Mkutano wa 15 wa baraza la sehemu ya Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki tarehe 24 ulitoa "Taarifa ya Mwenyekiti" huko Singapore ikisisitiza kuimarisha mazungumzo na ushirikiano, kulinda amani na usalama wa sehemu hiyo.
Kwenye "Taarifa ya Mwenyekiti", mawaziri wa mambo ya nje wa nchi mbalimbali walisisitiza umuhimu wa baraza la sehemu ya Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki, ambalo ni baraza muhimu la pande nyingi kuhusu mambo ya siasa na usalama katika sehemu hiyo, wanaunga mkono umuhimu wa uongozi wa Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki katika baraza hilo, na kuhimiza nchi wanachama wa baraza hilo ziendelee kushirikiana na kutoa mchango zaidi kwa maendeleo ya baraza hilo. Washiriki wa mkutano walisema, wanaridhika na maendeleo ya baraza hilo pamoja na kazi zilizofanywa na baraza hilo katika mwaka uliopita kuhusu kuimarisha mazungumzo na ushirikiano katika mambo ya siasa na usalama pamoja na kujenga uaminifu kati ya nchi wanachama. Kutokana na ongezeko la idadi ya changamoto za aina mbalimbali pamoja na maeneo ya shughuli, kwa hiyo washiriki wanaona kuwa baraza hilo linatakiwa kufanya ushirikiano mkubwa na halisi zaidi.
Mawaziri na wajumbe wa nchi mbalimbali walijadili suala la kupunguza athari za maafa. Walifuatilia idadi kubwa ya vifo vya watu, majeruhi pamoja na hasara za mali zilizosababishwa na kimbunga kilichotokea nchini Myanmar na matetemeko ya ardhi yaliyotokea katika wilaya ya Wenchuan, China, wakiona kuwa misaada ya kibinadamu iliyotolewa na jeshi linalotekeleza jukumu ya utoaji misaada ya kibinadamu kwa watu waliokumbwa na maafa nchini Myanmar ni yenye ufanisi. Kwa kuwa nchi nyingi wanachama wa umoja huo zinakabiliwa na tishio la maafa ya kimaumbile, kwa hiyo washiriki wa mkutano wamesisitiza kuwa, baraza hilo linapaswa kuimarisha ushirikiano na mashirika ya kimataifa na ya Umoja wa Mataifa kuhusu kufanya maandalizi ya kukabiliana na matukio ya dharura, kupunguza athari za maafa na ujenzi mpya baada ya maafa, licha ya hayo nchi wanachama zinatakiwa kuanzisha miradi ya ushirikiano kati yao kuhusu mazoezi ya pamoja na utoaji wa teknolojia na misaada. Washiriki wa mkutano walitoa mapendekezo manne kuhusu kuimarisha ushirikiano kwenye eneo la usalama: Kwanza, zianzishe mazoezi ya pamoja na kunufaika kwa pamoja kutokana na habari zilizopatikana, vilevile ziimarishe ushirikiano kati ya makundi ya kiraia ya utoaji wa misaada na majeshi ili kukabiliana na maafa makubwa yanayozihusu nchi nyingi. Pili, idara za utoaji misaada za nchi wanachama ziimarishe maelewano na ushirikiano. Tatu, pande zinazohusika na utoaji misaada wakati wa kutokea kwa maafa za baraza la sehemu ya Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki, zinatakiwa kufanya ushirikiano na nchi wanachama za baraza hilo, kubuni mpango wa kazi za kupunguza athari za maafa, na kujadili namna ya kuweza kutumia vizuri nguvu za makundi ya kiraia ya utoaji misaada na nguvu za majeshi wakati yanapotokea maafa. Nne, washiriki walikubali mapendekezo yaliyotolewa na Philippines na Marekani kuhusu kufanya "mazoezi ya pamoja ya kupunguza athari za maafa ya baraza la sehemu ya Umoja wa Nchi za Asia ya Kusini Mashariki.
Washiriki wa mkutano pia walijadili suala la nyuklia la peninsula ya Korea na suala la bahari ya China ya sehemu ya kusini. Kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea, washiriki walisisitiza kuunga mkono utekelezaji wa taarifa ya pamoja ya tarehe 19 Septemba. Kuhusu suala la bahari ya China ya sehemu ya kusini, washiriki wa mkutano walisisitiza kuwa, "azimio la vitendo vya pande mbalimbali kwenye bahari ya Kusini", lililotiwa sahihi mwaka 2002 na nchi za Umoja wa Asia ya Kusini Mashariki pamoja na China, linaonesha ahadi zilizotolewa na pande mbalimbali kuhusu kutatua migogoro ya sehemu hiyo kwa njia ya amani, zinaona kuwa azimio hilo limejenga imani na uaminifu kati ya pande mbalimbali, na linasaidia kulinda amani na utulivu wa sehemu hiyo.
Kuhusu kupambana na ugaidi, washiriki wanaunga mkono utekelezaji wa "mpango wa kupambana na ugaidi na kutoa adhabu kwa vitendo vya uharifu wa kuvuka mipaka.
|