Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-05 18:29:30    
Wanasayansi wanawake wa China watarajia kutoa michango mikubwa zaidi

cri

Kutokana na maendeleo ya jamii, wanawake wengi zaidi wanafanya kazi za utafiti wa sayansi na teknolojia duniani. Nchini China theluthi moja ya watafiti wa sayansi na teknolojia ni wanawake, hata mkutano wa mwaka wa shirikisho la sayansi na teknolojia la China uliofanyika hivi karibuni ulianzisha baraza la ngazi ya juu la wanasayansi wanawake kujadili kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake na utafiti wa sayansi na teknolojia.

Bi. Mao Jianying ni profesa wa chuo kikuu cha usafiri wa ndege na safari ya anga ya juu cha Beijing, baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Beijing na chuo kikuu cha usafiri wa ndege na safari ya anga ya juu cha Beijing katika miaka ya 60 ya karne iliyopita, Bi. Mao Jianjing alianza kujitolea kwenye kazi za tafiti za teknolojia za kijeshi, mwaka 1985 alikuwa mmoja katika kundi la kwanza la madaktari tangu China mpya ianzishwe. Akiwa mtu aliyeshuhudia maendeleo ya wanawake katika shughuli za tafiti za sayansi na teknolojia nchini China, Bi. Mao Jianying alisema:

"idadi ya watafiti wanawake walioandaliwa baada ya China kujipatia uhuru ilizidi sana ile ya walioandaliwa kabla ya hapo, na hadhi yao ya kijamii pia iliinuka zaidi kuliko wale waliandaliwa kabla ya hapo. Hasa baada ya China kuanza kufanya mgeuzi, watafiti wanawake wa China wameongezeka zaidi."

Kuanzia mwaka 1984 hadi sasa, Bi. Mao Jianying amefanya miradi mikubwa 20 ya tafiti za sayansi ya China, na alitoa makala 150 ya utafiti kwenye magezeti muhimu ya sayansi ya China na ya nje, makala 60 kati yao yamechukuliwa kwenye majarida muhimu ya kitaaluma duniani. Bw. Mao Jianjing pia alikwenda Uingereza na Marekani mara 15 kutoa mihadhara.

Bi. Mao Jianying alisema, wanawake wanafanya juhudi na bidii kubwa zaidi kuliko wanaume wakitaka kupata mafanikio katika utafiti wa sayansi na teknolojia. Bw. Mao Jianjing aliwahi kuacha fursa ya kutunukiwa shahada ya udaktari na chuo cha uhandisi cha kifalme cha Uingereza kwa sababu ya kuitunza familia yake. Lakini mafanikio yake yamethibitisha kuwa, wanawake pia wanaweza kufanya kazi hodari katika utafiti wa teknolojia ya juu kama vile katika eneo la safari ya anga ya juu. Bi. Mao Jianying alisema:

"kutokana na uzoefu wangu, ingawa kazi za utafiti wa teknolojia za safari ya anga ya juu ni kazi kubwa za kutumia akili nyingi, lakini wanawake ni sawasawa na wanaume, pia wanaweza kufanya vizuri kazi za utafiti wa sayansi."

Tangu China mpya ilipoanzishwa mwaka 1994, wanasayansi wengi wanawake wengi hodari kama Bi. Mao Jianying walijitokeza. Kwa mujibu wa takwimu husika, hivi sasa China ina watafiti wanawake zaidi ya milioni 10, ambao wanachukua asilimia 37 ya idadi ya watafiti wote wa China. taasisi ya sayansi na ya uhandisi ya China ambazo zinawakilisha kiwango cha juu cha utafiti wa sayansi na teknolojia nchini China zina wanachama 70 wanawake. idadi ya watafiti wanawaka wa ngazi ya juu nchini China hata imezidi ile ya nchi zilizoendelea, zikiwemo Marekani, Ufaransa na Ujerumani. Naibu mwenyekiti wa zamani wa shirikisho la sayansi na teknolojia la China Bi. Liu Shu aliwahi kutoa ripoti kuhusu watafiti wanawake wa China, alisema, kundi hilo hivi sasa limeonesha mustakabali mzuri wa maendeleo. Bi. Liu Shu alisema:

"watafiti wanawake wengi wa China wana umri mdogo, wengi wao wana umri chini ya miaka 50, wanafunzi wa kike wanaosoma shahada la pili katika vyuo vikuu vya China pia wanaongezeka kwa kasi, hali hiyo imethibitisha kuwa wanawake wengi zaidi wana hamu ya kushiriki kwenye tafiti za sayansi."

Kuongezeka kwa watafiti wanawake hakuondokani na bidii na juhudi zao wenyewe, wala hakuondokani na maendeleo ya jamii ya China na kuinuka kwa hadhi ya wanawake nchini China. wanawake na wanaume wana haki sawasawa za kupewa elimu ya msingi hadi elimu ya juu, hali hiyo imeweka msingi imara kwa wanawake kushiriki kwenye tafiti za sayansi. Mkuu wa chuo kikuu cha kilimo cha Henan Bi. Wang Yanling alisema:

"katika miaka ya hivi karibuni idadi ya wanafunzi wa kile wanaosoma shahada ya kwanza na shahada ya pili katika vyuo vikuu vya China imeongezeka kwa kasi sana ambayo haijawahi kutokea zamani. Hivi sasa wanafunzi wa kike wanachukua asilimia 47.08 katika wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini China, wanafunzi wa kile wanaosoma shahada ya pili wanachukua asilimia 6 na wanaosoma shahada ya udaktari wanachukua asilimia 32.57."

Lakini matatizo mbalimbali pia yanazuia maendeleo ya wanawake katika njia zake za tafiti za sayansi. Hali ya kutokuwepo watafiti wanawake katika ngazi ya juu ya eneo lao ni tatizo linalosumbua kote duniani. Nchini China kutokana na athari za utamaduni wa jadi, wanawake wanabeba wajibu mkubwa zaidi wa kuitunza familia, hivyo wanakabiliana na shinikizo za njia mbili kutokana na kazi na za familia. Naibu mwenyekti wa zamani wa shirikisho la sayansi na teknolojia la China Bi. Liu Shu alisema,

"nchi yetu inapoweka sera husika inapaswa kuzingatia mahitaji ya wanawake wa uzazi na kuwatunza watoto, wanapaswa kuzingatiwa zaidi, jumuiya za kijamii, familia, idara za utafiti na shule zote zinapaswa kuwaelewa na kuwaunga mkono."

Kuhusu maendeleo ya wanasayansi wanawake wa China katika siku za baadaye, Bi. Liu Shu alieleza imani yake akisema:

"maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia yametoa fursa kwa wanawake kushiriki kwenye kazi za tafiti za sayansi. Watafiti wanawake wa sasa wamefanya kazi hodari katika maeneo yao, hii imeonesha mustakabali mkubwa wa wanawake katika eneo hilo."