Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-25 21:54:11    
Makubaliano ya kusimamisha vita kati ya Israel na Palestina yakumbwa na changamoto mpya

cri

Tarehe 23 na 24 mapambano kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Palestina yalitokea tena katika sehemu ya kusini ya Israel na ukanda wa Ghaza. Haya ni mapambano yaliyotokea baada ya kusimamisha vita kwa miezi 6 tokea makubaliano yalipoanza kutekelezwa. Tarehe 23 jioni, kombora moja lililopigwa kutoka ukanda wa Ghaza lililipuka katika sehemu ya kusini ya Israel. Hili ni tukio la kwanza baada ya makubaliano ya kusimamisha vita kuanza kutekelezwa. Tarehe 24 alfajiri mapema jeshi la Israel lilichukua hatua za kijeshi katika mji wa Nablus, mji uliopo kwenye ukingo wa magharibi wa mto wa Jordan na liliwaua askari wawili wa Kundi la Jihad. Ingawa kwenye makubaliano ya kusimamisha vita hakuna vifungu vya kuzuia jeshi la Israel kuchukua hatua za kijeshi katika sehemu ya ukingo wa magharibi wa mto wa Jordan, lakini kabla ya makubaliano Kundi la Jihad liliwahi kuonya kwamba kama Israel likishambulia watu wake walioko kwenye ukingo wa magahribi wa mto wa Jordan, Kundi hilo litalipiza kisasi, na kweli kama lilivyosema, alasiri ya siku hiyo hiyo Kundi la Jihad lilirusha makombora matatu kwenye sehemu ya kusini ya Israel.

Matukio hayo yamesababisha hali ya wasiwasi kati ya Israel na wanamgambo wa Palestina. Waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Olmert alishutumu mashambulizi hayo kuwa ni kitendo cha kuharibu moja kwa moja makubaliano ya kusimamisha vita, na Israel itachukua hatua. Msemaji wa Kundi la Hamas linalodhibiti ukanda wa Ghaza Bw. Sami Abu Zuhri alisisitiza kwamba Kundi la Hamas litaendelea kuheshimu makubaliano, na Kundi la Jihad pia lilisema lina matumaini kwamba watu wa Palestina wataendelea kufurahia utulivu baada ya vita kusimamishwa, kwa hiyo halitachukua hatua nyingine, hata hivyo kama Israel itaendelea kuchukua hatua za kijeshi, kundi hilo hakika litalipiza kisasi kwa kiwango kikubwa zaidi.

Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na "masharti ya kipindi" kwenye makubaliano ya kusimamisha vita na mahitaji ya Israel na mahitaji ya pande mbili, kusimamisha vita kunazinufaisha pande zote mbili. Kwa mujibu wa makubaliano, Israel na makundi ya kisiasa ya Palestina kwanza yasimamishe vita kwenye ukanda wa Gaza, kama hali itakuwa nzuri, baada ya siku kadhaa Israel itafungua forodha iliyo karibu na ukanda wa Ghaza ili mizigo mingi zaidi ipelekwe kwenye ukanda wa Ghaza. Hivi sasa vipindi viwili vya mwanzo kwenye makubaliano vimepita shwari. Tarehe 24 Rais Hosni Mubarak wa Misri alipokutana na waziri mkuu wa Israe aliahidi kwamba suala la kumwachia huru askari wa Israel Gilad Shalit aliyetekwa nyara na kundi la Hamas limepiga hatua kubwa. Hivi sasa hali ya kutokuwa na vita inaweza kutarajiwa. Lakini makubaliano ya kusimamisha vita bado yanakabiliwa na changamoto.

Kwanza kuna makundi mbalimbali ya Palestina, na kila moja linatetea maslahi yake. Kwa mfano Kundi la Hamas litakubali au la kulingana na manufaa ya shughuli zake za magendo ya silaha, ambazo ni muhimu sana kwa ajili ya kuimarisha nguvu zake za kijeshi.

Pili hali ya kisiasa nchini Israel ni ya wasiwasi, tarehe 24 vyama vya leba na Meretz vilisisitiza kuunga mkono kuvunja bunge na kutaka waziri mkuu aondoke madarakani, na chama cha Beiteinu kinaona kwamba kusimamisha vita kunamaanisha kusalimu amri kwa wanamgambo wa Kundi ya Hamas na makundi mengine. Tarehe 25 bunge la Israel litapiga kura kuhusu ushauri wa kuvunja bunge uliotolewa na wabunge wa chama cha upinzani cha Likud, na matokeo yake yataathiri moja kwa moja hali ya utawala wa serikali ya sasa. Wachambuzi wanaona kuwa hali ya makubaliano ya kusimamisha vita ni dhaifu.