Mkutano wa 8 wa Baraza la marais wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai ulifanyika tarehe 28 huko Dushanbe, mji mkuu wa Tajikstan. Kwenye mkutano huo, marais wa nchi 6 wanachama walisaini Taarifa ya Dushanbe ya Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai na nyaraka nyingine, na mkutano huo pia ulitoa taarifa ya pamoja ya mkutano, masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo yamefuatiliwa zaidi na watu.
Mtafiti wa Idara ya utafiti wa masuala ya Russia, Ulaya ya mashariki na Asia ya kati katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Jiang Yi alisema:
Suala la kwanza lililofuatiliwa na watu ni kuhusu suala la Osetia ya kusini. Kwani hii ni mara ya kwanza kwa marais wa nchi wanachama wa Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai kujadili suala moja linalofuatiliwa lililoko nje ya eneo la kazi ya jumuia hiyo. Na kutokana na Taarifa ya pamoja ya mkutano huo, tunaweza kuona kuwa, nchi zote wanachama wa jumuia hiyo zimeeleza ufuatiliaji wake kwa suala hilo na kueleza matumaini ya kuhimiza mazungumzo kuhusu suala hilo.
Kwenye mkutano huo nchi wanachama wa jumuia hiyo zimesaini "Kanuni za Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai kuhusu wenzi wa mazungumzo", hili pia ni suala linalofuatiliwa. Hivi sasa mbali na nchi 6 zilizo wanachama rasmi, Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai pia imepokea nchi 4 wachunguzi, na nchi nyingine pia zimeeleza matumaini ya kujiunga na jumuia hiyo, hivyo kusainiwa kwa kanuni hizo kutaziwezesha nchi hizo kutoa maombi ya kujiunga na jumuia hiyo. Mtafiti mwingine wa idara ya utafiti wa masuala ya Russia, Ulaya ya mashariki na Asia ya kati katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Sun Zhuangzhi alisema:
Mkutano huo umesaini kanuni hizo ambazo zina umuhimu maalum kwa ajili ya Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai kupanua zaidi mawasiliano na nje na kuongeza mvuto wake duniani, pia kuonesha msimamo wazi na ufunguaji mlango wa jumuia hiyo.
Kwenye mkutano huo, rais Hu Jintao wa China alitoa hotuba muhimu akizitaka nchi wanachama ziimarishe mshikamano, kutekeleza kikamilifu kwa muda mrefu "Mkataba wa ujirani mwema, urafiki na ushirikiano", na kujenga sehemu yenye masikilizano iliyo ya amani na usitawi wa pamoja. Hotuba hiyo imefuatiliwa na watu wa pande mbalimbali. Mtafiti Jiang Yi alisema:
Tokea Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai ianzishwe, China imekuwa kama kichwa cha gari moshi kwenye maendeleo ya jumuuia hiyo. Masuala aliyozungumzia rais Hu Jintao yote yanatakiwa kufuatiliwa zaidi na jumuia hiyo katika siku za mbele, na China pia inatakiwa kuonesha umuhimu wake katika kukamilisha zaidi ujenzi wa utaratibu wa jumuia hiyo, kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi na dawa za kulevya na kulinda usalama na utulivu wa kikanda; kuendeleza kwa kina ushirikiano wa uchumi ili kupata maendeleo ya pamoja.
Baada ya kuendelezwa kwa miaka 7, athari ya Jumuia ya ushirikiano ya Shanghai duniani imeongezeka siku hadi siku. Na miaka miwili ya hivi karibuni nchi wanachama wa jumuia hiyo zilifanya luteka za pamoja. Lakini mtafiti Sun Zhuangzhi alisisitiza kuwa, jumuia hiyo haiwezekani kuwa shirikisho la kijeshi, na hakika haiwezekani kuwa tishio au changamoto kwa nchi nyingine na jumuia nyingine za Kimataifa. Kwani tangu ianzishwe, imeeleza wazi kuwa jumuia hiyo ni jumuia moja ya ushirikiano wa kikanda, ushirikiano huo haulengi upande wa tatu wala kupinga nchi ya tatu. Jumuia hiyo inafuata moyo wa kufungulia mlango na kuhimiza maendeleo ya kikanda kwa njia ya amani.
|