Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-09-26 15:47:18    
China kuinua kiwango cha misaada kwa nje

cri

Ili kuzisaidia nchi zinazopokea misaada kuongeza uwezo wa kujiendeleza, China siku zote inatilia maanani kazi ya kuzisaidia nchi hizo kuwaandaa watu wenye ujuzi. Mpaka sasa maofisa, wasimamizi na mafundi laki moja wamekuja China kushiriki kwenye semina mbalimbali. Hasa katika miaka kadhaa iliyopita, China iliandaa mara nyingi semina na kongamano kwa ajili ya nchi za Afrika, ili nchi za Afrika ziweze kujifunza na kuigiza uzoefu wa maendeleo ya China.

Mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa kazi ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya kiuchumi wajiendeleze cha baraza la serikali la China Bw. Fan Xiaojian alisema, China inapenda kutoa misaada kwa pande nyingi ili kuisaidia Afrika katika kupunguza umaskini. Alisema China inapenda kufanya mawasiliano na nchi za Afrika kuhusu uzoefu wa China katika kupunguza umaskini na kujiendeleza mambo ya jamii, vilevile inapenda kuendelea kuziunga mkono katika kuendeleza nguvu kazi, na kutoa misaada ya teknolojia kwenye sekta husika.

Mkurugenzi wa ofisi ya utoaji wa misaada kwa nje ya wizara ya biashara ya China Bw. Wang Shichun alisema, utoaji wa misaada kwa nje umehimiza maendeleo ya uchumi wa nchi zinazopekea misaada, vilevile umeimarisha uhusiano kati ya China na nchi zinazoendelea. Alisema China itaendelea kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea,na kuinua zaidi kiwango cha kazi ya kutoa misaada kwa nchi za nje. Bw. Wang Shichun alisema katika siku zijazo China itazingatia zaidi mahitaji ya kimsingi ya watu wa nchi zinazopokea misaada, na kutoa misaada zaidi katika miradi inayowanufaisha raia, kama vile kujenga hospitali na shule, kujenga miundo mbinu, kuendeleza uchumi wa vijiji, kukinga na kutibu magonjwa, na kuwaandaa watu wenye ujuzi.