Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-10 18:49:53    
Mkutano wa wakuu wa nchi nane wafungwa

cri

 Mkutano wa wakuu wa nchi nane, ambao ulifanyika kwa siku 3 kwenye ziwa la Toyoko, Hokkaido nchini Japan, ulifungwa tarehe 9 alasiri, waziri mkuu wa Japan Bw. Yasuo Fukuda alitangaza kuwa mkutano umefanikiwa. Lakini vyombo vya habari vinaona kuwa, mkutano huo haukupata maendeleo halisi, kufungwa hivi hivi kwa kawaida kunaonesha mgongano kati ya maslahi ya nchi hizo nane. Kwa upande mwingine, athari za kundi la nchi nane la viwanda kwa dunia inatiliwa mashaka kwa mara nyingine tena, ambapo athari ya nchi zinazoendelea inainuka kila siku ipitayo.

Suala la mazingira ilikuwa ni ajenda muhimu kwenye mkutano huo, nchi mwenyeji Japan pia inataka kuonesha athari yake kwa dunia kutokana na maendeleo yanayopatikana kuhusu kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani kwenye mkutano wa wakuu wa nchi nane. Waziri mkuu wa Japan, Bw. Yasuo Fukuda anaona, kufikia makubaliano hayo kuhusu lengo la muda mrefu la mwaka 2050 kupunguza utoaji wa hewa inayosababishwa kuongezeka kwa joto duniani, ni maendeleo halisi yaliyopatikana kwenye mkutano huo. Lakini nchi nane ikiwemo Marekani zinakubali lengo la muda mrefu la kupunguza kwa nusu utoaji wa hewa inayoongeza joto la dunia mwaka 2050, lakini hazikueleza bayana kuhusu idadi ya msingi wa lengo hilo, ila tu kupunguza kwa 50% ya "hali ya hivi sasa". Kuhusu lengo la muda mrefu wa kiasi la kupunguza utoaji wa hewa ya kuongeza joto, viongozi wa nchi mbalimbali walisema tu, watachukua hatua kwa kufuata hali halisi ya nchi zake, wala hawakugusia matakwa ya kuweka hesabu kamili. Hali hiyo imepunguza kabisa mafanikio ya mkutano huo kuhusu kupunguza utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto.

Nchi hizo nane pia hazikutoa mapendekezo halisi kuhusu suala la kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na nafaka. Zilisisitiza kuwa katika muda mfupi ujao nchi zinazotoa mafuta zinatakiwa kuongeza utoaji wa mafuta na kuinua uwezo wa kusafisha mafuta; Nchi zinazoagiza mafuta zinatakiwa kuongeza ufanisi wa matumizi ya nishati. Kuhusu suala la nafaka, viongozi wa nchi mbalimbali walisema watatunga sera kadiri iwezekanavyo ili kukabiliana na misukosuko mbalimbali inayosababishwa na kupanda kwa kiwango cha juu kwa bei ya nafaka. Lakini vyombo vya habari vimeona kuwa, nchi nane hazikutoa maoni kamili kuhusu masuala hayo yanayohusiana na maisha ya watu wa nchi zinazoendelea.

Kuhusu suala la maendeleo ya bara la Afrika, nchi nane zimesema zitaendelea kujitahidi kutekeleza lengo la maendeleo la milenia lililotolewa na Umoja wa Mataifa, zinaendelea kuunga mkono maendeleo ya Afrika, lakini hazikutoa mbinu mpya kamili.

Kuhusu suala la usalama wa dunia, wakuu wa nchi nane walijadili suala la nyuklia la peninsula ya Korea na suala la nyuklia la Iran, walipongeza hatua za maendeleo ya suala la nyuklia la peninsula ya Korea, walieleza kuunga mkono mkutano wa pande 6 wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea na kuihimiza Iran itekeleze maazimio husika ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Lakini nchi nane hazikujadili kuhusu mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel pamoja na hali ya Iraq na Afghanistan.

Wachambuzi wanaona kuwa, tofauti ya masuala yanayofuatiliwa na mgongano wa maslahi za nchi mbalimbali kwenye mkutano huo ni chanzo cha kufungwa hivi hivi tu kwa mkutano huo. Marekani ilikwepa suala la mazingira, lakini ilifuatilia suala la nyuklia la peninsula ya Korea, Japan ilifuatilia suala la kuwa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama na suala la mateka, Russia ilifuatilia usalama wa kimkakati na mgogoro wa ardhi kati yake na Japan ?? lakini kuna migongano mikali ya kimaslahi kati ya nchi mbalimbali katika masuala ya kimataifa ya kupunguza utoaji wa hewa inayosababisha kuongezeka kwa joto, kupanda kwa bei za mafuta na nafaka, pamoja na maendeleo ya Afrika.

Wakati nchi kubwa kiuchumi haziwezi kuleta maendeleo mkubwa, nchi zinazoendelea zilizoalikwa kushiriki kwenye mkutano huo, hususan shughuli zilizofanywa na China nchini Japan zilifuatiliwa sana na nchi mbalimbali. Vyombo vya habari vimesema, masuala yote yawe kuhusu mazingira, nafaka au nishati, yote yanahusiana na China.