Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-27 10:05:42    
Watanzania wanafuatilia Michezo ya Olimpiki ya Beijing

cri

Kabla ya kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini China, Bw. Mapuli alielewa hali chache kuhusu China.

Mwaka 2006 Bw. Mapuli aliteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini China, maisha yake mjini Beijing yalibadilisha maoni yake ya mwanzo kuhusu China.

Bw. Mapuli aliona kuwa baada ya Beijing kukubaliwa kuwa mwenyeji wa kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Beijing tarehe 13 mwezi Julai mwaka 2001, mabadiliko makubwa zaidi yametokea mjini Beijing, ambapo maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing yanapata maendeleo siku hadi siku.

Upo urafiki wa kijadi kati ya China na Tanzania, licha ya mambo ya siasa na uchumi, nchi hizo mbili zinafanya ushirikiano kwenye mambo ya michezo. Kwa mfano China iliisaidia Tanzania kujenga uwanja wa michezo wa Amani wa Zanzibar na uwanja mpya wa michezo wa taifa mjini Dar es Salam. Bw. Mapuli alisema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye michezo utahimiza zaidi maelewano kati ya wananchi wao, na kuufanya urafiki kati ya nchi hizo mbili uwe urafiki kati ya wananchi wao.

Kwenye shughuli za mbio za mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, Tanzania ni nchi pekee barani Afrika iliyochaguliwa na kamati ya maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing kushiriki kwenye mbio za kukimbiza mwenge. Mbio za mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing zilifanyika kwa mafanikio makubwa mjini Dar es Salam, na mwenge huo ulikaribishwa sana na watu wa huko. Bw. Mapuli alisema kufanyika kwa mafanikio kwa mbio za kukimbiza kwa kupokezana mwenge wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing nchini Tanzania kulionesha urafiki wa jadi kati ya China na Tanzania na China na Afrika.

Watanzania wanapenda michezo, watafuatilia Michezo ya Olimpiki ya Beijing kwa vyombo mbalimbali vya habari na njia mbalimbali. Watafuatilia michezo ya Olimpiki ya Beijing, pia wanafuatilia utamaduni wa China.

Idhaa ya kiswahili 2008-06-27