Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-17 15:53:29    
Mafundi wanaotoa uhakikisho wa upashanaji habari kwa ajili ya michezo ya Olimpiki

cri

Michezo ya Olimpiki ya kusisimua imemalizika, mashindano ya siku 16 ya michezo hiyo imewapa watu kumbukumbu nyingi, lakini kwa baadhi ya watu, kumbukumbu kuhusu michezo ya Olimpiki si mashindano, bali ni vifaa na waya mbalimbali zilizoko kwenye majumba ya michezo. Katika kipindi hiki, tatawaelezeni kuhusu wafanyakazi wanaotoa uhakikisho wa upashanaji habari kwa ajili ya michezo ya Olimpiki.

 

Kampuni ya huduma za mtandao ya China CNC ni mwenzi wa ushirikiano wa huduma za mawasiliano ya habari kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing, kampuni hiyo ilitandika waya zaidi ya elfu moja ya mawasiliano yenye urefu wa kilomita zaidi ya elfu 10 kwenye majumba na viwanja 37 vya michezo, na waya hizo zimekuwa njia ya kutangaza mamia ya mashindano ya michezo hiyo kwa televisheni ya picha ya hali ya juu. Na kwa kutumia mtandao wa VLAN ulioanzishwa na kampuni hiyo, wapiga picha kutoka nchi mbalimbali duniani wanaweza kutuma picha walizozipiga kwa njia rahisi na ya haraka. Tunaweza kusema kuwa, ndiyo kutokana na kazi za kampuni ya huduma za mtandao ya China CNC, watu walioko kote duniani wakaweza kutazama kwa pamoja michezo hiyo ya Olimpiki isiyoshindikana. Maneja anayeshughulikia mambo ya teknolojia ya majumba ya kulenga shabaha katika kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing Bw. Li Bin alisema, huduma ilizozitoa kampuni ya CNC na mafundi yake wote ni hodari sana. Bw. Li Bin alisema:

"hasa kuhakikisha vyombo watangazaji wenye hakimiliki walimaliza utangazaji wa mashindano 15 katika siku 9 bila matatizo, ishara ya mashindano hayo yote haikukatika na ilikuwa nzuri sana wakati wote. Waandishi wa habari wanaweza kuitangaza mara moja habari walizozipata. Mwandishi mmoja wa Uholanzi aliwahi kuniambia kuwa hawakutegemea kwamba mtandao wa hapa ni wa kasi sana, na wanaweza kufungua haraka tovuti za nchi za nje. Sasa michezo ya Olimpiki ya Beijing imemalizika kwa mafanikio, nalishukuru kundi la kampuni ya CNC kwa misaada yake mikubwa."

Kwenye majumba na viwanja mbalimbali vya michezo, ili kuhakikisha mfumo wa mawasiliano ya habari kuhusu mashindano unafanya kazi bila matatizo, mafundi wa kampuni ya CNC wanafanya upimaji wa vifaa vyote na njia za mtandao kila siku.

kwenye kipindi cha maandalizi ya mwanzo ya jumba la mpira wa kikapu la Wukesong, jumba hilo lilifungwa kuanzia tarehe 23 mwezi Julai, ambapo watu na vifaa havikuruhusiwa kuingia kwenye jumba hilo. Lakini tarehe 21 mwezi huo, vifaa kadhaa viligunduliwa kuwa havikuweza kuunganishwa kwenye mtandao, baada ya kufanyiwa upimaji na vikundi vinne vya mafundi, hatimaye waligundua kuwa hali hiyo si tatizo la uunganisho la waya za mawasiliano, bali ni kwamba vifaa hivyo vyenye nguvu ndogo haviwezi kutumia mtandao wa jumba la michezo. Lakini wakati huo haikuwezekana kubadilisha vifaa vingine, kwa hivyo baada ya kufanya majadiliano ya usiku mzima, kundi la CNC hatimye liliamua kumaliza kazi hiyo kwa kushindana na wakati, yaani walikuwa wanatakiwa kumaliza kazi za siku 4 hadi 5 ndani ya siku moja na kutandika tena waya ya aina mpya kwa kuzunguka jumba hilo. Ofisa wa kundi la CNC aliyewajibika na jumba hilo Bw. Li Yang alisema:

"saa 2 asubuhi ya tarehe 22, kundi la wafanyakazi 50 liliingia kwenye jumba hilo na kuanza kazi ya kutandika waya mpya yenye urefu wa mita 2000 kuzunguka jumba hili, saa moja usiku wa siku hiyo, kazi hiyo ilimalizika. Saa 2 usiku, vifaa vyote vilirejea kwenye hali ya kawaida na kuweza kutumika."

Mashindano ya mpira wa kikapu yanafuatiliwa sana kwenye michezo ya Olimpiki, mafundi wa CNC waligawanyika kwa vikundi viwili na kufanya kazi kwa zamu. Saa 12 asubuhi waliingia kwenye jumba na kufanya maandalizi, walipoondoka jumba hilo baada ya mashindano kwa kawaida ilikuwa ni saa 9 alfajiri. Katika siku tatu za mwanzo za mashindano, watumiaji wengi walianza kutumia mtandao, wakati mashindano ya mpira ya kikapu kati ya China na Marekani yalipofanyika, kazi za huduma za mawasiliano ya habari zilikuwa ni nyingi zaidi, katika siku hizo tatu, Bw. Li Yang na wenzake kwa jumla walilala kwa saa 4 tu. Alipoulizwa kuwa walimaliza vipi kazi hizo ngumu, Bw. Li Yang alisema:

"nadhani tuliweza kumaliza kazi hii kwa nia thabiti, kwa ajli ya China, kwa ajili ya kuonesha China, kuonesha Beijing na kuonesha kampuni yetu CNC kwa dunia. Kwa kweli hii ni fursa nzuri kwangu, huenda ni fursa ya pekee katika maisha yangu kuhudumia michezo ya Olimpiki."

Watu wa kote duniani wameweza kutazama michezo ya Olimpiki bila matatizo kutokana na kazi za mafundi hao wa CNC, lakini kwa watazamaji, mafundi hao hawakuonekana kama wafanyakazi wengi wengine wa michezo hiyo. michezo ya Olimpiki ni tamasha kubwa, watu wa rangi mbalimbali kutoka nchi na sehemu mbalimbali walikusanyika pamoja, kushiriki ndio ni ushujaa, bila kujali kwenye jukwaa la kukabidhi medali na nje ya majumba ya michezo. Tuwashukuru watu wale waliojitolea kufanya kazi na kutoa mchango kwa ajili ya michezo hiyo bila kujitokeza.