Maofisa na askari 172 kwa jumla waliobaki wa kikosi cha kwanza cha askari wahandisi cha China kinachotakiwa kwenda Darfur nchini Sudan kutekeleza jukumu la kulinda amani, tarehe 16 usiku walifunga safari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zhengzhou, mkoani Henan.
Wakati wa usiku wa majira ya joto, hali ya furaha na shamrashamra zilijaa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zhengzhou, na sauti ya muziki wa bendi ya jeshi ilikuwa ikisikika kwenye uwanja wa ndege. Maofisa na askari 172 waliovaa sare za kijeshi waliingia kwa ukakamavu kuelekea kwenye ndege, na kwenda kutekeleza jukumu la kulinda amani. Kuondoka kwao kunaonesha kuwa kikosi ha askari wahandisi cha China kinachokwenda kwenye sehemu ya Darfur, Sudan kimekamilika, ambapo serikali ya China imetimiza ahadi iliyotoa kwa dunia.
Kabla ya kuondoka, naibu kiongozi wa kundi hilo la askari wahandisi, Bw. Xu Hanfa aliwaambia waandishi habari wa China na wa nchi za nje, kutokana na habari kuhusu hali ya kisiasa na mazingira ya kimaumbile zilizoletwa na kikundi cha utangulizi, ambacho kilikwenda Darfur tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2007, askari waliobaki walirekebisha mpango wa mafunzo, na kufanya maandalizi ya pande mbalimbali ili kutekeleza vizuri zaidi jukumu la kulinda amani na kuongeza sifa kwa jeshi la China. Alisema,
"Kwanza, kutokana na kuzingatia hali ya usalama ya sehemu ya Darfur, waliimarisha mafunzo ya ulinzi pamoja na uwezo wa kukabiliana na matukio ya dharura. Pili, kuimarisha mafunzo ya ustadi wa kazi maalumu za kutekeleza majukumu ili kuwahakikishia maofisa na askari wawe na uwezo kamili wa kumaliza kazi zao maalumu. Tatu, kuimarisha mafunzo ya kuwawezesha maofisa na askari hao kutekeleza majukumu katika mazingira ya huko na kuweka msingi kwa askari hao kutekeleza jukumu la kulinda amani kwa ufanisi na kwa kiwango cha juu."
Darfur ni moja ya sehemu zilizokuwa nyuma kiuchumi nchini Sudan, kwa kufuata hali maalumu ya joto na ukame kwenye sehemu hiyo na hali halisi ya ugumu wa kazi za uhandisi, maofisa na askari waliobaki wa kikundi cha askari wahandisi cha China walipewa mafunzo ya kuvumilia joto, kiu, uchovu na kuzuia kuumizwa na jua kali. Vilevile, maofisa na askari hao waliongezewa mafunzo kuhusu ufahamu wa kimsingi wa kuimarisha uwezo wa kulinda amani, wamefahamu sera na sheria mbalimbali husika zikiwemo "Katiba ya Umoja wa Mataifa" na "Sheria ya Kimataifa, na kuinua kiwango cha kufahamu lugha za kigeni, ili kuwa na uwezo zaidi katika kuwasiliana na watu wa huko.
Baada ya kufanya mafunzo na maandalizi kwa muda mrefu, maofisa na askari hao waliobaki wamekuwa na uwezo mkubwa zaidi iwe kwa sifa za kisaikolojia au kwa ufundi wa kijeshi. Naibu kiongozi Bw. Xu Hanfa alisema akiwa na imani, mazingira magumu ya kimaumbile na hali ya usalama yenye matatizo mengi, hayawezi kuwatisha wanajeshi wa China. Alisema
"Tukiwa jeshi la kulinda amani linalotumwa na Umoja wa Mataifa, tutafuata kwa makini maagizo ya Umoja wa Mataifa, kutekeleza kwa ufanisi jukumu la kulinda amani, kutimiza majukumu yote tunayokabidhiwa na Umoja wa Mataifa, kuonesha sura nzuri ya jeshi lenye nguvu, jeshi lenye sifa nzuri na jeshi la amani ili kutoa mchango kwa amani, utulivu na maendeleo ya sehemu ya Darfur ya Sudan."
Sasa, mashujaa hao wataondoka hivi karibuni kwenye maskani yao na kuagana na jamaa zao, watakwenda kukabiliana na changamoto mpya kabisa na kutekeleza majukumu magumu. Kwenye mpango wa kuingia kwenye ndege, maofisa na askari hao walipunga mikono na kuagana na watu walioko huko, na wote walikuwa na tabasamu ya kujiamini. Askari wawili walizungusha bendera nyekundu yenye nyota tano na bendera ya Umoja wa Mataifa hadi askari wa mwisho alipoingia kwenye ndege saa 3, na nusu usiku ndege maalumu iliyowabeba maofisa na askari wa kulinda amani wa China iliruka.
|