Tumezoea kuona mchezo wa soka au kandanda au wengine huliita gozi la ngombe. Wengine pia huliita kabumbu. Lakini kwa maana hiyo hiyo mpira wa miguu, wakicheza zaidi wanaume.
Hayo mambo sasa ni tofauti kabisa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
Ama mazoea kweli yanatabu lakini nayo pia huweza kubadilika siku moja na kuwa kitu cha kawaida wala hakishangazi tena miongoni mwa jamii husika.
Kama utajiuliza wanawake nao wameanza lini na hili soka jawabu mbona kitambo sasa.
Hebu tuangalie mataifa ambayo yapo juu katika fani hii ya soka la wanawake bila kusahau kuwa sheria ndio hizo hizo.
Unafahamu kuwa mfalme wa soka ulimwenguni. Pele ametokea nchini ya Brazil basi kama walioyotamba akina dunga, Romario, Rai, Jazinho Rivado, Rorbato Carlos, Cafu na sasa wapo Robihho, Riaucho, kaka na wengine wengi tu basi akinadada wa Brazil wakiingia uwanjani utapenda kuangalia jinsi wanavyokaba wanaovyotoa pasi na kufunga magoli mazuri pia.
Ujerumani
Kama unawakumbuka vizuri akina Rudde Voller, Clisman, Berkenbar, na wengine basi kinadada wa Ujerumani wamechukua mikoba hasa katika ufungaji wa magoli ya vichwa huamini waoyosakata soka kwa magoli hayo ya utosi.
Norway
Ni nchi za mwanzo mwanzo kuanza kucheza gozi la kike wakifuatiwa na hata Sweden, hawa mbali ya kucheza kwao pia walioneza sehemu mbali mbali hasa kwa nchi za Afrika.
China
Ni moja inayochukua nafasi ya ubora wa mchezo huo hapa China kwani hata ukizungumza na wachina wenyewe basi wanakiri timu ya wanawake katika soka ni bora zaidi hata ya wanaume. Sijui kama kweli.
Argentina
Argentina nao wanafuata zile nyayo za akina Maradona, Folan na sasa Tavez kwa maana hiyo nao wapo makini kiwanjani kusakata hilo gozi la ngombe.
Japan na Canada, USA, South Korea japo hazina wachezaji maarufu sana lakini nao wamo.
Nigeria
Hivi ni vijogoo vya Afrika katika soka hili la wanawake kwani nao pia wanafuata nyayo za kaka zao wapo wa kali akina kana okocha, Finidi Amonike, Amokachi.
Mimi nafurahi katika michezo ya Olympics ya Beijing 2008 kuna karibu timu 12 za wanawake wanashiriki katika michuano hiyo: China, Brazil, USA, Canada, Japan, South Korea, Sweden, Nigeria, New Zealand, Norway, Argentina na Ujerumani na zitakia kila la kheri timu zote hizo.
|