Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-18 18:43:45    
Mwongozaji mkuu wa sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Beijing Bw. Zhang Jigang

cri

Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ilifunguliwa Tarehe 6 Septemba, sherehe ya ufunguzi huo iligusa hisia za watu na kuwapa picha nzuri zisizosahauliwa.

Mliosikia ni wimbo uitwao "Kwenye eneo la mbinguni" ulioimbwa na mwimbaji mlemavu asiyeweza kuona Bw. Yang Haitao. Mwimbaji huyo alipoimba wimbo huo, ndege aliyemithilisha mwangaza wa jua akiruka angani na kutua kwenye ardhi ya majani,

Baada ya kuimba wimbo, mwimbaji Yang Haitao aliwaambia watazamaji wa uwanjani akisema, "kama nigeweza kupata siku tatu za kuona nigetaka kuwaona baba yangu, mama yangu na niye mliopo." mara watazamaji walisisimka sana.

Katika sherehe ya ufunguzi wa michezo, maonesho ya michezo ya sanaa yaliyogusa hisia za watu ni mengi. Bw. Zhang Jigang alisema,

"Maonesho ya michezo ya sanaa katika sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki inatakiwa kuonesha hali ya kawaida na ya utukufu, iwe ya kusisimua na kuwa kama ya njozi huku ikionesha moyo wa walemavu wa kujiendeleza bila kuogopa taabu."

Walemavu 400 walishiriki katika maonesho ya michezo ya sanaa kwenye sherehe ya ufunguzi huo. Ili kufanikisha sherehe hiyo ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya walemavu, Bw. Zhang Jigang pamoja na wenzake mara nyingi walifanya mazungumzo na wachezaji walemavu wa michezo ya sanaa na kujadiliana nao kuhusu usanii na maisha, ambapo ufahamu walionao walemavu kuhusu maana ya maisha uligusa sana hisia zao, na kuwahimiza waoneshe kadiri wawezavyo mada ya kusifu "maisha ya binadamu yenye uvumbuzi, maadili ya watu na ubinadamu".

Kwenye sherehe hiyo, ngoma iitwayo: "Kuendelea daima kucheza Dansi" hapo awali ilipangwa kuchezwa na Kundi la Wasanii Walemavu, lakini baadaye msichana Li Yue mwenye umri wa miaka 11 aliyepoteza mguu wake wa kushoto katika tetemeko la ardhi la Wenchuan alichaguliwa kucheza ngoma hiyo. Msichana Li Yue alisema "Ingawa nimepoteza mguu wangu wa kushoto, lakini sitaacha ndoto yangu niliyokuwa nayo ya kucheza ballet." Bw. Zhang Jigang aliposikia hayo alirowa na machozi na akamchagua papo hapo.

Katika maonesho hayo ya ngoma, msichana Li Yue alikaa kwenye kiti cha magurudumu akiwa amevaa kiatu kimoja cha ballet na kucheza kwa mikono. Walemavu wasioweza kusikia walimzunguka na kucheza dansi kwa mikono kwa kumithilisha miguu ya msichana Li Yue. Mchezaji hodari wa ballet Bw. Lu Ming alimwinua juu na kuzunguka zunguka huku skati ya msichana huyo ikipeperuka......

Ni kama gazeti la michezo la Hispania "Marca" lilivyosema, kwamba kwa mara nyingine tena michezo ya sanaa katika sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu inavutia sana.

Shirika la Habari la Ufaransa lilichapisha makala ikisema maonesho ya michezo ya sanaa kwenye sherehe ya ufunguzi huo yameleta mazingira kama ya peponi, Beijing ikiwa na lengo la kuifanya sherehe ya ufunguzi huo iwe na hali murua isiyosahaulika na kuvutia dunia, basi lengo hilo limetimizwa.

Sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Beijing imewavuta watu wa dunia, hii inatokana na juhudi za muda mrefu alizofanya Bw. Zhang Jigang kuhusu michezo ya sanaa ya walemavu.

Bw. Zhang Jigang alizaliwa mkoani Shanxi miaka 50 iliyopita, alipokuwa na umri wa miaka 12 alianza kujifunza kucheza dansi na alipokuwa na umri wa miaka 17 alianza kutunga michezo ya dansi. Katika muda wa miaka 30 iliyopita alitunga opera ya dansi, opera ya nyimbo, opera ya muziki na michezo ya dansi zaidi ya 300 na michezo hiyo iliwahi kuoneshwa katika nchi zaidi ya 60. Bw. Zhang Jigang alisema, uwezo wake wa kutunga michezo ya sanaa unatokana na kuchunguza maisha kwa makini. Alisema,

"Msanii anapaswa kupata virutubisho kutoka kwa maisha halisi ya kila siku, msanii lazima awe mwepesi wa kugundua mambo maishani. Mara kwa mara tunakwenda kujiunga na maisha ya watu wa jamii fulani, lakini kwa nini baadhi ya watu wamevuna kitu na wengine hawakupata? Kwa hiyo ni muhimu kwa msanii kuwa mwepesi wa kugundua mambo ya maishani."

Mwaka 1994 alipokuwa mwongozaji mkuu wa michezo ya sanaa kwemue sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Walemavu ya Yuan Nan alianza kujihusisha na sanaa ya walemavu.

Mwaka 2000 kwa kushirikiana na wasanii wengine alitunga michezo ya dansi iitwayo "Ndoto Yangu", kati ya michezo hiyo mchezo wa dansi wa "Budha Guanyin Mwenye Mikono Elfu Moja" unajulikana na kusifiwa kote duniani. Mchezo huo unachezwa na walemavu wasioweza kusikia na kuongea kwa vitendo na kuinama, kuinuka, kuzunguka na kugeukia upande, kueleza jinsi mungu huyo anavyowapenda na kuwahangaikia wanadamu. Kwa sababu wachezaji hao wote ni walemavu wanacheza kwa kuangalia ishara ya mikono aliyotoa mwongozaji wa mchezo huo. Bw. Zhang Jigang alisema, alipokuwa pamoja na walemavu katika kufanya mazoezi ya kucheza dansi hiyo, alitiwa moyo sana na nia yao ya kuthubutu kupamana na matatizo ya kimaisha bila kuogopa taabu kubwa, aliona wachezaji hao ingawa wana ulemavu, lakini kisaikolojia wao ni watu wasio na ulemavu.

Mwaka 2004 mchezo wa "Budha Guanyin Mwenye Mikono Elfu Moja" ulihaririwa na kushiriki katika sherehe za ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Athens. Bw. Zhang Jigang alisema,

"Naona Kikundi cha Wasanii Walemavu cha China ni cha ngazi ya juu duniani, maendeleo yake hayawezi kutengana na uungaji mkono wa serikali na wasanii wa fani mbalimbali."

Tarehe 17 Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Beijing imefungwa, Bw. Zhang Jigang pia ni mwongozaji mkuu wa maonesho ya michezo ya sanaa kwenye sherehe ya ufungaji wa michezo hiyo. Alisema, sherehe ya ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Beijing ni sherehe ya mwisho katika kipindi cha Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Kwa hiyo michezo katika sherehe hiyo imeonesha matumaini mema, upendo, hali ya kupatana kati ya binadamu na dunia ya asili.