Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo ya milenia, Shirika la kusaidia maendeleo ya wanawake la Umoja wa Mataifa tarehe 18 lilitoa ripoti kuhusu maendeleo ya hali ya wanawake duniani wa mwaka 2008 hadi mwaka 2009, ripoti hiyo imezitaka nchi mbalimbali na mashirika mbalimbali ya Kimataifa yaanzishe taratibu za kubeba wajibu kwa nguvu zaidi, na kutimiza vizuri zaidi ahadi zao kuhusu kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon siku alisema, serikali inayohakikisha haki na maslahi ya wananchi ndiyo serikali inayobeba wajibu kikweli. Alisema:
Kama kuna watu watakaoniuliza kuwa kwa nini ninaunga mkono kuanzisha taratibu za kubeba wajibu zenye ufanisi zaidi kwa ajili ya kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake, ningependa kuwaambia wote, kwa sababu naona kuwa serikali inayofuatilia haki na maslahi ya wanawake ndiyo serikali inayoweza kufuatilia kila mtu na kubeba wajibu wake.
Ripoti hiyo imedhihirisha kuwa, kutoa ahadi hadi kutimiza ahadi kuhusu kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake kunatakiwa kushika njia ndefu. Hivi sasa ingawa hali ya kuishi ya wananchi duniani imeboreshwa kwa kiasi kikubwa, lakini hali ya wanawake bado inakabiliwa na changamoto na taabu kubwa. Takwimu zimeonesha kuwa, miongoni mwa watu wanaofanyika kazi nyumbani na wasio na mapato ya kudumu, asilimia 60 ni wanawake; wastani wa mapato ya wanawake wenye ajira ni chini kuliko yale ya wanaume kwa asilimia 17; theluthi moja ya wanawake walishambuliwa kimabavu kutokana na hali ya kijinsia; na katika baadhi ya sehemu duniani, kila wanawake 10, mmoja kati yao alikufa kwa sababu ya kupata mamba au kujifungua.
Ripoti hiyo ilidhihrisha kuwa, kazi ya kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake ni lazima iwekwe ndani ya mfumo wa usimamizi wa kazi wa serikali, na kazi hiyo inapaswa kuwa kazi kubwa ya kukagua mafanikio ya kazi za kila ofisa wa utawala wa serikali. Ripoti hiyo pia imefafanua kila lengo la malengo ya maendeleo ya milenia, na kudhihirisha kuwa serikali za nchi mbalimbali na mashirika mbalimbali ya Kimataifa yanatakiwa kuchukua hatua za dharura katika mambo matato ya usimamizi wa kazi ya utawala, huduma za umma, uchumi, utekelezaji wa haki wa sheria na utoaji misaada ya Kimataifa. Mkurugenzi utendaji wa Shirika la kuwasaidia wanawake la Umoja wa Mataifa Bw. Ines Alberdi alisema, kufuatilia kazi ya kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake kunahusiana moja kwa moja na kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa. Alisema:
Wiki ijayo, wakuuu wa serikali za nchi mbalimbali watakusanyika New York na kujadili malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa, ambapo suala kuhusu kuhakikisha haki na maslahi ya wanawake litaonekana kuwa ni muhimu zaidi. Ripoti hiyo imeonesha kuwa, kama tutafahamu zaidi wajibu wetu wa kutimiza ahadi zetu, basi tutapiga hatua kubwa kwa kuelekea kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia.
Bw. Alberdi alisema, ingawa ripoti hiyo imesisitiza kuwa kazi ya kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake inakabiliwa na changamoto kubwa, lakini imedhihirisha zaidi ukweli wa mambo ambao mamilioni ya wanawake duniani wamefanya juhudi zisizolegalega kwa ajili ya kubadilisha hali ya maisha yao. Ofisa wa Shirika la kuwasaidia wanawake la Umoja wa Mataifa Bibi Anne Marie Goetz ni mtungaji wa ripoti hiyo, alisema, ripoti hiyo imetaja matatizo, pia imewaambia watu namna ya kutatua matatizo hayo. Alisema:
Wananchi wa nchi mbalimbali duniani wametoa maoni na mapendekezo yao ya kutatua matatizo yanayowakabili, hii ni sababu yetu ya kutoa mbinu na njia nyingi za kuhimiza juhudi za watu kwa ajili ya kutatua matatizo hayo, ili kutusaidia kutimiza ahadi tulizotoa kuhusu kuhakikisha na kuboresha haki na maslahi ya wanawake.
|