Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-06-30 20:33:31    
Ziwa Xihu pamoja na chai ya Longjing

cri

Ziwa Xihu la mji wa Hangzhou linajulikana sana duniani, watu hulihusisha ziwa hilo pamoja na ziwa Geneva la Uswisi, na kuyasema kama ni lulu mbili zinazong'ara duniani. Katika kipindi hiki cha leo tutawafahamisha kuhsu Ziwa Xihu na chai ya Longjing.

Mji wa Hangzhou ulijengwa zaidi ya miaka 2,200 iliyopita, ambao ni moja ya chimbuko za utamaduni wa China. Hangzhou pia ilikuwa mji mkuu wa enzi mbili katika historia ya China, na ni moja kati ya miji 7 ya kale ya China. Katika karne ya 13, mtalii mkubwa wa Italia, Bw. Marco Polo aliwahi kutembelea Hangzhou, na kuutaja mji huo kuwa ni mji wa peponi, na kuusifu kuwa ni "mji mzuri adimu zaidi wa duniani".

Watu wengi wanaupenda mji wa Hangzhou kutokana na mandhari nzuri ya Ziwa Xihu, ziwa hilo pia ni kiini cha uzuri wa mji wa Hangzhou, iwe siku nzuri yenye jua au ya kunyesha mvua, au katika kila moja ya majira manne ya mwaka, Hangzhou ina sura nzuri. Kwa hiyo, watu husema, "nchini China kuna maziwa 36 yanayoitwa maziwa ya xihu, lakini zuri zaidi ni ziwa Xihu la Hangzhou." Sehemu ya Ziwa hilo ina vivutio vingi. Ziwa hilo lina mlima mmoja, kingo mbili na visiwa vitatu. Mlima wake unaitwa "mlima wa kipekee", ambao unaonekana kama ni taji la maua linalopendeza. "Kingo mbili" ni ukingo mweupe na ukingo wa Su, ambapo maua mazuri ya kupendeza yanachanua katika majira yote manne ya mwaka. Toka zamani, watu wanasema Ziwa Xihu lina vivutio kumi, ambavyo vingine viko kwenye mlima wa ziwani, na baadhi ya vingine viko kwenye kando za ziwa, vivutio hivyo vinaungana pamoja na kupendeza sana katika majira yote manne ya mwaka.

Tokea mwezi Machi mwaka uliopita, watalii waliotembelea Ziwa Xihu wakati wa mchana, waliweza kuona mchezo uliochezwa kwenye Ziwa Xihu wakati wa usiku. "Picha waliyopata watu kuhusu Ziwa Xihu" ni maonesho makubwa ya mchezo kuhusu hadithi za jadi za kale unaochezwa kwenye mandhari halisi ya mlima na ziwa, ambayo ilionyesha "mvua ya Ziwa la Magharibi" iliyotengenezwa kwa teknolojia ya sayansi ya kisasa, na kuonesha uzuri wa kimaumbile wa Ziwa Xihu lililoko katika mvua, na mvua ya Ziwa Xihu.

Mji wa Hangzhou ni mahali penye milima na mito ya kupendeza, na pia ni mahali penye rasilimali nyingi za kilimo na madini. Moja ya mazao maalumu ya Ziwa Xihu ni chai ya Longjing inavyojulikana sana duniani, chai hiyo ilionekana katika enzi ya Tang, imekuwa na historia ndefu, katika kitabu cha kwanza cha duniani kuhusu chai kilichoandikwa na mtaalamu wa chai Lu Yu, kuna habari kuhusu chai iliyozalishwa kwenye sehemu ya Tianzhu na mahekalu mawili ya Linyin ya Hangzhou. Nchini China kuna hadithi nyingi za jadi kuhusu chai ya Longjing, mfanyakazi wa jumba la makumbusho ya chai Gao Hong alisema,

"Mfalme Qian Long wa enzi ya Qing alikuwa mtoto anawayependa sana wazazi wake, alipofahamu kuwa mama yake ni mgonjwa, alikuwa na wasiwasi mkubwa, wakati ule aliweka jani moja alilochuma katika kitabu alichosoma, akaenda nalo. Wakati kitabu kilipofunguliwa, harufu nzuri ya chai ilitoka, mama yake alisema, alipona kutokana na harufu hiyo nzuri, hivyo mfalme Qian Long aliagiza, majani ya miti hiyo 18 sharti yapelekwe kwenye jumba la mfalme. Jani hilo lilikuwa bapa baada ya kubanwa katika kitabu, hivyo tokea hapo majani ya michai ya Longjing baada ya kuchumwa, yanakaangwa kwenye sufuria na kuwa na umbo la bapa kabisa."

Sifa ya chai ya Longjing inatokana na ufundi mkubwa wa utengenezaji, njia ya kukaanga majani ya Longjing siyo kazi rahisi, watu walioangalia kazi ya utengenezaji wa chai ya Longjing, wanaona kuwa chai ya Longjing kweli ni kitu cha sanaa ya mikono. Chai hiyo ina rangi ya kijani, harufu nzuri na ni moja ya aina maarufu za chai ya China. Kwenye eneo la mandhari ya Ziwa Xihu kuna mikahawa mingi ya chai, ni jambo la kufurahisha sana kwa mtalii huku anaburudishwa na vivutio vya Ziwa Xihu huku anatafuta nafasi kwenda kunywa chai ya Longjing.

Michai ya Longjing ya Ziwa Xihu inaota kwenye milima iliyoko pembezoni mwa Ziwa Xihu, sifa ya chai hiyo inahusiana sana na mazingira ya maumbile ya huko, hali ya hewa ya sehemu ya kijiji cha Longjing si joto wala si baridi, sehemu hiyo pia ina mvua nyingi, tena kiasi cha mvua inayonyesha katika kila mwezi karibu ni sawa, licha ya hayo, udongo wake una mchanga mwingi na ni laini, ni rahisi kutoka kwa maji na inafaa kwa ukuaji wa michai. Sifa ya chai huwa ni tofauti kwa majani ya michai yaliyochumwa katika majira mawili. Majani ya michai yaliyochumwa kabla ya tarehe 5 mwezi Aprili ni mazuri zaidi, kwa kufuata ni majani yaliyochumwa kabla ya siku ya Guyu, ambayo yanaitwa "Chai ya Spring ya pili".

Chai ya Longjing husifiwa kwa sifa zake, "rangi ya kijani, harufu nzuri, ladha tamu na umbo zuri". Wakati wa kutengeneza chai ya Longjing, inatakiwa kutia majani ya chai kwenye glasi, kisha kumimina maji moto, hapo tunaweza kuona majani ya chai yanayoelea juu kwenye maji, namna yake ni ya kupendeza sana. Mhudumu wa mkhahawa wa chai, dada Xu Zemei alikua kwenye sehemu ya kuzalisha chai, na alijifunza kutengeneza chai tokea utotoni mwake, anapenda sana majani ya chai, alisema,

"Kitu muhimu sana katika kutengeneza chai ya rangi ya kijani ni kumimina maji moto katika glasi moja kwa mara tatu, kumimina maji kwa mara tatu, kunafanya majani ya chai yalowe kabisa na maji moto, tena ni kuonesha heshima kwa mgeni kama kumwinamia kichwa mara tatu, tena ni kumimina maji moto hadi kufikia kiasi cha 70% ya glasi."

Kila mwaka kabla ya siku ya Qingming na siku ya Guyu kwa kalenda ya kichina, watalii wengi huvutiwa na wakulima waliokuwa wakichuma majani ya chai, na kukaanga majani ya chai, ambapo harufu nzuri ya chai inajaa. Bw. Kiraz Perincek, ni mtalii aliyetoka Uturuki, nchi yake ni nchi inayolima sana zao la chai, na watu wengi wa nchi hiyo wanatumia chai. Alijiburudisha kwa chai ya Longjing huku akuwa anaangalia mandhari ya Ziwa Xihu. Aliimba wimbo wa chai wa kwao, akisema,

"Hapa Hangzhou nimejua kuwa wachina badala ya kusema kunywa chai, wanasema kuonja chai, ninapotembelea hapa, pia ni kujiburudisha kwa mji huo, si mandhari ya kimaumbile tu, bali pia kwa utamaduni wake."

Chai ya Longjing imekuwa na historia ndefu sana hapa China, sifa yake nzuri kwanza ni kutokana na uzuri wa chai ya Longjing, pili ni kutokana na chimbuko la historia na utamaduni wake. Kwa hiyo, chai ya Longjing si kama tu ina thamani ya chai peke yake, bali pia ina thamani ya sanaa na utamaduni.