Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-16 20:34:34    
Sudan yakataa mashitaka ya mahakama ya kimataifa

cri

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kesi za jinai ya kimataifa iliyowekwa The Hague, nchini Uholanzi, Bw. Luis Moreno Ocampo Tarehe 14 alimfungulia mashitaka rais Omar al-Bashir wa Sudan kwa hatia ya kuanzisha vita kwenye sehemu ya Darfur nchini Sudan, na kuiomba mahakama kutoa amri ya kumkamata. Serikali ya Sudan imekataa mashitaka hayo, ikisema kitendo hicho kitaharibu mchakato wa amani nchini Sudan, hata kinaweza kusababisha tena umwagaji damu kwenye sehemu ya Darfur. Mchambuzi mmoja amesema kukataa kwa serikali ya Sudan kunatokana na sababu mbili.

Kwanza, serikali ya Sudan haitambui mashitaka ya mahakama ya kesi za jinai ya kimatiafa kuhusu Bw. Bashir, ikisema suala la Darfur ni mambo ya ndani ya Sudan, mashitaka ya mahakama ya kimatiafa yana "malengo ya kisiasa", na yanaingilia kati mambo ya ndani ya nchi hiyo. Serikali hiyo pia imesema, kitendo hicho cha mahakama ya kimataifa kitabadilisha zaidi suala la Darfur kuwa suala la kimataifa, hivyo serikali ya Sudan inapinga kutoka zamani.

Pili, serikali ya Sudan inaona kuwa, Sudan haikusaini "Mkataba wa Rome" kuhusu kuanzishwa kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai, inasisitiza kuwa mahakama hiyo haina nguvu ya kisheria kuhusu rais wa Sudan, hivyo serikali ya Sudan haitatekeleza uamuzi wowote wa mahakama hiyo.

Jumuiya ya kimataifa imetoa maoni yake baada ya mahakama ya kimatiafa kutoa mashitaka dhidi ya Bw. Bashir. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-moon alitoa taarifa ikisema, ana "wasiwasi mkubwa" kuhusu mashitaka yaliyotolewa na mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa, kwani yanaweza kusababisha matokeo mabaya kwenye kazi za kulinda amani. Viongozi wa baadhi ya nchi za kiarabu na Afrika pia wameonya kuhusu matokeo yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho cha mahakama ya kimataifa. Umoja wa Nchi za Kiarabu umesema, utaanzisha mazungumzo kuhusu mgogoro wa Sudan. Jumuiya ya kiislamu imeonya kuwa huenda mashitaka hayo yatasababisha "matokeo mabaya sana". Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China, Bw. Liu Jianchao alisema, China inafuatilia suala hilo na kuona wasiwasi, inatarajia kuwa pande mbalimbali zitakuwa na uangalifu na kumaliza migongano kwa njia ya mazungumzo. Rais George Bush wa Marekani alitoa hotuba tarehe 15, ikisisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika utatuzi wa mapambano ya sehemu ya Darfur, na kutaka Umoja wa Mataifa na serikali ya Sudan ziimarishe ushirikiano kuhusu suala la Darfur na kutuma jeshi la kulinda amani kwa sehemu hiyo.

Hivi sasa, jeshi la mseto la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika linaendelea kutekeleza jukumu la kulinda amani kwenye sehemu ya Darfur na kufanya kazi ya kutuliza hali ya Darfur, lakini limekumbwa na tatizo la upungufu wa idadi ya askari, fedha na vitu vya mahitaji, zaidi ya hayo usalama wa jeshi la kulinda amani unakabiliwa na changamoto.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon alitoa taarifa baada ya Bw. Bashir kufunguliwa mashitaka, akitarajia rais Bashir awe na busara zaidi kuhsu mashitaka hayo, alisisitiza kuwa msimamo wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Darfur ya Sudan haujabadilika, kitu muhimu kwa hivi sasa ni serikali ya Sudan ijitahidi kuhakikisha usalama wa askari wanaolinda amani na watu wanaoshughulikia utoaji wa misaada ya kibinadamu kwenye sehemu ya Darfur.

Mchambuzi mwingine anasema, kitendo hicho ya mahakama ya uhalifu wa jinai ya kimataifa hakisaidii utatuzi wa mgogoro wa Darfur, kinyume chake, kinaweza kutatanisha zaidi hali ya Darfur. Hivi sasa kuendelea pole pole kwa mchakato wa siasa ya Darfur, kimsingi kunatokana na sababu mbili muhimu. Kwanza ni makundi yanayoipinga serikali ya huko hayataki kurudi kwenye meza ya mazungumzo; Pili, ni baadhi ya nchi za nje zenye nguvu ya kuathiri makundi hayo, zinataka kujinufaisha kwa kutumia mgogoro huo.