Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-25 19:47:39    
Kujiuzulu kwa Thabo Mbeki kumesababisha mtafaruku wa kisiasa nchini Afrika Kusini

cri

Tarehe 25 bunge la Afrika Kusini litafanya mkutano na kupitisha ombi la rais Thabo Mbeki kujiuzulu, na pia kupitisha maombi ya kujiuzulu kwa makamu wa rais Phumzile Mlambo-Ngcuka na mawaziri 11 pamoja na manaibu mawaziri wanne. Kujiuzulu kwa Thabo Mbeki na mawaziri walio karibu nusu kumesababisha mtafaruku wa kisiasa nchini Afrika Kusini, hata hivyo mwenyekiti wa chama tawala ANC Bw. Jacob Zuma alisema chama chake kimejiandaa kwa kazi zote baada ya rais Thabo Mbeki kuondoka madarakani na watu wa fani zote wasiwe na wasiwasi.

Tarehe 21 jioni Rais wa Afrika Kusini Bw. Thabo Mbeki alitangaza uamuzi wake wa kujiuzulu kupitia televisheni na alikabidhi ombi hilo kwa bunge. Alisema, yeye pamoja na serikali yake hakuingilia kati ukaguzi wa kisheria wala hakuingilia kati mashitaka ya ufisadi ya mahakama ya taifa dhidi ya mwenyekiti wa chama tawala ANC Bw. Jacob Zuma. Baada ya Rais Thabo Mbeki kujiuzulu, makamu wa rais Bw. Phumzile Mlambo-Ngcuka tarehe 23 alitangaza kuwa atajiuzulu pamoja na Mbeki. Mawaziri 11 na manaibu mawaziri wanne pia walitoa maombi yao ya kujiuzulu, kati yao alikukwepo waziri wa fedha aliyeheshimika sana, waziri wa ulinzi na mawaziri wa serikali za mitaa.

Kabla ya rais Mbeki kujiuzulu, katibu mkuu wa chama cha ANC Bw. Gwede Mantashe katika mkutano na waandishi wa habari alisema, kwa sababu Bw. Mbeki kutuhumiwa kujihusisha na kesi ya ufisadi wa Jocob Zuma, baada ya majadiliano ya Kamati ya utendaji, chama hicho kimeamua kumtaka Mbeki ajiuluzu kabla ya kipindi chake cha urais kumalizika, na uamuzi huo umewasilishwa bungeni. Bw. Gwede Mantashe alisisitiza kuwa kumtaka Mbeki ajiuzulu sio adhabu kwake binafsi bali ni kwa ajili ya kuondoa hitilafu ndani ya chama na kuimarisha umoja wa chama. Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na kazi muhimu aliyofanya Bw. Mbeki katika kesi ya uhalifu wa Zuma, malalamiko dhidi yake yanazidi kuwa makali ndani ya chama na kusababisha chama hicho kufanya uamuzi wa kumtaka Mbeki ajiuzulu.

Ukweli wa mambo ni kwamba tokea mwaka 2005 Bw. Zuma aliyekuwa makamu wa rais wa Afrika Kusini alipofukuzwa madarakani na Thacob Mbeki, chama cha ANC kimetokea mpasuko. Mwaka jana baada ya Jacob Zuma kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho mpasuko huo umekuwa mkubwa zaidi na zaidi. Baada ya tarehe 12 mahakama kuu ilipokana kesi dhidi ya Jacob Zuma na kuondoa vikwazo vyake vya kugombea uchaguzi wa urais utakaofanyika mwaka kesho, mgongano ndani ya chama unazidi kuwa wazi.

Kujiuzulu kwa Thabo Mbeki kumesababisha msukosuko wa kisiasa nchini Afrika Kusini. Katika siku ambayo waziri wa fedha alipotangaza kujiuzulu, thamani ya fedha nchini Afrika Kusini mara ilishuka kwa kiasi kikubwa na kusababisha msukosuko wa soko la fedha. Vyama vya upinzani vinaulaumu uamuzi wa chama cha ANC wa kumtaka Mbeki ajiuzulu. Wanasiasa wanafafanua kwamba uamuzi huo umezamisha Afrika Kusini katika hali ya wasiwasi wa kisiasa, na vina matumaini kwamba maamuzi yoyote ya baadaye yaakayofanywa na kamati ya utendaji ya chama cha African National Congress yapaswa kufuata utaratibu wa kisheria ili yasilete ghasia nchini.

Chama cha ANC tarehe 22 kilipendekeza naibu mwenyekiti wa chama hicho Bw. Kgalema Motlanthe awe rais mpya na tarehe 25 atashika rasmi wadhifa huo baada ya kukubaliwa na bunge. Muda wa urais wake utamalizika mwezi Aprili mwaka kesho kabla ya uchaguzi mkuu mpya kufanyika.