Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-24 19:47:16    
Watu wenye tabasamu waonesha sura nzuri ya Beijing

cri

Katika Michezo ya Olimpiki ya Beijing iliyomalizika siku chache zilizopita, kuna watu wanaojitolea milioni 1.47 waliotoa huduma katika kazi mbalimbali zikiwemo maandalizi ya mashindano, usalama, mawasiliano, utoaji huduma kwa vyombo vya habari na uendeshaji wa mji. Huduma zilizotolewa nao zimesifiwa sana duniani. Hivyo kwenye sherehe ya kufungwa kwa Michezo ya Olimpiki, kamati ya Olimpiki ya kimataifa kwa mara ya kwanza iliongeza sherehe ya kuwapa maua kwa wajumbe wa watu wanaojitolea.

"Kama una maswali yoyote kuhusu Michezo ya Olimpiki, unaweza kutupigia simu: 0086-10-12308. Au unaweza kutembelea tovuti yetu: www.2008beijing.cn."

Mliosikia ni sauti ya Bibi Panthipa Asavatheputhai aliyetoka Thailand. Yeye ana umri wa miaka 25, na alitoa huduma kwa watazamaji wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing. Mwaka 2004, Panthipa Asavatheputhai alikuja kusoma nchini China, na tokea hapo alianza kuifahamu China na kufuatilia Michezo ya Olimpiki ya Beijing.

Kwa kuwa wachezaji, waandishi wa habari na watalii wengi wa nchi za nje walikuja mjini Beijing wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, hivyo lugha ni moja ya suala muhimu lililotakiwa kutatuliwa. Kwa hiyo kamati ya maandalizi ya Olimpiki ya Beijing iliwaajiri watu wengi wanaojitolea, ambao wanatoa huduma ya ukalimani, na Bibi Panthipa Asavatheputhai ndiye mmoja kati yao. Alisema aliona fahari kwa kuwa mtu wa kujitolea wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing, na alithamini sana fursa hiyo.

Watu waliojitolea kwenye Michezo ya Olimpiki ya Beijing wengi ni wanafunzi wa vyuo vikuu, vilevile kuna baadhi ya watu wanaojitolea wa nchi za nje na Wachina wanaoishi nchi za nje. Bibi Wang Fang aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Bath cha Uingereza ni msaidizi wa kiongozi wa ujumbe wa Uingereza. Wakati wa Michezo ya Olimpiki, Bibi Wang Fang alikuwa na shughuli nyingi. Kila siku alipaswa kuwapokea maofisa wengi na kuhojiwa na vyombo vingi vya habari. Lakini hakuona uchovu. Alisema katika siku hizi, ama kufanya kazi pamoja na ujumbe wa Uingereza au kuongea na watu wanaojitolea wa nchi za nje, aliona fahari kwa kuwa Mchina. Akisema,

"Baada ya sherehe ya ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki, nilimuuliza kiongozi wa ujumbe wa Uingereza kuwa aonaje kuhusu sherehe hiyo, alisema sherehe ya ufunguzi huo ni nzuri zaidi kuliko nyingine, nilifurahi sana niliposikia hayo. Kiongozi huyo pia alisifu sana kijiji cha Olimpiki mjini Beijing, China, alisema aliwahi kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya awamu 12, na kijiji hiki ni kizuri zaidi cha Michezo ya Olimpiki. Kweli naona fahari nikiwa Mchina."

Licha ya watu wanaojitolea kwenye mashindano, Michezo ya Olimpiki ya Beijing pia ilikuwa na watu wengi waliotoa huduma mjini kwa kujitolea. Walifanya kazi katika barabara na viwanja vya mjini, ambao walitoa huduma za habari na kushughulikia mambo ya dharura kwa watu waliohusika na Michezo ya Olimpiki ya Beijing, watalii wa nchi za nje na wakazi mjini Beijing.

Mbele ya mlango wa bustani ya michezo ya Shijingshan kulikuwa na kituo cha utoaji huduma. Watu waliotoa huduma za kujitolea hapo wote walikuwa wanafunzi wa vyuo vikuu, walitoa misaada kwa watalii kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 alasiri. Walisema waliona fahari kwa kuweza kushiriki kwenye kazi ya utoaji huduma kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing.

Katika kikundi kikubwa cha watu wa kujitolea, licha ya wanafunzi wa vyuo vikuu, pia kilikuwepo watu wa sekta mbalimbali, ambao walitaka kufanya kadiri wawezavyo kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki. Katika uwanja wa michezo wa taifa "Kiota", alikuwa mtu maalum wa kujitolea, yeye ndiye bingwa wa zamani wa Wushu wa China Bibi Wu Min. Aliwahi kupata ubingwa wa Wushu wa China kwa mara nyingi. Mwaka 1996, Bibi Wu Min alikwenda Ujerumani, na kuwa kocha wa Wushu katika klabu moja mjini Berlin. Bibi Wu Min alisema, safari hii alifuatana na ujumbe wa Ujerumani kuja hapa Beijing, licha ya kutazama maonesho ya Wushu, pia ana matumani kuwa anaweza kutoa huduma kwa taifa lake, hivyo yeye na mume wake, waliomba kuwa watu wa kujitolea katika uwanja wa michezo wa taifa, na kutoa huduma ya ukalimani.

Bibi Wu Min alisema, ingawa kazi za watu wanaojitolea ni nyingi, lakini aliona wakazi wa Beijing waliwaelewa na kuwafuatilia. Alisema,

"Kwa kuwa niliishi katika nchi za nje kwa muda mrefu, hivyo sikuzoea baada ya kurudi nchini China. Tuliamka mapema, saa kumi na nusu asubuhi, hivyo baada ya siku mbili niliumwa. Mwanzoni tulikuja kwa ajili ya kutoa huduma kwa wengine, lakini baada ya mimi kuumwa, watu wengi zaidi walitoa huduma kwetu, walituletea dawa na kutupelekea hospitalini. Huduma zilizotolewa kwa sisi watu wa kujitolea pia ni kwa makini sana."

Mbali na vijana, vilevile kuna wazee wengi walioshiriki katika utoaji huduma kwa Michezo ya Olimpiki. Mzee Chang Zhifu mwenye umri wa miaka 66 alisema, baada ya Beijing kufanikiwa kushinda nafasi ya kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki, alitaka kushiriki kwenye utoaji huduma kwa michezo hiyo. Hivyo licha ya kutoa huduma, pia alijifunza Kiingereza na ishara ya mikono.

Idhaa ya kiswahili 2008-09-24