Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-23 16:27:24    
Mustakabali wa maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu ni mzuri

cri

Mmkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu ulifunguliwa tarehe 31 mwezi Julai huko Beihai, mkoani Guangxi. Maofisa wa serikali, wataalamu na wanaviwanda karibu mia 6 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo China, Singapore, Philippines na Vietnam walihudhuria mkutano huo, ambapo walifanya majadiliano kuhusu kuhimiza ushirikiano mpya wa ukanda mdogo katika eneo la biashara huria kati ya China na Jumuiya ya Asia ya kusini mashariki, na wanaona kuwa mustakabali wa maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la  Ghuba ya Beibu ni mzuri.

Ghuba ya Beibu ni ghuba inayozungukwa na sehemu ya pwani ya mkoa unaojiendesha wa wa kabila la Wazhuang wa Guangxi, peninsula ya Leizhou ya mkoa wa Guangdong, sehemu ya magharibi ya mkoa wa Hainan na sehemu ya kaskazini mashariki ya Vietnam. Eneo la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la  Ghuba ya Beibu ni pamoja na China, Vietnam, Malaysia, Singapore, Indonesia, Philippines na Brunei, ambalo ni sehemu muhimu ya eneo la biashara huria la kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini mashariki. Ili kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi wa eneo hilo, kuanzia mwaka 2006 serikali ya mkoa wa Guangxi ikishirikiana na wizara na idara husika za serikali kuu ya China na mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo benki ya maendeleo ya Asia, inafanya mkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la Pan Ghuba ya Beibu kila mwaka.

Katibu wa kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China cha mkoa wa Guangxi Bw. Guo Shengkun alisema, kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la Pan Ghuba ya Beibu katika pande zote kunaendana na utandawazi wa uchumi duniani na wa kikanda, akisema,

"Tunafurahi kuona kuwa, tangu ushirikiano wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu kuanzishwa, unakubaliwa na kuungwa mkono na viongozi wa nchi mbalimbali za nchi za eneo hilo. Kutokana na uhimizaji wa pande mbalimbali, maoni ya pamoja ya ushirikiano huo yameanza kutekelezwa, na yamepata mafanikio ya kufurahisha."

Hivi sasa maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Umoja wa Asia ya Kusini mashariki unapata maendeleo mazuri, na kila upande umekuwa mwezi mkubwa wa nne wa kibiashara wa upande mwingine. Maendeleo ya haraka ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili yamezifanya China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja. Kwenye mkutano na waandishi wa habari wa mkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneokubwa la  Ghuba ya Beibu, naibu mkuu wa mkoa wa Guangxi Bw. Chen Wu alisema, mwaka 2007 thamani ya biashara kati ya China na jumuiya ya ASEAN ilikuwa dola za kimarekani bilioni 202.55, ambayo iliongezeka kwa asilimia 25.9 kuliko mwaka juzi. Thamani hiyo ilitimizwa mapema kwa miaka mitatu kuliko mpango wa awali.

Naibu mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Zheng Wantong aliusifu ushirikiano huo, akisema,

"Katika miaka ya karibuni, hali ya kisiasa na kiuchumi ya kimataifa ina utatanishi wengi, hasa bei za mafuta na nafaka zinaendelea kupanda, hatari ya mgogoro wa mikopo ya ngazi ya pili yanaongezeka nchini Marekani, na thamani ya dola za kimarekani inaendelea kupungua. Mambo yo yamekuwa shinikizo na changamoto mpya kwa ushirikiano wa kiuchumi wa ukanda mdogo. Katika hali hiyo, tunaweza kuona kuwa ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la Pan Ghuba ya Beibu bado unapata maendeleo na kuwavutia wawekezaji wengi."

Wakati utandawazi wa uchumi duniani unaendelea kupata maendeleo kasi, utandawazi wa uchumi wa kikanda na wa ukanda mdogo pia unaimarika siku hadi siku. Ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la Pan Ghuba ya Beibu unafuatiliwa zaidi ya jumuiya ya kimataifa. Katibu wa kudumu wa wizara ya biashara ya Thailand Bw. Pisanu Rienmahasarn alisema Thailand inapenda kushiriki kwenye ushirikiano huo. Kwenye mkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo la Pan Ghuba ya Beibu, mtaalamu wa uchumi wa Chuo Kikuu cha Columbia cha Marekani ambaye amesifiwa kuwa baba wa fedha za Euro Prof Robert A. Mundell alisema kutokana na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kiuchumi wa eneo hilo, pande mbalimbali za ushirikiano huo zimepata mafanikio makubwa yanayofuatiliwa na dunia. Kuhusu hali isiyo na uwiano ya maendeleo ya uchumi duniani, Prof. Mundell alipendekeza kuwa, pande mbalimbali zinatakiwa kujali maslahi ya pande nyingine, na kushirikiana katika pande zote, ili kuhimiza maendeleo ya ushirikiano huo.

Ikiwa ni moja kati ya idara zinazoandaa mkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu, benki ya maendeleo ya Asia inafuatilia na kuunga mkono ushirikiano huo wa ukanda mdogo. Naibu mkuu wa benki hiyo Bw. Lawrence Greenwood alisema, ushirikiano wa kiuchumi wa eneo hilo una fursa nyingi mpya za maendeleo, akisema,

"Kufanyika mkutano wa baraza la ushirikiano wa kiuchumi wa eneo kubwa la Ghuba ya Beibu mwaka huu kutasaidia eneo hilo kukabiliana na hali ya kudidimia kwa uchumi duniani ambayo huenda itatokea. Utandawazi wa uchumi ni muhimu kwa mafanikio ya Asia, pia unahimiza maendeleo ya pande zote hapa Asia na duniani. Benki ya maendeleo ya Asia inaunga mkono maendeleo ya ukanda huo mdogo."

Mafanikio muhimu ya mkutano wa baraza hilo ni kuanzishwa kwa kikundi cha wataalamu cha ushirikiano wa eneo la Pan Ghuba ya Beibu, ambacho kinaundwa na wataalamu wa China na nchi za Umoja wa Asia ya kusini mashariki na wajumbe wa benki ya maendeleo ya Asia.

Idhaa ya kiswahili 2008-09-23