Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-04 21:22:05    
Lebanon na Israel kubadilishana mateka

cri

Katibu mkuu wa Chama cha Hezbollah cha Lebanon Bw. Hassan Nasrallah tarhe 2 alipozungumza na waandishi wa habari alithibitisha kuwa chama chake kitabadilishana mateka na Israel ndani ya wiki mbili zijazo. Kwenye mkutano na waandishi wa habari Bw. Nasrallah alitangaza kuwa Israel itawaachia huru mateka wa kivita wa Lebanon walioongozwa na Samir Kantar na kukabidhi miili ya mateka wa Lebanon na nchi nyingine za Kiarabu, na kuwaachia huru askari wawili Eldad Regev na Ehud Goldwasser wa Israel waliotekwa na Hezbollah mwaka 2006 na kutoa maelezo kuhusu rubani wa Israel aliyetekwa nyara mwaka 1986. Bw. Nasrallah alisema pande mbili zitabadilishana mateka wa kivita baada au kabla ya tarehe 15.

Mazungumzo kati ya Chama cha Hezbollah na Israel kuhusu suala la mateka yalifanyika faraghani. Bw. Nasrallah alidokeza kuwa tangu vita kati ya Lebanon na Israel vimalizike mwaka 2006 Chama cha Hezbollah kimeanza kushughulikia suala hilo, na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alimtuma ofisa wake mmoja muhimu kufanya usuluhishi. Baada ya kufanya mazungumzo marefu na yenye utatanishi, mwezi Oktoba mwaka jana Chama cha Hezbollah kilibadilishana miili miwili ya wanachama wake kwa mwili mmoja wa Mwisrael aliyekufa maji. Mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu Israel ilimwachia huru mateka mmoja wa Lebanon kwa ajili ya kupata mwili wa askari mmoja wa Israel aliyeuawa katika vita kati ya Lebanon na Israel mwaka 2006. Tarehe 29 Julai baraza la serikali ya Israel iliidhinisha makubaliano ya kubadilishana mateka wa kivita na Chama cha Hezbollah na kukubali kutoa wanachama watano wa Chama cha Hezbollah waliofungwa kwa askari wawili wa Israel waliotekwa, hatua hii imeleta utatuzi kamili wa suala la mateka kati ya Israel na Chama cha Hezbollah.

Wachambuzi wanaona kuwa kama Chama cha Hezbollah na Israel zitaweza kubadilishana matekwa wa kivita kwa wakati uliopangwa, hii italeta athari kubwa kwa pande zote mbili. Kwanza, baada ya vita kati ya Chama cha Hezbollah na Israel kumalizika mwaka 2006, Ushawisi wa Chama cha Hezbollah umekuwa mkubwa nchini Lebanon. Baada ya pande mbili kufikia makubaliano Rais Michel Sulaiman wa Lebanon alitoa pongezi kwa Chama cha Hezbollah. Ofisi ya Habari ya waziri mkuu wa Lebanon tarehe mosi Julai pia ilitoa taarifa ikisema, ushindi kilioupata Chama cha Hezbollah katika mazungumzo pia ni ushindi wa mapambano ya watu wa Lebanon. Baadhi ya wataalamu wanaona kuwa kama mabadilishano hayo yakitekelezwa kikamilifu, sio tu kwamba Chama cha Hezbollah kitakuwa na nguvu kubwa zaidi katika serikali itakayoundwa hivi karibuni na pia kitapata hali nzuri katika uchaguzi wa bunge uliopangwa kufanyika katika majira ya Spring mwaka kesho. Zaidi ya hayo mabadilishano yatasukuma mchakato wa amani kati ya Lebanon na Israel.

Pili, kama mabadilishano hayo ya mateka yakitekelezwa kikamilifu pia yatailetea athari kubwa Israel. Hivi sasa mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel, na kati ya Syria na Lebanon umepata maendeleo na unafuatiliwa sana na jumuyia ya kimataifa. Lakini pamoja na hali hiyo waziri mkuu wa Israel Bw. Ehud Ormert akakumbwa na shinikizo kubwa kutoka kwa wahafidhina nchini Israel. Kwa sababu habari zilizopatikana hivi karibuni zinasema askari wawili waliotekwa na Chama cha Hezbollah wamekwisha kufa, vyombo vya habari vinalalamika kwa kusema kwamba haifai kuwaachia huru askari wa Chama cha Hezbollah kwa miili ya askari hao wawili, kwani kufanya hivyo kutahimiza Chama cha Hezbollah kuzidi kuwakamata askari wa Israel. Zaidi ya hayo baada ya tukio la kigaidi kutokea tarehe 2 huko Jerusalem, Kundi la Galilee Freedom Battalion lenye uhusiano na Chama cha Hezbollah lilitangaza kuwajibika na tukio hilo, na hiki pia ni kivuli kwa mpango wa kubadilishana mateka wa kivita.