Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-01 20:47:47    
Barua za wasikilizaji 0701

cri

Msikilizaji wetu Mbarouk Msabaha Mbarouk ametutumia barua pepe yenye kichwa kisemacho: "Kufaulu kwa mbio za mwenge wa Michezo ya Olimpiki mkoani Tibet, China ni jibu mwafaka kwa wachochezi!!!". Bw. Mbarouk alisema katika barua hiyo kuwa, Kwanza kabisa ningependa kuyapongeza mapokezi mazuri ya mbio za mwenge wa Olimpiki uliokimbizwa katika Jimbo la Tibet nchini Jamhuri ya Watu wa China mwezi June mwaka huu , kwa kweli mapokezi hayo ya mwenge wa Olimpiki yanadhihirisha jinsi gani choko choko na fitiza na baadhi ya watu kutaka kuchafuwa sifa za Michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Beijing mwezi August mwaka huu zimeshindwa kufuwa dafu.

Ni wazi kabisa Wananchi wote wa China wenye uchungu na imani na nchi yao wamekuwa wakiunga mkono kwa dhati Serikali yao katika kufanikisha tamasha hilo la Michezo ya Kimatifa , ili liweze kufanyika nchini mwao katika hali ya amani , upendo na mafanikio makubwa , kwani huko kunaweza kuhesabaiwa kama ni fahari kubwa kwa Wachina wote.

Kwa maoni yangu binafsi kufaulu vyema kwa mbio za mwenge wa Olimpiki jimboni Tibet kunatosha kuwa ni jibu muwafaka kwa wale wote waliojaribu kulivalia njuga sana swala la kuchochea michafuko ya kisiasa katika jimbo hilo dhidi ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kutumia kisingizio cha Michezo ya Olimpiki.

Msikilizaji wetu Mogire O Machuki wa sanduku la posta 646 Kisii Kenya ambaye anajidai kuwa ni Bingwa wa salamu Afrika mashariki na kati ametuletea barua pepe kwa mpendwa mtangazaji wa Radio China Kimataifa anasema, zangu za kila la kheri ziwafikie

James Bosire Makori, Joseph Miroro, Rebecca Kwamboka, William Mekenye, Jane Kerubo Mekenye, Nicholas Mokaya Magasi, Philip Machuki, Kefa O Gichana wote wa Kisii Kenya;

Xavierl Telly Wambwa na Mtanda Ayub Sharrif wakiwa Bungoma Kenya;

Ras Franz Manko Ngogo, Zakaria Ndemfoo, Hussein Mirachi, Bob Shega wa Shega, Mitwe S Mitwe, Bw. na Bibi Maganga S.Maganga, Paroko wa Paroko, Kaziro Dutwa, Ghulam Hajji Karimu, Emmanuel S Kapela, Liz Richie na Mtoto Happyness Julius wote wa Sehemu mbalimbali za Tanzania;

Rukia H Mohammed na Mbarouk Msabaha, Alli Ghassani wakiwa Dubai;

Arthur Nyirongo wa Kaporo Malawi;

Ongole Charles John wa Uganda wote nawasihi waendelee kuitegea sikio Radio China Kimataifa CRI.

Na msikilizaji wetu Maulidi Waziri Tangula wa sanduku la posta 24 Kihonda Morogoro Tanzania ametuletea barua pepe akiwatakia kheri na Baraka wafuatao:

Mke wangu mpenzi Mary Kingalu (Barafu wa moyo wangu), Waziri Mauliddi Waziri Tangula, Mchana J Mchana, Onesmo Mponda, Mr. Kong'olo, Kea Joshua Kea wa Morogoro mjini;

Juma Iddi Issa, Eliakimu Ndalukoba, Kaziro Dutwa popote Tanzania;

Kasimu Abedi Ngea wa Lindi, Juma Magimba wa Libya, Saida Miro wa Misri , Mkungilwa Shindano, Emanueli Mwintanga, Hellena Apele Andeka na Ram Apele Andeka wa Kenya;

Daudi Kikosti, Joseph Ngonyani, Veneranda Malima, Rosse Malima, Mama Amina Midundulu, Awadhi Midundulu, Asiat Dammbaya, Joyce Andrea, Mwajuma Kisoto, Rosina Hamidee, Mama Urasa wa Dar es Salaam;

Saimon Dagila, Raimondi Simbo Masawe wa Moshi.

Ujumbe wake unasema, chanzo cha uovu wote ni kupenda fedha, jihadhali pesa isiwe kama Mungu wako.