Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-01 10:36:51    
Mkoa wa Hainan wapata mafanikio makubwa katika kazi ya kuhifadhi mazingira.

cri

Mkoa wa Hainan umesifiwa kuwa bustani wa mwaka mzima nchini China. Mwaka 2007 eneo linalofunikwa na miti mkoani humo lilikuwa zaidi ya asilimia 57, ambayo ni mara tatu ya wastani wa kiasi hicho nchini China. Mkoani humo kuna bustani 8 za misitu za ngazi ya kitaifa na hifadhi 69 za maumbile. Robo ya eneo la mkoa huo ni hifadhi ya mazingira ya viumbe ya kitaifa. Wakati uchumi wake unapopata maendeleo ya haraka, mkoa huo unahakikisha mazingira mazuri zaidi ya viumbe.

Habari zinasema mkoa wa Hainan ulitangua kuanzisha ujenzi wa mkoa unaohifadhi mazingira ya viumbe nchini China mwaka 1999, na mwaka 2007 ulitoa mpango wa kimkakati kuhusu shughuli hizo. Naibu mkurugenzi wa idara ya maendeleo na mageuzi ya Hainan Bw. Zhu Yunshan alisema, mazingira mazuri ya viumbe ni msingi wa maendeleo endelevu ya mko huo, pia ni sifa na fursa za mkoa huo, alisema,

"Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya mkoa wetu zimetambua kuwa ni lazima mazingira ya viumbe ya mkoa huo yahifadhiwe vizuri. Hayo ni matakwa ya kwanza ya maendeleo endelevu ya mkoa wetu. Wakati mkoa wetu unapoendeleza viwanda umezingatia zaidi kuendeleza viwanda visivyo na uchafuzi, na kujenga miradi mikubwa ya viwanda ambayo haitaharibu mazingira na maliasili na haitakuwa miradi ya marudio. Tumetunga mpango, na kuongoza ujenzi wa viwanda, na serikali na jamii zinasimamia kwa makini vitendo vya viwanda, tunaweza kudhibiti uchafuzi kwenye kiwango cha chini zaidi."

Alisema serikali kwenye ngazi mbalimbali mkoani Hainan inadhibiti kwa makini miradi kutoka nje. Inaidhinisha makampuni yenye vifaa vya kisasa kutoka nje ambayo yanawajibika kwa jamii yaende kuanzisha ujenzi wa miradi mikubwa, ili kusaidia kudhibiti uchafuzi. Mkoa wa Hainan pia umetunga mpango kuhusu shughuli za sehemu mbalimbali mkoani humo kwa mujibu wa mazingira ya kijiografia. Sehemu ya kusini inashughulikia utalii na ujenzi wa nyumba, kwenye maeneo ya uendelezaji wa shughuli ya Yangpu na Dongfang yaliyoko kusini mwa mkoa huo kuna makampuni makubwa na miradi ya viwanda. Sehemu ya kati ya milimani yanashughulikia uhifadhi wa mazingira mazuri ya viumbe. Bw. Zhu Yunshan alidokeza kuwa serikali imeongeza nguvu kutoa ruzuku kwa shughuli za kuhifadhi mazingira za viumbe kwenye sehemu ya kati, alisema,

"Tunahitaji kuendelea kuanzisha na kukamilisha utaratibu wa kutoa ruzuku kwa sehemu zinazoshughulikia uhifadhi wa mazingira ya viumbe. Misitu mingi ya tropiki iko kwenye sehemu ya kati, tunahitaji kuwahimiza wakazi wa huko wahifadhi mazingira ya huko kwa hiari, bali pia tutaboresha maisha ya wakazi wa huko mijini na vijijini, kuimarisha ujenzi wa miundo mbinu, na kuendeleza kilimo na utalii wenye sifa ya kipekee."

Habari zinasema serikali ya mkoa wa Hainan ulianzisha utaratibu wa wajibu wa uhifadhi wa mazingira, kuchukua shughuli za kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira kuwa vigezo vya kupima kazi za maofisa, na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwa hatua mbalimbali zikiwemo kutunga sheria na mipango, kutathimini hali ya mazingira, kutenga fedha na kutekeleza sheria. Mkoa wa Hainan ulichukulia kazi ya kuendeleza kilimo cha mazao ya kitropiki kuwa moja ya mikakati ya kiuchumi, na kuendeleza ufundi wa kuhifadhi mazingira kwenye uzalishaji wa kilimo. Wilaya ya Chengmai ni moja kati ya wilaya muhimu za uzalishaji wa kilimo nchini China. mkuu wa wilaya hiyo Bw. Yang Sitao alisema mkoa wa Hainan uliendeleza kilimo kinachohifadhi mazingira ya viumbe mapema zaidi, katika matumizi ya mbolea wa viumbe na ujenzi wa mashimo ya gesi ya kinyesi, kwango cha mkoa huo kiko cha juu nchini China alisema,

"Shughuli zinazohifadhi mazingira zina msingi imara mkoani Hainan, maofisa na wakazi wanatilia maanani kuhifadhi mazingira. Tukitaka kujenga mkoa unaohifadhi mazingira ya viumbe, ni lazima tutoe kipaumbele uhifadhi wa mazingira tunapofanya kazi mbalimbali ikiwemo kilimo. Mkoa wetu uliendeleza kilimo kinachohifadhi mazingira mapema zaidi. Mimea inastawi mwaka mzima hapa, hivyo ni rahisi kuzalisha mbolea wa viumbe. Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China na serikali ya mkoa wa Hainan zinafanya juhudi kubwa kueneza ujenzi wa mashimo ya gesi ya kinyesi, ambayo si kama tu yanaweza kutatua suala la nishati, bali pia yanaweza kuzalisha mbolea wa viumbe. Kiasi cha matumizi ya gesi ya kinyesi hapa ni kikubwa zaidi nchini China."

Wakati huo huo, mazingira na hali ya maisha ya kilimo vijijini inaboreshwa siku hadi siku. Mwaka 2000 mkoa huo ulianza kujenga vijiji vinavyohifadhi mazingira. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2007, vijiji zaidi ya elfu 7 vinavyohifadhi mazingira vimejengwa mkoani humo, ambavyo vinachukua tatu kwa kumi ya vijiji vyote mkoani huomo. Kijiji cha Xinghui cha wilaya ya Chengmai ni kimoja kati ya vijiji hivyo. Kijiji hicho kina miti mingi, hewa safi na mazingira mazuri, ambacho kimewavutia wakazi wengi wa mijini kupitisha likizo zao. Wanakijiji wa huko walianzisha mahoteli kwenye nyumba zao.

Mwanakijiji wa kijiji hicho Bi. Wang Lifen alisema kijiji hicho kikiungwa mkono na serikali, kilitenga yuan laki 6 kujenga miundo mbinu na kuboresha mazingira. Baada ya mazingira kuboreshwa, idadi ya watalii imeongezeka, na mapato ya wakulima pia yameongezeka. Alisema,

"Watalii wengi wa mijini na kutoka mikoa mingine wanakuja hapa kutembelea kijiji chetu, kula samaki na matunda ya sehemu ya tropiki, na kujionea uzalishaji na maisha yetu. Kujenga kijiji kinachohifadhi mazingira kumetupatia manufaa mengi, maisha yetu ni mazuri zaidi kuliko zamani, na mazingira yameboreshwa."

Mpango uliotungwa na serikali ya mkoa wa Hainan unaonesha kuwa, mkoa huo utaendelea kuimarisha kazi ya kulinda na kusimamia hifadhi za mazingira ya kimaumbile, maeneo ya mazingira ya viumbe, vyanzo vya maji na bahari, kuendelea kuongeza eneo linalofunikwa na miti, na kutenga fedha nyingi katika uhifadhi wa mazingira. Wakati mkoa huo unapotunga mpango wa maendeleo ya viwanda, kuwavutia wawekezaji na kutoa uidhinishaji kwa miradi, utaimarisha wazo la kubana matumizi ya maliasili na kuhifadhi mazingira, kuacha njia ya maendeleo yanayotumia ovyo maliasili nyingi, na kutafuta maendeleo makubwa ya kiuchumi kwa kubana matumizi ya maliasili na kutochafua mazingira kadri iwezekanavyo.