Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-10 19:54:29    
Hali ya mvutano wa kisiasa nchini Zimbabwe bado haijaondolewa

cri

Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini tarehe 8 alikwenda tena Harare, mji mkuu wa Zimbabwe ili kufanya juhudi za mwisho kwa ajili ya kuondoa hali ya mvutano wa kisiasa kati ya vyama mbalimbali vya Zimbabwe. Lakini hadi kufikia usiku wa tarehe 9, mazungumzo kati ya pande mbalimbali bado hayajapata maendeleo, ambapo pande hizo hazijafikia makubaliano kuhusu kugawa madaraka.

Chini ya usuluhishi wa rais Mbeki, viongozi wa pande tatu za Chama tawala cha ZANU PF cha Zimbabwe, na makundi mawili ya chama cha upinzani MDC wamehudhuria mazungumzo hayo.

Baada ya mazungumzo hayo kumalizika, rais Mugabe aliwaambia waandishi wa habari kuwa, ingawa hivi sasa vyama mbalimbali bado havijafikia makubaliano yoyote kuhusu kugawa madaraka, lakini mazungumzo hayo yanaendelea na hayarudi nyuma, ambayo ni mazungumzo yanayohimiza pande mbalimbali zifanye juhudi. Msemaji wa kundi la Tsvangirai la chama cha upinzani cha MDC Bw. Nelson Chamisa alisema, majadiliano bado yanaendelea. Hivi sasa pande mbalimbali zinajitahidi kutafuta maoni ya pamoja, ingawa migongano bado ni mikubwa sana, lakini pande mbalimbali zinajitahidi kuipunguza. Na kiongozi wa kundi lingine la chama cha upinzani MDC Bw. Arthur Mutambara alisema, ingawa mikwaruzano kati ya pande mbalimbali bado ni mikali, lakini ana matumaini juu ya mustakabali wa mazungumzo hayo.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe alisema, Rais Thabo Mbeki wa Afrika kusini atakaa nchini Zimbabwe zaidi ya siku mbili, ambapo atafanya mazungumzo na viongozi wa vyama mbalimbali vya Zimbabwe. Kabla ya hapo, rais Mbeki ni msuluhishi wa hali ya Zimbabwe aliyekabidhiwa kazi hiyo na Umoja wa maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC, na alifanya usuluhishi mara kwa mara. Mwezi uliopita, mkutano wa mwaka wa Jumuia ya SADC ulifanyika nchini Afrika kusini, Bw. Mbeki amekuwa mwenyekiti wa zamu wa jumuia hiyo. Ndiyo maana kutatua vizuri msukosuko wa kisiasa nchini Zimbabwe baada ya uchaguzi mkuu, na kuhimiza vyama mbalimbali vya nchi hiyo vifikie makubaliano ya kugawa madaraka, kumekuwa kazi moja kuu ya chombo cha uongozi cha Jumuia ya SADC. Ziara hii ya Bw. Mbeki nchini Zimbabwe pia ni kwa ajili ya kukamilsiha jukumu la usuluhishi alilopewa na Jumuia ya SADC.

Mazungumzo kati ya vyama mbalimbali vya Zimbabwe yalianza kufanyika baada ya kusainiwa kumbukumbu ya maelewano kati ya pande mbalimbali tarehe 21 Julai mwaka huu. Na mazungumzo hayo yalifanyika mara nyingi nchini Afrika ya kusini na Zimbabwe katika muda wa zaidi ya mwezi mmoja, ambapo pande mbalimbali zilizoshiriki kwenye mazungumzo hayo yameafikiana kuhusu ajenda 13 kati ya 14, lakini zilikwama kwenye suala la mwisho yaani suala muhimu zaidi kuhusu kugawa madaraka. Kwani chama cha upinzani cha MDC kikiwa chama kikubwa zaidi kwenye bunge la awamu mpya kimekataa pendekezo kuhusu rais wa sasa Robert Mugabe aendelee kudhibiti mambo ya usalama wa nchi. Ni vigumu kupata maendeleo kwa mazungumzo kuhusu kugawa madaraka, ambapo kuna mwelekeo wa kuzidi kuwa mbaya kwa hali ya mambo. Rais Mugabe juzijuzi alisema, kama kiongozi wa chama cha MDC Bw. Tsvangirai anashikilia kukataa kusaini makubaliano ya kugawa madaraka, yeye mwenyewe ataunda Baraza la mawaziri bila kushirikisha chama cha upinzani. Juu ya hayo, Bw. Tsvangirai alisema kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na chama cha upinzani tarehe 7 kuwa, kama hali ya mvutano ya hivi sasa haitaondolewa, Zimbabwe inapaswa kufanya mara nyingine uchaguzi mkuu chini ya usimamizi wa jumuia ya Kimataifa. Alisema, bora kutofikia makubaliano, chama chake hakitaweza kupokea makubaliano yasiyo na mafanikio.

Wachambuzi wameona kuwa, safari hii rais Thabo Mbeki atajitahidi kuvifanya vyama mbalimbali vya Zimbabwe vitafute maoni ya pamoja huku kuwela kando migongono kati yao, ili kupata mfumbuzi wa kuondoa hali ya mvutano.