Wizara ya mambo ya nje ya Georgia tarehe 2 ilitoa taarifa kwa ubolozi wa Russia nchini humo na kutangaza rasmi kuvunja uhusiano wa kibalozi na Russia. Wizara hiyo siku hiyo pia ilitangaza rasmi kuwa, Georgia inajitoa kwenye makubaliano yaliyosainiwa kati ya nchi hiyo na Russia kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Ossetia ya kusini. Wachambuzi wanaona kuwa, hatua hiyo ya Georgia imefanya uhusiano uliokwama kati ya nchi hizo mbili uwe mbaya zaidi, hali ya wasiwasi ya uhusiano huo pia imetoa changamoto kubwa kwa uhusiano kati ya Russia na Ulaya.
Wizara ya mambo ya nje ya Georgia iliutaka ubalozi wa Russia kusimamisha kazi rasmi kuanzia tarehe 3 mwezi huu, taarifa nyingine ya wizara hiyo pia inasema, kutokana na Georgia kutangaza kujitoa kwenye makubaliano ya utatuzi wa mgogoro wa Ossetia ya kusini, Georgia inalitaka jeshi la Russia liache ukaliaji wake nchini humo kwa kisingizo cha kulinda amani. Mjumbe wa Russia nchini humo Bw. Andrei Smaga tarehe 2 huko Tbilisi alisema, "ni kosa" kwa Georgia kutangaza kuvunja uhusiano na Russia, wanadiplomasia wa Russia wataondoka nchini humo hivi karibuni.
Lakini tukio hilo si jambo la kushangaza. Tarehe 26 mwezi Agosti Russia ilitangaza kutambua uhuru wa Ossetia ya kusini na Abkhazia. Bunge la Georgia tarehe 28 likapitisha azimio la kuitaka serikali ya nchi hiyo kuvunja uhusiano wa kibalozi kati yake na Russia. Tarehe 29 mwezi huu naibu waziri wa mambo ya nje wa Georgia Bw. Grigori Vashadze alitangaza kuwa nchi hiyo itarudisha wanadiplomasia wote isipokuwa balozi mdogo kutoka kwenye nchini Russia, na serikali ya nchi hiyo imetekeleza azimio lililopitishwa tarehe 28 na bunge la nchi hiyo. wachambuzi wanaona kuwa, baada ya Russia kutangaza kutambua uhuru wa sehemu za Ossetia ya kusini na Abkhazia, Gerogia kuvunja uhusiano na Russia ni suala la wakati tu. Georgia inaweza tu kupata uungaji mkono wa umma na misaada ya nchi za magharibi kwa kuchukua msimamo na hatua kali. Hali hii imepunguza zaidi uwekezano wa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili kuhusu mgogoro wa Ossetia ya kusini. Uhusiano kati ya nchi hizo mbili pia utakuwa wa wasiwasi katika muda mrefu ujao.
Uhusiano wa wasiwasi kati ya Georgia na Russia pia imeathiri uhusiano kati ya Russia na Ulaya. Katika siku za hivi karibuni, Umoja wa Ulaya umeilaani vikali Russia kutorudisha jeshi lake kutoka nchIni Georgia kutokana na makubaliano ya kusimamisha vita, na pia umeilaani Russia kwa kutambua uhuru wa Ossetia ya kusini na Abkhazia, hata umeonya kwa mara kadhaa kuweka vikwaza kwa Russia, uhusiano kati ya pande hizo mbili umeshuka chini kabisa baada ya vitu baridi. Lakini baada ya mawasiliano kadha ya kadha, Ufaransa ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa Umoja huo ililegeza msimamo wake na kutangaza kuwa umoja huo hautafanya uamuzi wa kuiwekea vikwazo Russia. Lakini Russia hina mahangaiko hata kidogo kukabiliana na "hatua kali" zitakazoweza kuchukuliwa na Umoja wa Ulaya na nchi za magharibi ikiwemo Marekani. Rais Dmitry Medvedev wa Russia alisema, "vita baridi au mambo yoyote mengine hayatishii Russia, na Russia haiogopi vita vipya vya baridi." Rais Dmitry Medvedev pia amesema, inayotaka Russia si "vita baridi", bali ni uhusiano halisi wa kiujenzi kati yake na nchi wenzi wa magharibi ikiwemo Marekani, lakini kutimiza lengo hilo kunahitaji moyo wa kutenda mambo halisi na nia ya pamoja ya pande mbili.
Umoja wa Ulaya na Russia ni majirani, kujenga uhusiano mwema na majirani ni sera muhimu ya umoja huo. Makubaliano ya ushirikiano na uhusiano wa wenzi yaliyosainiwa kati ya pande hizo mbili mwaka huu pia yanalenda kuimarisha uhusiano kati ya pande mbili. Wachambuzi wanaona kuwa, kutokana na hali ya hivi sasa, Russia na Ulaya zote hazipendi kuwa na migongano ya muda mrefu, kwa kuwa hainufaishi pande zote mbili.
|