Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-03 20:03:15    
Filamu ya "Mali za Urithi za Dunia Nchini China" yaanza kuoneshwa

cri

Wakati Michezo ya Olimpiki ya Beijing inapokaribia, filamu ya "Mali za Urithi za Dunia Nchini China" imeanza kuoneshwa. Hii ni filamu ya kwanza inayoeleza kirefu mali za urithi wa mabaki ya utamaduni na sehemu za asili nchini China.

Upigaji wa filamu hiyo yenye sehemu 28 ulichukua miaka 7 kukamilika, mali za urithi zinazoelezwa ndani ya filamu hiyo ni pamoja na mabaki 33 ya sehemu za asili , mabaki ya utamaduni na utamaduni usioonekana, ambazo zimeorodheshwa na Shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kwenye "Orodha ya mali za Urithi za Dunia". Filamu hiyo licha ya kuonesha mandhari nzuri ya sehemu za asili, utamaduni unaong'ara wa China wenye histoira ya miaka elfu 5, na pia imeonesha mila na desturi za watu wa makabila 56, na nyimbo na ngoma za kiasili za kikabila za China.

 

Mfilamu ya mali za urithi wa mabaki ya utamaduni na mabaki ya sehemu za kimaumbile nchini China ni kama muhtasari wa utamaduni wenye historia ndefu wa China. Mlima Taishan ulioko katika sehemu ya mashariki ya China ulikuwa ni mlima wa kuabudiwa na wafalme katika jamii ya kimwinyi yenye miaka zaidi ya 2,000 nchini China na pia ulikuwa ni mahali kwa wasanii na wasomi kupata msukumo wa utunzi. Sentensi ya kishairi isemayo "Milima yote yaonekana midogo ukiwa kwenye kilele cha Mlima Taishan" imeonesha wazi urefu mkubwa wa mlima huo; Ukuta Mkuu uliojengwa kabla ya miaka 2000 iliyopita una urefu wa kilomita zaidi ya 6000 kaskazini mwa China. Huu ulikuwa mradi mkubwa zaidi wa ujenzi duniani na umechukuliwa kuwa ni alama ya taifa la China; Mapango ya Mogao katika sehemu ya Dunhuang mkoani Gansu, magharibi mwa China, yalichongwa kwa miaka zaidi ya elfu moja, ni hazina kubwa ya dini ya Kibudha kutokana na picha na sanamu zilizochongwa ndani ya mapango yapatayo mia kadhaa, na sanaa hizo zimekuwa elimu ya "taaluma ya Dunhuang" duniani.

Mali za Urithi wa utamaduni usioonekana ni pamoja na opera ya Kunqu yenye historia ya miaka zaidi ya 600, "Usanii wa Mukamu Mkoani Xinjiang" inayokusanya muziki na ngoma, ala ya muziki yenye nyuzi saba Guqin katika zama za kale nchini China, yote hayo yameonesha utamaduni mkubwa wenye historia ndefu ya China.

 

Filamu hiyo ilitengenezwa kwa muda wa miaka saba. Ili kukamilisha filamu hiyo, kikundi cha kupiga filamu hiyo kilisafiri kilomita laki moja na kuzungumza na wataalamu zaidi ya 300, kilipiga kutoka angani, ardhini na majini na mwishowe kimekamilisha filamu hiyo yenye muda wa saa zaidi ya 40. Hii ni filamu iliyo ndefu sana katika historia ya matengenezo ya filamu ya rikodi nchini China. Mtengenezaji mkuu wa filamu hiyo Bw. Guan Hui alisema,

"Mandhari nzuri ikipigwa kwa teknolojia ya kawaida haitavutia sana watazamaji, kwa hiyo tulitumia teknolojia ya juu kupiga filamu hiyo kwani tunataka kuwafurahisha watazamaji kwa mandhari nzuri ya mito na milima na huku wanafahamishwa utamaduni mkubwa wa China."

Licha ya kufurahisha watazamaji, filamu hiyo pia imezingatia kuwawezesha watu waongeze ufahamu wa kuthamini na kuhifadhi mali zetu za urithi. Mlima Qingcheng katika mji wa Dujiangyan ambao pia ni mali ya urithi ya dunia, tarehe 12 Mei mlima huo uliharibiwa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi. Kituo cha televisheni tarehe 16 kilipoanza kuonesha filamu hiyo, kwa makusudi kilionesha mlima huo mwanzoni kabisa.

 

Naibu mkurugenzi wa Kituo Kikuu cha Televisheni cha China Bw. Gao Feng alisema, kupiga filamu ya kurikodi mabaki ya kale kwa picha safi ni njia nzuri ya kuhifadhi mali za urithi wa utamaduni, na wakati mali za urithi zilipoharibiwa, filamu hiyo ina thamani kubwa zaidi. Alisema,

"Katika siku za kawaida tunapoangalia Mlima Qingcheng mjini Dujiangyan tunaona tu mandhari ni nzuri, lakini baada ya kuharibiwa na kutoweka kwa mali hiyo, tunaumizwa rohoni, hii ndio maana ya filamu yetu. Sisi tunahifadhi mali za urithi wa utamaduni kwa filamu yetu, watazamaji wanazithamini na kuhifadhi kwa kuangalia filamu yetu. Kutunza na kuzifanyia matangazo mali zetu za urithi wa utamaduni ni jukumu la kila Mchina."

 

Mshiriki wa upigaji wa filamu hiyo, mkurugenzi wa kampuni ya Japan China's Story INC Bw. Kentaro Tsvjita alisema kampuni yake itatumia kila njia kueneza filamu hiyo nchini Japan na duniani, anaona kuwa filamu hiyo inafaa sana kuwa kitabu cha kufundishia utamaduni wa China. Alisema,

"Filamu hiyo licha ya kuonesha mandhari nzuri ya milima na mito nchini China na pia imeonesha ushupavu wa China wa kujiimarisha baada ya uharibifu wa tetemeko la ardhi. Hii ni filamu nzuri ya kuueleza na kuuenzi utamaduni unaong'ara wa China."