Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-10 20:39:39    
Mapishi ya vipapatiro vya kuku

cri

Mahitaji:

Vipapatiro vya kuku gramu 500, vitunguu gramu 100, figili gramu 100, pilipili hoho gramu 20, vitunguu saumu gramu 20, tangawizi gramu 15, cumin vijiko viwili, mchuzi wa sosi vijiko viwili, sukari vijiko viwili, mvinyo wa kupikia kijiko kimoja, chumvi kijiko kimoja, mafuta ya ufuta kijiko kimoja , chembechembe za pilipili manga kijiko kimoja

Njia:

1. kata vitunguu maji viwe vipande, kata figili iwe vipande, kata pilipili hoho iwe vipande.

2.kata vipapatiro vya kuku viwe vipande viwili na koroga pamoja na mchuzi wa sosi, mvinyo wa kupikia na chembechembe za pilipili manga.

3.washa moto, mimina mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vipapatiro vya kuku kwenye sufuria vikaange mpaka viwe hudhurungi, vipakue. Washa moto tena, tia vipande vya tangawizi, vitunguu saumu, pilipili hoho, korogakoroga, tia vipande vya figili na vitunguu saumu korogakoroga, tia vipande vya vipapatiro vya kuku, korogakoroga, tia mchuzi wa sosi, sukari, cumin, chumvi ,korogakoroga, mimina mafuta ya ufuta , ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.