Kama ilivyokuwa miaka iliyopita, tarehe 11 Septemba serikali ya mji wa New York ilifanya maadhimisho ya miaka saba tangu tukio la "Septemba 11" litokee kuwakumbuka watu waliokufa katika tukio hilo. Usiku wa siku hiyo kwa saa za huko, kama kila mwaka ilivyofanywa, kurunzi mbili zitawaka na kutoa mwali mbili za mwangaza kwenye mahali kilipokuwa Kituo cha Biashara Duniani kwa kumithilisha majengo marefu mawili ya kituo hicho yaliyobomolewa katika tukio hilo ili watu wawakumbuke marehemu.
Kwa mujibu wa mpango wa maadhimisho, meya wa New York Michael Bloomberg pamoja na watu wa jamii watatulia kimya na kuomba katika asubuhi ya siku hiyo saa 2 na dakika 46, saa 3 na dakika 3, saa 3 ma dakika 59 na saa 4 ma dalola 29. Saa hizo zilikuwa ni wakati ndege mbili za abiria zilipogonga jumba la kaskazini na la kusini na majumba hayo mawili yalipoporomoka. Kwenye maadhimisho, majina ya watu 2751 waliokufa katika maporomoko ya majumba hayo watatajwa. Ingawa miaka 7 imepita tangu tukio la "Septemba 11"litokee, lakini baadhi ya wamerikani wanaona kama lilitokea siku ya jana. Maadhimisho ya kila mwaka yanawahuzunisha na kuwaumiza roho zao.
Wakati wanapowakumbuka waliokufa huwasahau watu waliojeruhiwa kwenye tukio hilo, ambao walinusurika kwa bahati, lakini baadaye wamekuwa kundi la watu wenye bahati mbaya katika jamii. Kabla ya tukio hilo Bi. Lauren Manning alifanya kazi katika Wall Street, lakini siku moja tu maisha yake yamebadilika kabisa. Kutokana na kuungua vibaya kwenye tukio la tarehe 11 Septemba, alilala kitandani wiki kadhaa na baada ya miezi kadhaa aliondoka hospitali na kurudi nyumbani. Hivi sasa na hata katika majira ya joto alilazimika kuvaa nguo ndefu, hawezi kutoka nje kutembea na mbwa wake kama alivyokuwa zamani, kwani mbwa akikimbia na kumvuta, ngozi yake itapasuka, na hata hawezi kuwapikia chakula watu wa familia yake, kwa sababu hata tone la mafuta lingeweza kumwathiri vibaya ngozi yake.
Watu waliojeruhiwa kama Bi. Lauren Manning ni wengi, lakini mpaka sasa bado hakuna hesabu sahihi ya idadi ya jumla ya watu hao. Wakati kumbukumbu za tukio la "Septemba 11" zinapokuwa hafifu akilini mwa watu, msiba wa majeruhi hao bado hautatoweka. Kwa mujibu wa takwimu, kati ya ruzuku za dola za kimarekani bilioni 7 kwa ajili ya watu walioathirika katika tukio la "Septemba 11" bilioni 6 zilitolewa kwa watu waliokufa katika maporomoko ya majumba, mashambulizi ya Pentagon na ndani ya ndege za abiria, majeruhi walipewa dola za Marekani bilioni moja na kati yao wengi zaidi ni wazima moto na wagonjwa wa pumu. Licha ya watu walioathirika moja kwa moja, wakazi waliokuwa karibu na Kituo cha Biashara Duniani pia wameathirika kiafya na kisaikolojia.
Uchunguzi wa kiafya umeonesha kuwa katika muda wa miezi 10 tangu tukio la "Septemba 11" litokee, zaidi ya nusu ya watu walioshuhudia tukio hilo walikuwa na matatizo ya mapafu na wengi wana matatizo ya kisaikolojia. Aidha, Wamarekani wenye asili ya China walioathirika pia ni wengi kwenye sehemu ya Kituo cha Biashara ya Dunia. Tarehe 11 Septemba mwaka jana hospitali moja ya huko ilianzisha kituo cha afya kwa ajili ya kuwasaidia wakazi kwenye sehemu hiyo. Hadi sasa waliokwenda kutibiwa katika kituo hicho thuluthi mbili ni Wamerekani wenye asili ya China, na wengi wao ni wagonjwa wa pumu. Lakini kadiri muda unavyozidi kupita, watu watafuatilia zaidi watu waliojeruhiwa kimwili na kisaikolojia katika tukio la "Septemba 11". Serikali ya Marekani hivi sasa iko tayari kutoa msaada wa kifedha kuwasaidia watu hao kurejesha hali ya kawaida ya afya na maisha.
|