah Maatouk, na zawadi hizo zimethibitisha mawasiliano ya kirafiki kati ya China na nchi za kiarabu.

Vitu vya mabaki ya historia katika jumba hilo vinawavutia wageni wengi kutoka nchi za nje. Mkuu wa bustani ya kuonesha utamaduni wa kabila la Wahui Bw. Lei Runze alisema,

"Tangu kuzinduliwa kwa jumba la makumbusho ya kabila la Wahui, mabalozi wa nchi mbalimbali za kiislamu zikiwemo Kuwati, Yemen, Iran, Pakistan, na Misri nchini China walilitembelea kwa nyakati tofauti. Walifurahi na kuipongeza China kwa kujenga majengo makubwa ya kiislamu ili kuonesha utamaduni wa kiislamu."

Bw. Lei Runze alisema utamaduni wa kiislamu wa China unaoonekana kwenye jumba hilo unawashangaza maofisa na watu wengine kutoka nchi za kiislamu duniani, walieleza kuwa watafanya ushirikiano na jumba hilo, na kulichangia vitu vya mabaki ya kale ili kutia nuru zaidi kwa jumba hilo la makumbusho. Bw. Lei Runze alisema atashirikiana na wafanyakazi wenzake kuendelea na juhudi za kufanya bustani ya utamaduni wa kabila la Wahui ya Ningxia iwe kituo cha waislamu duniani kufanya mikutano, makongamano na mawasiliano, alisema,

"Madhumuni yetu ya kuanzisha bustani hiyo ni kuwafanya watalii kutoka nchini na nchi za nje waweze kuelewa kabila la Wahui, kukidhi mahitaji yao ya kufahamu utamaduni, desturi, sanaa na historia ya kabila hilo. Hatua yetu ijayo ni kupanua bustani hiyo, na kuifanya iwe kituo cha waislamu wa nchini na nchi za nje kufanya mikutano, makongamano na mawasiliano. Aidha, tunapanga kuanzisha kituo cha mawasiliano ya utamaduni wa kiislamu, shule ya lugha ya kiarabu, ili kutoa sehemu nzuri kwa ajili ya kufanya mawasiliano ya kirafiki kati ya China na nchi za kiislamu. Naona kuwa hatua hizo pia zitanufaisha mkoa wa Ningxiang, na kuifanya ifunguliwe zaidi."

Idhaa ya kiswahili 2008-06-23