Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-08 15:16:36    
Chemsha bongo kuhusu ujuzi wa Mkoa wa Guangxi(6)

cri
Msikilizaji mpendwa:

Radio China Kimataifa imeanzisha mashindano ya chemsha bongo ya mwaka huu kuhusu ujuzi wa vivutio vya utalii mkoani Guangxi, China. Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka iliyopita, kila baada ya kusoma makala moja, tutauliza maswali mawili. Baadaye kamati yetu ya uthbiitishaji itachagua wasikilizaji washindi wa nafasi ya kwanza, pili na tatu pamoja na nafasi maalum. Leo tunakuleta maswali ya makala tano tuliyosoma kwenye chemsha bongo.

1. Alama ya utalii ya mji wa Guilin ni nini?

___________________________________________________________________

2. Urefu wa jumla wa Mto Lijiang ni kilomita ngapi?

___________________________________________________________________

3. Mbali na mkoa wa Guangxi, China, kuna sehemu nyingine duniani ambazo pia zina kima wenye vichwa vyenye manyoya meupe yaliyosimama?

___________________________________________________________________

4. Hivi sasa bado kuna kima wangapi wenye vichwa vyeupe?

___________________________________________________________________

5. Kinanda cha kale cha kabila la wazhuang kinaitwaje?

___________________________________________________________________

6. Maporomoko ya maji ya Detian yako kwenye sehemu ya mpaka kati ya China na nchi gani?

___________________________________________________________________

7. Sikukuu yenye shamrashamra kubwa zaidi ya kabila la wajing ni sikukuu gani?

___________________________________________________________________

8. Mji unaosifiwa kuwa ni mji wenye hewa nyingi zaidi ya oxygen kuliko miji mingine nchini China ni mji gani?

___________________________________________________________________

9. Mji mdogo wa kale wa Huangyao umekuwa na historia ya miaka mingapi?

___________________________________________________________________

10. Kwenye eneo la Mlima Gupo kuna vilele vingapi vya mlima?

___________________________________________________________________

Karibuni ushiriki kwenye chemsha bongo hii, makala tano tuliyosoma tumeweka kwenye kipindi cha Sanduku la Barua katika tovuti yetu ya mtandao wa internet, unaweza kuzisoma. Tafadhali utuletee majibu kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Idhaa ya Kiswahili ya CRI