Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-06 16:39:02    
Maendeleo ya utamaduni wa jadi mkoani Tibet

cri
Mkoa unaojiendesha wa Tibet ni sehemu yenye utamaduni mkubwa wa jadi watu wa makabila madogo madogo wanayoishi. Miaka 50 iliyopita wakati wa Tibet ilipotekeleza mfumo wa wakuilma watumwa na utawala wa kisiasa pamoja na kidini, utamaduni wa kidini ulikuwa unatiliwa mkazo, na utamaduni wa jadi hautiliwa maanani, hata baadhi yao ulitoweka. Tangu mwishoni mwa miaka ya 50 ya karne iliyopita, serikali ya China iliongeza nguvu ya kuhifadhi utamaduni wa jadi mkoani Tibet, na kupata mafanikio mazuri.

Tangu mwishoni mwa miaka 50 ya karne 20, hasa katika miaka 20 iliyopita, serikali ya China iliongeza kutenga fedha kwa ajili ya kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa jadi mkoani Tibet. Naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti wa makabila ya taasisi ya sayansi ya jamii ya mkoa wa Tibet Bw. Tsering Jabu alisema,

"Nchi yetu inatilia maanani sana mabaki ya utamaduni wa jadi mkoani Tibet, iliweka shairi maarufu la historia ya kabila la Watibet 'Utenzi wa Mfalme Gesar' kuwa ni mradi muhimu wa utafiti wa taasisi kuu ya sayansi ya jamaa ya China."

Katika mwanzoni mwa miaka 90 ya karne iliyopita, chini ya uungaji mkono na msaada wa serikali, idara ya utamaduni na uchapishaji ya mkoa wa Tibet ilikamilisha kutunga vitabu vitatu vyenye maneno milioni 3.84 kuhusu hadithi, nyimbo na methali za jadi za kabila la Watibet baada ya kufanya juhudu kubwa za miaka mitatu. Mwenyekiti wa Shirikisho la Waandishi na Wasanii wa Jadi Mkoani Tibet Bw. Tseten Dorje alisema,

"Vitabu hivyo haivikutokea katika historia ya Tibet. Ili kumaliza kazi ya kutunga vitatu hivyo vitatu, China ilitenga yuan za renminbi kati ya milioni moja na mbili."

Bw. Tseten Dorje alisema licha ya watalaamu wa kabila la Watibet na Wahan mkoani Tibet, watalaamu wa Beijing pia walishiriki kwenye kazi za kutunga vitabu hivyo vitatu. Alisema mradi mkubwa wa utamaduni haukuweza kukamilika kabla ya ukombozi wa Tibet, wakati huo kutokana na mfumo wa wakuilma watumwa, utamaduni wa jadi haukuhifadhiwa, na wasanii wa utamaduni wa jadi mkoani Tibet pia walidharauliwa sana, na hawakuwa na heshima, alisema,

"Wakati mfumo wa wakulima watumwa ulipotekelezwa, hadhi ya wasanii wa utamaduni wa jadi ilikuwa chini sana, hawakupewa heshima wala uhuru, na waliendesha maisha kwa kufanya maonesho fichaficha."

Lakini sasa hali imebadilika. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 50 ya karne iliyopita, serikali ya China ilitilia maanani sana utamaduni wa jadi, na utamaduni huo mkoani Tibet ulipewa heshima kubwa, ambapo hadhi ya wasanii wa jadi pia ilipanda juu. Bw. Tseten Dorje alijulisha kuwa sasa baadhi ya wasanii hao waliteuliwa kuwa wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa, na maisha ya wasanii wengine pia yameboreshwa sana.

Akiwa mwenyekiti wa Shirikisho la Waandishi na Wasanii wa Jadi Mkoani Tibet, Bw. Tseten Dorje alieleza kuwa shirikisho hilo linashughulikia kukusanya, kutafuta, kuokoa, kurekebisha, kuhifadhi na kutafiti fasihi na sanaa za jadi, na lina wanachama zaidi ya 200 wanaojishughulisha na kazi za kuhifadhi utamaduni wa jadi mkoani Tibet.

Bw. Tseten Dorje alisema katika miaka kadhaa iliyopita, chini ya uungaji mkono na misaada ya serikali kuu ya China, Shirikisho la Waandishi na Wasanii wa Jadi Mkoani Tibet limefanya kazi nyingi katika kuhifadhi utamaduni wa jadi wa kabila la Watibet, hali hii ni ushahidi mzuri zaidi wa kutibitisha maneno ya Dalai Lama kuwa utamaduni wa Tibet umeteketea kabisa ni uwogo mtupu. Alisema,

"Zamani hatukuweza kutarajia maendeleo ya sasa ya utamaduni wa jadi wa Tibet. Kundi la Dalai na wafarakanishaji wanasema utamaduni wa Tibet umeteketea kabisa, maneno hayo ni uwongo mtupu, na ni kwa ajili ya kupaka matope kwa nchi yetu. Tunakasirika sana kuona vitendo hivyo. Wafarakanishaji hao hawajui maendeleo ya utamaduni wa Tibeti, lakini sisi tunaofanya kazi za kuhifadhi utamaduni huo tunajua sana kuwa juhudi za kuhifadhi na kuendeleza utamaduni wa Tibet zimepata mafanikio makubwa."

Imefahamika kuwa sasa Shirikisho la Waandishi na Wasanii wa Jadi Mkoani Tibet linashughulikia kazi ya kuhariri vitabu viwili vya Hadithi za Wilaya Mbalimbali Mkoani Tibet na Picha za Tangka za Tibet. Bw. Tseten Dorje alisema utamaduni wa Tibet ni mkubwa sana, na China inatilia maanani kazi za kuhifadhi utamaduni huo, baada ya kukamilisha vitabu hivyo viwili, shirikisho hilo litaendelea na kazi ya kutunga kitabu cha Majengo ya Tibet.

Mtalaamu wa kabila la Watibet anayeshughulikia kazi za kuhifadhi mabaki yasiyoonekana ya utamaduni mkoani Tibet Bw. Phuntsok Namgyai alijulisha kuwa, kutokana na serikali kuu ya China kuongeza nguvu katika kuhifadhi utamaduni wa Tibet siku hadi siku, utamaduni na sanaa za Tibet zimepata maendeleo makubwa, alisema,

"Katika miaka 50 iliyopita, serikali kuu ya China imetenga mali na hali kubwa katika uhifadhi wa utamaduni wa Tibet, na inaokoa, kurithisha na kuhifadhi vizuri utamaduni huo kwa njia za kisheria, kiuchumi na kisiasa, na utamaduni na sanaa za jadi za Tibet zikiwemo mafunzo ya lugha ya kitibet, muziki na ngoma za jadi ya Tibet, na hadithi za jadi zimepata maendeleo makubwa. Sasa utamaduni wa Tibet unastawi chini ya juhudi kubwa za pande mbalimbali, na ni lulu linalong'aa kati ya utamaduni wa China na wa kimataifa."

Idhaa ya kiswahili 2008-10-06