Mgombea urais wa Marekani kutoka chama cha Demokrasia Bw. Barack Obama tarehe 20 alifanya mazungumzo na rais Hamid Karzai wa Afghanistan huko Kabul, mji mkuu wa nchi hiyo, viongozi hao walijadiliana kuhusu hali nchini humo na ya kanda hiyo, na masuala mengi kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na biashara ya dawa za kulevya, ukarabati wa Afghanistan na ushirikiano wa usalama na wa kiuchumi kati ya Marekani na Afghanistan. Bw. Obama siku hiyo pia aliwatembelea wanadiplomasia wa Marekani nchini humo, kamanda wa jeshi na askari wa Marekani, Bw. Obama pia alifahamishwa kuhusu hali ya Afghanistan na jeshi la Marekani nchini humo.
Kwa mujibu wa ofisa wa Afghanistan, kwenye mkutano huo Bw. Obama alisema, vyama vya Demokrasia na Rupublican vya Marekani vyote vinaunga mkono jeshi la Marekani kuendelea kuwepo nchini humo na kutoa uungaji mkono wa muda mrefu kwa nchi hiyo. Bw. Obama alisema, kama atachaguliwa kuwa rais, Marekani itaendelea kuiunga mkono serikali ya Afghanistan na kuendelea na mapambano dhidi ya ugaidi.
Bw. Obama alitoa taarifa baada ya kuondoka nchini Afghanistan akisema, yeye na wabunge wawili wa baraza la juu la bunge la Marekani walioambatana naye wote wanazitaka Marekani na Jumuiya ya NATO zitoe misaada zaidi kwa nchi hiyo, serikali ya Afghanistan inapaswa kuchukua hatua nyingi zaidi ili kuinua kiwango cha maisha ya watu wa nchi hiyo. Aidha, Bw. Obama alipohojiwa alisema, serikali ya Marekani inapaswa kuendelea kutoa misaada kwa serikali ya Pakistan ili kupambana na magaidi walioko kwenye sehemu ya mpaka wa Pakistan.
Mbali na kutembelea Afghanistan, Bw. Obama pia atafanya ziara katika nchi za Iraq, Jordan, Israel, Ujerumani, Ufaransa na Uingereza. Hii ni ziara ya kwanza kwa Bw. Obama tangu achaguliwe na chama chake kuwa mgombea urais wa Marekani mwezi uliopita, lengo la ziara hiyo ni kueleza kikamilifu mitizamo yake ya kidiplomasia, na kuonesha kuwa ana uwezo wa kuongoza jeshi la Marekani baada ya kuchaguliwa kuwa rais, ili kujibu shutuma za chama cha Republican kuhusu yeye kutokuwa na uzoefu kwenye mambo ya kidiplomasia. Kuichagua Afghanistan kuwa kituo cha kwanza cha ziara yake ya kimataifa, kidhahiri kunahusiana na msimamo wake thabiti kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi.
Kwanza, Bw. Obama anaona kuwa Afghanistan inapaswa kuchukuliwa kuwa ni sehemu ya kiini kwenye mapamabno dhidi ya ugaidi, pia amesisitiza kuwa nguvu za kundi la Taliban na Al-Qaeda zinarudi, kwa hiyo Marekani inapaswa kutuma askari wengi zaidi nchini humo na kuhamaisha ufutiliaji wa Marekani Afghanistan kutoka Iraq. Kabla ya serikali ya Bush kuanzisha vita vya Iraq, Bw. Obama alisema vita vya Iraq vitahamisha ufuatiliaji wa watu kwa magaidi waliopanga na kuzusha shambulizi la Septemba 11. hali hiyo inasumbua vita vya Marekani dhidi ya ugaidi.
Kwa hiyo suala la Afghanistan huenda litakuwa moja ya mambo atakayoyapa kipaumbele naye katika sera za kidiplomasia baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Pili, sababu nyingine kwa Bw. Obama kutilia maanani suala la Afghanistan ni kufuatana na hisia za wapiga kura wa Marekani. Wakati vita vya Iraq vilivyoanzishwa na rais Bush vinapingwa na watu wengi zaidi, bado kuna zaidi ya nusu ya wamarekani wanaounga mkono shughuli za jeshi la Marekani nchini Afghanistan, na kuona kuwa juhudi na gharama ilizotoa Marekani zinastahili, Marekani inapaswa kuyashinda makundi ya Taliban na Al-Qaeda yaliyoko nchini Afghanistan ili kushinda vita hivyo dhidi ya ugaidi.
Vyombo vya habari vinaona kuwa, ingawa Bw. Obama hakufafanua kikamilifu sera zake kwa Afghanistan katika ziara yake nchini humo, lakini sera za Marekani kwa nchi hiyo zitarekebishwa baada ya kipindi cha Rais Bush kwisha. Hivi sasa ingawa Bw. Obama na Bw. McCain wana misimamo tofauti kuhusu suala la vita vya Iraq, lakini wana msimamo unaofanana katika suala la Afghanistan, wote wawili wanapedekeza kuhamisha kiasi cha nguvu ya jeshi la Marekani kutoka Iraq hadi Afghanistan, na wote wanapendekeza Marekani na Afghanistan zidumishe uhusiano wa wenzi na kuongeza zaidi misaada kwa nchi hiyo.
|