Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-24 20:58:26    
Mapishi ya mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe yenye ladha ya pilipili hoho

cri

Mahitaji:

mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe gramu 200, chumvi vijiko viwili, chembechembe za pilipili manga kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, sosi ya chaza vijiko viwili, vipande vya vitunguu maji, pilipili hoho gramu 10, vitunguu saumu na tangawizi

Njia:

1. Osha mbavu za nyama ya nguruwe, kasha changanyakoroga pamoja na chumvi, chembechembe za pilipili manga,sukari, mchuzi wa sosi, sosi ya chaza, na vipande vya vitunguu maji na tangawizi.

2. washa moto , mimina mafuta kwenye sufuria, halafu tia mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe zikaange, mpaka ziwe hudhurungi, zipakue.

3. baadaye, tia pilipili manga na pilipili hoho, halafu tia vitunguu saumu, korogakoroga halafu tia mifupa yenye nyama ya mbavuni mwa nguruwe, korogakoroga, tia karanga korogakoroga zipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.