Tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya India tarehe 10 ilitangaza mswada wa makubaliano ya uhakikisho yaliyofikiwa kati ya India na Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa kuhusu kuhimiza utekelezaji wa makubaliano kati ya India na Marekani kuhusu mambo ya nyuklia. Wakati huo huo serikali ya India ilisema, India imewasilisha nyaraka za mswada huo kwenye Baraza la Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa, na itasaini rasmi makubaliano ya uhakikisho na Shirika hilo mapema zaidi.
Kutangazwa kwa mswada huo wa makubaliano kumeleta mara moja mkoroganyo kwenye jukwaa la kisiasa la India. Kwani tarehe 8 mwezi huu, serikali ya India ilishikilia msimamo wa kutodokeza yaliyomo ya mswada huo kwa vyama vya mrengo wa kushoto, ikavifanya vyama hivyo vilivyoiunga mkono serikali ya India kwa miaka minne viache kuiunga mkono serikali, na kuvujika kwa muungano wa utawala, ambapo waziri wa mambo ya nje wa India Pranab Mukherjee alitafsiri kuwa, yaliyomo ya mswada wa makubaliano ni ya waraka wa kisiri uliofikiwa kati ya serikali ya India na Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa, ambao hauruhusiwi kutangazwa hadharani kabla ya kusainiwa rasmi. Baada ya vyama vya mrengo wa kushoto kuacha uungaji mkono wake kwa serikali, Bw. Mukherjee alisema pia, baada kupata kura ya imani kutoka kwa bunge, serikali ya India itatafuta tena kusaini makubaliano ya uhakikisho kati yake na Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa. Lakini siku moja tu baada ya kuyasema hayo, serikali ya India ikaanza kuwasilisha mswada huo wa makubaliano kwa Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa, na kutangaza yaliyomo ya mswada huo.
Ndiyo maana serikali ya India imelaumiwa vikali na chama cha upinzani cha umma cha India na vyama vya mrengo wa kushoto vilivyokuwa washirika wake katika siku zilizopita. Kiongozi wa chama cha umma cha India Bw. L.K.?dvani aliilaani serikali kwa kusema uwongo kwa wananchi kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya India na Marekani, alisema serikali hiyo haiaminiki na baada vyama vya mrengo wa kushoto kuacha uungaji mkono wake kwa serikali, serikali hiyo ya sasa haina uhalali wa kuwawakilisha watu wengi zaidi, tena haina haki ya kuendelea kuhimiza mchakato wa utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia kati ya India na Marekani, hivyo ni lazima kupiga kura ya imani kwa serikali kwenye bunge.
Na vyama vya mrengo wa kushoto pia vinailaani serikali ya India kwa kusema maneno yasiyolingana na vitendo vyake. Kwa upande mmoja imewadanganya wananchi kuwa itahimiza mchakato wa utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia kati ya India na Marekani baada ya kupitisha upigaji kura ya imani, kwa upande mwingine iliwasilisha faraghani nyaraka ya makubaliano kwa Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa, ikijaribu kuifanya hali yenyewe iwe "ukweli wa mambo". Aidha hatua hiyo ya serikali ya India ilichukuliwa baada ya waziri mkuu wa India Bw Manmohan Singh kukutana na rais wa Marekani wakati alipohudhuria mkutano wa kundi la nchi nane nchini Japan, tena tovuti ya Marekani kwenye mtandao wa internet ilitangulia kutangaza yaliyomo ya mswada wa mapato, hivyo vyama vya mrengo wa kushoto vimeona kuwa, serikali ya India imesujudu mbele ya shinikizo ya Marekani kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya India na Marekani.
Msemaji wa Chama tawala cha National Congress cha India alisema, serikali ya India kukabidhi nyaraka za mswada kwa Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa, ni kufuata utaratibu tu, haumaanishi kuwa pande hizo mbili zimesaini rasmi makubaliano. Alisema serikali ya India itafuata ahadi yake ya kusaini rasmi makubaliano hayo na Shirika la nishati atomiki la Kimataifa baada ya kupiga kura ya imani.
Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, hatua hiyo ya India haimaanishi kuwa makubaliano ya nyuklia kati ya India na Marekani yaliyokwama kwa muda mrefu yatafufuliwa mara moja. Hata kama Shirika la nishati ya atomiki la Kimataifa litayaunga mkono makubaliano hayo, India bado inatakiwa kupata ruhusa ya biashara ya nyuklia kutoka kwa kundi la nchi 45 zinazotumia nishati ya nyuklia, pamoja na idhini ya bunge la taifa la Marekani. Hivyo mustakabali wa makubaliano hayo kati ya India na Marekani bado hauonekani wazi ni wa namna gani.
|