Mkutano wa kwanza wa Baraza la carbon dioxide la Afrika unatazamiwa kufungwa tarehe 5 huko Dakar, mji mkuu wa Senegal baada ya kufanyika kwa siku tatu. Mkutano huo unalenga kuhimiza nchi zilizoendelea kuwekeza kwenye miradi ya "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" barani Afrika, ili kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
"Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi", kihalisi ni kama mbinu ya nchi zilizoendelea kwa kutimiza lengo lao la kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani. "Makubaliano ya Kyoto" yaliamua kuwa, kuanzia mwaka 2008 hadi 2012, nchi zilizoendelea za viwanda zinapaswa kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani kwa asilimia 5.2 kuliko ule wa mwaka 1990. Lakini gharama za kazi hiyo ya nchi zilizoendelea ni kubwa sana kuliko zile za nchi zinazoendelea, hivyo nchi nyingi zilizoendelea zimesema kuwa zina taabu ya kutimiza lengo. "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" unaziruhusu nchi zilizoendelea kupitia njia ya kutoa misaada ya mitaji na kuhamisha teknolojia kwa kuzisaidia nchi zinazoendelea kukuza nishati safi na kujenga miradi mingine inayosaidia kupunguza utoaji wa hewa ya carbon dioxide, ambapo kiasi cha upungufu wa utoaji wa hewa hizo kikithibitishwa kitachukuliwa kuwa matokeo ya kazi hiyo ya nchi zilizoendelea, kufanya hivyo kunaweza kusaidia nchi zilizoendelea kutimiza lengo lao la kupunguza hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani.
Hivi sasa miradi zaidi ya 1150 ya utaratibu huo imeanza kutekelezwa katika nchi 49, na mingine zaidi ya 2000 iko katika mchakato wa kusajiliwa. Kama miradi hiyo inaweza kutekelezwa vizuri, inatazamiwa kuwa, ifikapo mwaka 2012, utoaji wa carbon dioxide na hewa nyingine utapungua kwa tani bilioni 2.7. Katibu mtendaji wa ofisi ya ukatibu ya "Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa" Bw. Yvo de Boer alisema, "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" umepata mafanikio makubwa, ambao umetoa njia muhimu kwa ajili ya uwekezaji kwenye miradi ya kujipatia maendeleo bila uchafuzi, pia umehimiza uhamishaji wa teknolojia, ambapo nchi zinazoendelea zinaweza kubadilisha njia zao za uzalishaji mali na matumizi ili kuhifadhi mazingira zaidi.
Lakini wakati nchi nyingi zinazoendelea zinapopata manufaa kutokana na utaratibu huo, Afrika kama imekuwa bara linalosahauliwa. Ripoti iliyotolewa na Benki ya dunia wakati wa mkutano wa Baraza la carbon dioxide ilisema kuwa, hivi sasa miradi ya "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" kwa jumla imefikia 3902, lakini miradi 53 tu kati yao inatekelezwa barani Afrika. Ripoti hiyo inaona kuwa, sababu ya hali hiyo ni kwamba wawekezaji hawajui mengi juu ya hali ya barani Afrika. Hivyo Bw. Boer anataka mkutano huo uwawezeshe wawekezaji wafuatilie nchi za Afrika, pia amezihimiza nchi mbalimbali za Afrika zitumie fursa na kufanya mawasiliano na wawekezaji pamoja na mashirika mbalimbali ya Kimataifa, ili wawekezaji wawe na imani juu ya uwekezaji wao barani Afrika.
Watu waliohudhuria mkutano huo wanaona kuwa, nguvu kubwa ya sehemu za Afrika za kuanzisha "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" inawafurahisha. Ripoti ya benki ya dunia imedhihirisha kuwa, barani Afrika miradi ya nishati inayotoa kiasi cha chini cha carbon dioxide ambayo inalingana na "Mfumo wa kujipatia maendeleo bila uchafuzi" inafikia 3200, kama miradi hiyo yote itatimizwa, sehemu za Afrika zitaweza kupunguza utoaji wa hewa ya carbon dioxide kwa tani milioni 7.4. Bw. Boer ametaja zaidi kuwa, nchi za Afrika zina nguvu ya kuvutia uwekezaji katika miradi ya upandaji wa miti, kuondoa hali ya jangwa na kuendeleza utandawazi wa umeme vijijini. Muhimu zaidi ni kuwa, hivi sasa nchi za Afrika zimetambua kuwa, kuendeleza nishati safi kutaleta manufaa kwa maendeleo ya uchumi, hivyo zimeeleza matumaini yao makubwa ya kuendeleza nishati safi. Kwenye mkutano huo, nchi nyingi za Afrika zimetoa matakwa yao, kwa mfano, Nigeria inataka kujenga chuo kikuu ambacho kinategemea nishati ya jua kuzalisha umeme, Cote Divoire inataka kuyabadilisha mazao ya kilimo kuwa nishati, na Senegal inataka kujenga kiwanda cha kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo.
|