Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-05 20:21:29    
Makampuni ya China yaliyopo nchi za nje yapaswa kushukuru jamii za huko

cri

Mkuu wa shirikisho la biashara ya mradi wa ukandarasi kwa nchi za nje la China Bw. Diao Chunhe hivi karibuni huko Algiers alisema shughuli za miradi ya ukandarasi za China kwa nchi za nje ziliendelea kwa kasi lakini makampuni ya China yalipoendelea kwenye nchi za nje yanapaswa kushukuru jamii za huko ili kujiendeleza na kupata manufaa pamoja na wananchi wa huko.

Bw. Diao Chunhe alisema, mradi wa ukandarasi kwa nchi za nje ni sehemu muhimu ya mkakati wa kujiendeleza kwa makampuni ya China, makampuni ya China yamepata maarifa mengi katika ushirikiano kati yao na nchi mbalimbali na yameongeza uwezo wao.

Bw. Diao Chunhe alisema, nchi zinazoendelea ni soko muhimu la miradi ya ukandarasi ya China kwa nchi za nje, nchi hizo zinahitaji kujenga miundo mbinu hivyo makampuni ya China yalipata fursa nzuri ya kujiendeleza. Alisisitiza kuwa makampuni ya China yanapaswa kuwa na moyo mzuri na kutilia maanani kutekeleza jukumu la jamii baada ya kupata maslahi ya uchumi, na pia yanapaswa kuimarisha kujiwekea nidhamu kwenye shughuli zao ili kuepusha hali ya mashindano mabaya kati ya makampuni ya China.

Waziri wa nymba wa Algeria na mwenyekiti wa shirikisho la viwanda na biashara la Algeria walipokutana na ujumbe wa wafanyabiashara wa China akiwemo Bw. Diao Chunhe wakisifu sana kuanzisha shughuli za biashara kwa makampuni ya China nchini Algeria na wanataka kuimarisha ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya nchi hizo mbili.

Habari nyingine zilisema, waziri mkuu wa Algeria Bw. Ahmed Ouyahya hivi karibuni huko Algiers alipokutana na ujumbe wa uchumi na biashara wa China ulioongvozwa na naibu waziri wa bishara wa China Bw. Chen Jian, alisifu sana uhusiano kati ya Algeria na China na alitaka kuimarisha uhusiano wa kimkakati na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Bw. Ouyahya alifurahia ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na alitaka ushirikiano wa biashara na uchumi uendelezwe kwa kiwango cha juu. Aliyataka makampuni ya China yaliyoanzisha shughuli za biashara nchini Algeria yaimarishe ushirikiano na mawasiliano na makampuni ya Algeria.

Sherehe ya kusaini makubaliano ya mradi wa tathimini kuhusu uwezekano wa kujenga reli kutoka Takladi hadi Kumasi nchini Ghana kwa msaada wa China ilifanyika hivi karibuni kwenye wizara ya bandari na reli ya Ghana, balozi wa China nchini Ghana Bw. Yu Wenzhe na waziri wa bandari na reli wa Ghana Bw. Ameyaw Akumfi walisaini makubaliano ya kukabidhi mradi huo kwa niaba ya serikali yao.

Mradi wa tathimini kuhusu uwezekano wa kujenga reli ya Ghana kwa msaada wa China ulishughulikiwa na kampuni ya taasisi ya kwanza ya utafiti na usanifu ya reli ya China na ulianza kutoka mwezi Julai mwaka 2007, kampuni hiyo ilifanya utafiti kwenye sehemu hiyo na kumaliza ripoti husika.

Bw. Yu Wenzhe alisema, mradi wa tathimini kuhusu uwezekano wa kujenga reli ya Ghana umekabidhiwa kwa Ghana na umetoa data halisi kuhusu ujenzi wa reli ya Ghana ambao utasaidia mipango na ujenzi wa reli ya Ghana katika siku za baadaye. Alisifu sana ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Ghana katika sekta mbalimbali na alisema China inapenda kuendelea kutoa misaada kwa Ghana kadiri iwezekanavyo.

Bw. Ameyaw Akumfi aliishukuru sana serikali ya China kwa kusaidia Ghana kutekeleza mradi huo, na kuisifu ripoti iliyotolewa na China ambayo ni ya hali halisi na kutoa tegemeo muhimu kwa ujenzi wa reli ya Ghana, na kutaka Ghana na China zizidishe ushirikiano katika sekta ya ujenzi wa reli.

Habari nyingine zilisema, kituo cha utamaduni wa China nchini Benin kilifanya sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya kituo hicho kwenye jumba la mkutano wa Cotonou.

Sherehe hiyo iliendeshwa na mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha China Bw. Liu Hongge. Balozi wa China nchini Benin Bw. Geng Wenbing alitoa hotuba akikumbusha mchakato wa kuanzishwa kwa kituo hicho. Alidhihirisha kuwa: "Leo sisi si kama tu tunasherehekea miaka 20 ya kuanzishwa kwa kituo hicho, bali pia tunasherehekea mafanikio yaliyopatikana kwenye kituo hicho katika miaka 20 iliyopita. Hayo ni mafanikio mazuri ya mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Benin na pia yalionesha maelewano kati ya nchi hizo mbili na urafiki mkubwa kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Waziri wa utamaduni, viwanda vya utalii wa Benin Bw. Tolaiba Sumanu alisifu sana umuhimu wa kituo cha utamaduni cha China katika kuhimiza na kuendeleza sekta ya utamaduni wa Benin. Alisema serikali ya Benin inataka kituo cha utamaduni cha China kizidi kukua na kuendelea na kuongeza harakati za aina mbalimbali. Alisema wizara ya utamaduni wa Benin daima itauunga mkono shughuli zote za kusaidia za kituo cha utamaduni cha China.

Kituo cha utamaduni cha China nchini Benin kilianzishwa rasmi tarehe 27 mwezi Spetemba mwaka 1988 kutokana na uungaji mkono wa wizara ya utamaduni ya China na serikali ya Benin, ni kituo cha kwanza cha utamaduni kilichoanzishwa na serikali ya China barani Afrika.

Habari nyingine zinasema, balozi wa China nchini Kenya Bw. Zhang Ming tarehe 26 kwa niaba ya serikali ya China alikabidhi misaada ya kibinadamu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 3 zikiwemo fedha na vifaa, ili kusaidia ukarabati wa uchumi na kupanga wananchi baada ya kutokea msukosuko nchini Kenya. Balozi Zhang Ming na kaimu wa waziri wa fedha wa Kenya Bw. John Michuji kwa niaba ya serikali zao walisaini makubaliano husika. Bw. Zhang Ming alisema msukosuko wa uchaguzi wa urais uliotokea mwanzoni mwa mwaka huu nchini Kenya umesababisha wananchi wengi kupoteza makazi yao, serikali ya China na wananchi wa China wanapenda kutoa misaada ya kibinadamu kadiri iwezekanavyo. Alisema China na Kenya zina uhusiano na ushirikiano nzuri katika sekta mbalimbali, kwa ajili ya kuongeza uungaji mkono kwa serikali ya Kenya, serikali ya China iliamua kutoa misaada tena kwa Kenya. Bw. Michuji aliishukuru sana misaada ya China na alisifu sana misaada hiyo ambayo itaimarisha urafiki kati ya China na Kenya.