Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-02 20:35:01    
Mapishi ya supu ya paja la bata na mwani

cri

Mahitaji:

Mapaja mawili ya bata, mwani grami 20, mahindi gramu 50, maharagwe mabichi gramu 50, chumvi vijiko viwili

Njia:

1. osha mapaja ya bata, halafu chemsha maji ukisha tia mapaja ya bata kwenye maji, ili kuondoa damu, halafu yapakue.

2. osha mwani halafu ukate uwe vipande, kata maharagwe mabichi yawe vipande, kata mahindi yawe vipande.

3. chemsha maji, halafu tia mapaja ya bata, vipande vya mahindi, maharagwe mabichi, baada ya dakika 20, punguza moto, tia mwani, endelea kuchemsha kwa saa mbili, baadaye tia chumvi, korogakoroga. Ikiiva, ipua na hapo supu inakuwa tayari kwa kunywa.