Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-07-28 19:53:07    
Jumuiya ya kimataifa yapokea kwa pamoja michezo ya Olimpiki ya Beijing

cri

kadiri inavyokaribia ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Beijing, shughuli nyingi zenye kauli-mbiu ya michezo ya Olimpiki zinafanyika katika sehemu mbalimbali za dunia, watu wanatumia nafasi hiyo kuonesha matarajio na kuitakia kila la heri michezo ya Olimpiki ya Beijing.

"Dunia moja, ambayo ni maonesho ya sanaa ya ukoo mkubwa wa kimataifa wa wasanii wachoraji wa China" yanayoitikia kauli-mbiu ya michezo ya Olimpiki ya Beijing, yalifunguliwa tarehe 21 kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Maonesho hayo ya michoro yameonesha karibu michoro murua 200 ya wachoraji mashuhuri 200 wa sasa wa China kuhusu jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa wenye nchi wanachama 192, mabaki muhimu ya utamaduni, mila na desturi za watu, maua na ndege vilivyothibitishwa kuwa alama ya taifa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aliyeshiriki kwenye ufunguzi wa maonesho hayo ya sanaa, Bw. Ban Ki-moon alieleza kuitakia kila la heri michezo ya Olimpiki inayoandaliwa na China. Alisema

"Nimepata kumbukumbu nyingi kuhusu maandalizi yaliyofanywa na China kuhusu michezo ya Olimpiki, viwanja na majumba ya michezo ni majengo mazuri, ambayo hayajaonekana katika historia. Iliyonishangaza zaidi ni kuwa watu wa china waliokumbwa na maafa ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mkoani Sichuan, bado wanaweza kumaliza vizuri hivyo maandalizi yote ya michezo ya Olimpiki, ninatoa pongezi kwa jitihada zao. Ninaamini kabisa kuwa michezo ya Olimpiki ya Beijing itakayofunguliwa baada ya wiki mbili, itakuwa michezo ya Olimpiki ya kufana zaidi katika historia, sio kama itatoa nafasi ya kushindana kwa haki kwa wachezaji wa nchi mbalimbali, bali pia itatoa nafasi ya kuhimiza ustawi na utulivu, na kuimarisha maingiliano na maelewano kwa watu wa duniani."

Maofisa wa kamati ya Olimpiki ya China, kamati ya Olimpiki nchi ya umoja wa falme za kiarabu pamoja na ofisi ya konsela mkuu wa China aliyeko huko Dubai, walishiriki kwenye ufunguzi wa sherehe za kupokea michezo ya Olimpiki ya Beijing kwenye sehemu ya "mji wa dragon", mjini Dubai. Shughuli hizo zitafanyika kuanzia tarehe 17 hadi tarehe 28 mwezi Agosti, ambapo wachezaji kutoka China wataonesha michezo ya jimnastiki, mpira wa meza, taekwondo na judo. Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki ya nchi ya umoja wa falme za kiarabu, Bw. Ibrahim Abdulmalek alisema,

"Wakati michezo ya Olimpiki ya Beijing inakaribia kufunguliwa, tunafanya shughuli za kupokea michezo ya Olimpiki katika nchi ya umoja wa falme za kiarabu, lengo letu ni kuonesha uungaji mkono wa watu wa nchi hiyo kwa michezo ya Olimpiki inayoandaliwa na watu wa China. Tunaona michezo ya Olimpiki ya China itavumbua historia, tunaitakia mafanikio michezo ya Olimpiki ya Beijing."

Tarehe 23, Ofisi ya ubalozi wa China nchini Japan ulifanya maonesho ya picha ya "Beijing inakukaribisha", maonesho hayo yameonesha picha 94 kuhusu jadi na mambo ya kisasa ya Beijing, michezo ya kujenga mwili ya umma pamoja na viwanja na majumba ya michezo ya Olimpiki. Spika wa bunge la taifa aliyetembelea maonesho, Bw. Eda Satsuki alisema, michezo ya Olimpiki ya Beijing ni michezo mikubwa inayotarajiwa sana na watu, mafanikio ya michezo ya Olimpiki yanaifanya Beijing hata China nzima ipate maendeleo ya kasi zaidi.

Wachina wanaoishi nchini Argentina na Waargentina wenye asili ya China wamenuia kufanya gulio kubwa kwenye mtaa wa China wa mji mkuu Buenos Aires. Tena wakishirikiana na wakazi wa huko wataweka skrini kubwa ya televisheni kwenye mtaa wa China ili kuangalia sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki.