Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-23 20:25:56    
Barua 0923

cri

Wasikilizaji wapendwa, Bw. Suleiman Kumchaya aliwahi kuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio China Kimataifa kuanzia mwaka 1993 hadi mwaka 1998. Baada ya kurudi nyumbani Tanzania alikuwa msaidizi wa rais wa Tanzania, na sasa amekuwa mbunge wa Mtwara, Tanzania. Juzijuzi amefika Beijing, China na kutembelea Radio China Kimataifa. Alipozungumza na mtangazaji wetu alisema anapenda kuja China kujionea mabadiliko makubwa yaliyopatikana mjini Beijing, ambayo yamemshangaza sana; kukutana na marafiki zake wachina, kutafuta fursa ya kuwavutia wachina kwenda Tanzania kuwekeza vitega uchumi; hasa anapenda kuendelea na juhudi za kuhimiza ushirikiano kati ya China na Tanzania, na ushirikiano kati ya Radio China Kimataifa na Radio Tanzania Dar es salaam. Sisi pia tumeeleza matumaini yetu kwamba ushirikiano kati ya China Radio Kimataifa na Radio Tanzania Dzar es Salaam utaanzishwa mapema iwezekanavyo.

Msikilizaji wetu Yaaqub Saidi wa sanduku la posta 124 Kakamega Kenya ametuletea barua akisema kuwa, Pokeeni salamu nyingi kutoka kwake akitarajia sote watangazaji, viongozi, na wafanyakazi wa idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa tu wazima kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, tukiendelea na kuwahudumia wasikilizaji wetu kwa matangazo na vipindi vya kuelimisha, kufahamisha na hatimaye kuburudisha wasikilizaji wetu wa huko sehemu mbalimbali duniani.

Hapa anapenda kuandika barua na kuelezea aliyo nayo pasina mwanzo kuwapa mkono wa huzuni na kuwafariji kwa kuwapa moyo wa kusubiri na kuvumilia watu waliopata athari kutokana na maafa yaliyosababishwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mkoani Sichuan ambapo mamia na maelfu ya watu walifariki, walilemazwa, miundo mbinu iliharibiwa, majumba yalibomolewa na hatimaye vivutio vya utalii mkoani Sichuan viliharibiwa kwa kiasi kikubwa. Changamoto ni kuwa Jumuia ya Kimataifa kujitokeza kwa hali na mali kuwasaidia ndugu zetu wachina kwa kuwapa vyakula, mavazi vyandarua, maji safi, matibabu na dawa na pia kusaidia katika kukarabati upya majengo na miundo mbinu kama vile barabara, reli na viwanja vya ndege na kwa kutoa misaada ya kifedha ya kuwasaidia watu walionusurika na wahanga wa tetemeko hilo. Anachukua fursa hii kuwapongeza maofisa wa serikali ya China na wananchi wake wakiongozwa na rais na waziri mkuu kwa kuonesha nguvu kubwa na kujitolea kwao katika kuwashughulikia watu waliokufa na watu walionusurika kwenye tetemeko hilo la ardhi kwa kuwatuma wanajeshi kuwaokoa ndani ya majengo yaliyobomolewa baada ya kishindo cha tetemeko hilo la ardhi. Pia hana budi kuwapongeza wanajeshi kwa kufanya kila jitihada kuwaokoa watu bila kupata mapumziko usiku na mchana, nami nawatakiwa kila la heri na ana matumaini kuwa watadumisha moyo huo wa kuwasaidia wananchi.

Redio China Kimataifa haikubaki nyuma katika kuwafahamisha wasikilizaji na watazamaji wa CCTV kuhusu matukio mbalimbali mkoani Sichuan na hatua mbalimbali zilizokuwa zikichukuliwa na serikali ya watu wa China na Jumuia ya Kimataifa kuwasaidia watu walioathiriwa kwenye tetemeko hilo la ardhi, anarudi kwa lengo la kukuandikia barua hii, kwanza anapenda kukufahamisheni kwamba nimepata jarida la China Today la mwezi Aprili mwaka huu 2008, pamoja na kadi za salamu. Hivyo basi anachukua fursa hii kukushukuruni kwa jarida hilo ambalo mna makala mbalimbali yenye mafunzo. Pia anaomba wahariri wa jarida hilo kuanzisha jarida la China la leo kwa lugha ya Kiswahili.

Ana wingi wa matumaini kwamba pendekezo hili lake litazingatiwa na viongozi wa wahariri. Pia ameambatanisha fomu tuliomtumia kujaza kuhusu jarida la "China Today".

Tunamshukuru kwa dhati Bw. Yaaqub Saidi kwa barua yake ya kuwapa moyo watu walioathiriwa kwenye tetemeko kubwa la ardhi lililotokea huko Wenchuan mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China.