Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-08-12 16:28:02    
Ushindani uliojaa ni dhamu na ufundi

cri

Michezo ya 29 ya Olympics imo kuendelea vizuri michezo hiyo ambayo inazijumiisha nchi mbalimbali ulimwenguni.

Ushiriki wa michezo hii ambao haukujali taifa dogo wala kubwa kila nchi ina haki sawa ya kushiriki, pengine kikubwa ni uwezo wa nchi basi jinsi ilivyotuma washirika wake pia kuzingatia vigezo vya viwongo vinavyo kubalika katika michezo mbalimbali ambayo mchezaji anashiriki siyo kujaza kapu tu.

Nilikwisha sema mwanzoni jinsi ya ushindani wa michezo hii itakuwa ya ngumu zaidi. Pia nilieza jinsi ya nidhamu michezoni hayo tayari niliweka bayana.

Sasa kwa mtazamo wangu kadri siku zinazoyosonga mbele kwenye michezo hii ya Olumpics hapa Beijng kuna mambo mengi ambayo mimi najaribu kuangalia kwa mtazamo wa kiufundi, kiushindani na usoefu pia lakini kubwa ambalo nazingatia ni lile lile suala la nidhamu katika mchezo ambacho ndicho kigezo kizuri cha ushindani.

Labda nikumbushe kidogo tu nidhamu inaanza wapi nidhamu inaanzia kwa viongozi kidogo tu nidhamu inaanza wapi nidhamu inaanzia kwa viongozi, mwanachama mtazamaji kwa maana ya mshangiliaji hata mchezaji mwenyewe. Kauli yangu ni ushindani uliojaa nidhamu na ufundi na mazoezi. Nimeamua kusema hivi baada ya kufuatilia michezo mbalimbali ambayo unaendelea kufanyika katika viwanja na kumbi mbalimbali. Hadi sasa nina mifano mingi tu ya kueleza jinsi ya muono wangu katika ushindani wa michezo hii yenye kuvuta hisia ya wengi na pia kutatuliwa na watu wengi pia.

Awali ya yote tutizame mchezo wa soka.

Soka ni moja ya mchezo maarufu duniani ambao nao umo katika ushindani kwenye Olympics hapa Beijing timu mbali mbali zinazoshiriki wenye ushindani wa medali ya dhahabu kusema kweli hadi sasa zote zinacheza kwa ufundi na umakini wenye kuleta ushindani labda dosari dogo ni kule kwa wenyeji China kupewa kadi nyekundu kwa wachezaji wake wawili kwenye mchezo mmoja. Lakini hilo si dosari kubwa kwani kadi ya njano na nyekundu ni sehemu ya mchezo ambapo utakua umecheza vibaya.

Vitendo vingine vibaya bado havipo kama kugomea mchezo na kupiga waamuzi. Nimeangalia pia mchezo wa kupiga mbizi hakuna matata kwenye kupiga shabaha, hivyo hivyo. Hata kwenye michezo ya mpira wa mikono kwa wanaume na wanawake nako pia ufundi na nidhamu ndio iliyotawala zaidi hali kadhalika kwenye mpira wa mchangani na hata mpira wa magongo na ule wa mezani, matarajio yangu haitakua hivihivi hadi mwisho wa michezo hii na watakiwa heri na fanakawa wenyeji China wazidi kupata medali.