Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2008-10-07 17:13:03    
Kampuni ya Taishan yapata mafanikio kwa kutumia fursa ya Michezo ya Olimpiki ya Beijing

cri

Bidhaa zinazotengenezwa na China zinatambuliwa na dunia nzima, lakini inua sifa na umaarufu wa bidhaa zinazotengenezwa na China bado ni kazi kubwa ya makampuni mengi ya China. Michezo ya Olijmpiki ya Beijing imeleta fursa ya kuongeza umaarufu wa bidhaa za China na kuzisaidia bidhaa hizo kuingia kwenye soko la kimataifa.

Kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing, makampuni ya China yaliweka rekodi nyingi mpya, kwa mfano kampuni kubwa zaidi inayotengeneza vifaa vya michezo kwa michezo ya Olimpiki, kampuni ya kwanza inayotengeneza vifaa vya masomo kwa michezo ya Olimpiki na kampuni ya kwanza inayotengeneza vifaa vya viyoyozi kwa michezo ya Olimpiki. Makampuni mengi ya China yameonesha bidhaa zao kwa dunia nzima kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing.

Kampuni ya vifaa vya michezo vya Taishan ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya vifaa vya michezo nchini China, ikichukua fursa ya michezo ya Olimpiki ya Beijing, imekuwa kampuni kubwa zaidi iliyotengeneza vifaa vya michezo kwa ajili ya michezo ya Olimpiki kwenye historia. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Pian Zhiliang alisema bidhaa za kampuni yake zimebadilisha historia ya vifaa vya michezo ya Olimpiki kutengenezwa na nchi za nje katika miaka zaidi ya 100 iliyopita, akisema,

"Baada kampuni yetu kusaini mkataba na kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing mwezi Mei mwaka 2007, ilitengeneza vifaa vya aina zaidi ya mia kadhaa kwa michezo ya aina 6 ikiwemo jimnastiki, judo, taekwondo, mieleka, ndondi na riadha. Aidha miongoni mwa medali 302 za dhahabu zilizotolewa kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing, 122 zilitengenezwa na kampuni yetu. Kampuni yetu imetengeneza vifaa vya michezo vyenye usalama zaidi, na kuhakikisha wachezaji wapate mafanikio makubwa zaidi."

Mwaka 2004 kampuni ya Taishan ikishirikiana na kampuni ya J&F ya Uholanzi na kutumia chapa zao ilitengeneza vifaa vya michezo kwa michezo ya Olimpiki ya Athens. Mwaka 2007 kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki iliteua kampuni hiyo kutengeneza vifaa kwa michezo ya aina 6 kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing. Naibu meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Dong Huaduan alipozungumzia uzoefu wa kampuni yao wa kupata mafanikio alisema,

"Kuna sababu mbili muhimu. Kwanza teknolojia zetu za kutengenza vifaa vya michezo ni za kisasa zaidi duniani. Kwa mfano vigezo vyetu vya kutengeneza vifaa vinavyotumiwa kwenye mchezo wa kuruka juu kwa upondo vimekuwa juu zaidi kuliko vigezo vya kimataifa, na vigezo hivyo vimetambuliwa na dunia. Aidha, kampuni yetu imetengeneza vifaa vya michezo kwa miaka zaidi ya 30, ina uzoefu mkubwa wa kutoa huduma wakati wa mashindano. Kutokana na sababu hizo mbili, tuliteuliwa na kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya Beijing."

Bw. Dong Huaduan alisema kutokana na michezo ya Olimpiki ya Beijing, kampuni ya Taishan imekuwa chapa maarufu duniani, uwezo na imani ya ya kampuni hiyo imeinuliwa kwa kiasi kikubwa, akisema,

"Zamani makampuni maarufu ya nchi za nje tu yaliweza kutengeneza vifaa vya michezo kwa michezo ya Olimpiki, leo kampuni yetu imefanyikiwa kufanya hivyo, na imefanya vizuri zaidi. Baada ya kupata kibali cha kutengeneza vifaa vya michezo kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing, orodha za kuagiza bidhaa na makampuni yanayotaka kushirikiana na kampuni yetu yameongezeka. Katika mwaka huu ambao uchumi wa dunia unaendelea pole pole, uuzaji wa bidhaa zetu katika nchi za nje uliongezeka kwa mara mbili. Kwa mfano, blangeti za mchezo wa judo zilizotengenezwa na kampuni yetu zimechukua asilimia 70 ya blangeti zinazoagizwa na Marekani, na hivi sasa kiasi hicho bado kinaongezeka."

Michezo mikubwa duniani inaweza kuyasaidia makampuni kuanzisha chapa maarufu duniani. Adidas iliyokuwa chapa maarufu tangu mwaka 1972, Nike iliyokuwa chapa maarufu tangu mwaka 1984 na Sangsung iliyokuwa chapa maarufu tangu mwaka 1988 zote zimethibitisha jambo hilo. Bw. Dong Huaduan alipozungumzia mikakati ya maendeleo ya kampuni ya Taishan, alisema kuendelea kuinua sifa ya chapa ya Taishan ni lengo litakaloshikiliwa na kampuni hiyo, akisema,

"Kazi zinazofuata ni kueneza chapa yetu duniani. Kwa mfano tutaeneza chapa zetu kwenye michezo ya Olimpiki ya London, na michezo mbalimbali ya kimataifa duniani. Baadaye tutakapoinua sifa ya chapa yetu, tutahimiza maendeleo ya teknolojia ya kutengeneza vifaa vya michezo duniani."

Shughuli za kutengeneza vifaa vya michezo ni shughuli za jadi za nchi zilizoendelea za magharibi zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Marekani. Kuna makampuni mengi maarufu katika nchi hizo. Lakini Bw. Dong Huaduan akionesha imani kubwa alisema kuwa, kampuni yako itafanya juhudi ili kutengeneza vifaa kwa michezo ya aina 10 kwenye michezo ya Olimpiki ya London. Kampuni hiyo haitapotea fursa hiyo ya kibiashara, akisema,

"Tuna nia thabiti ya kupata fursa hiyo. Nchi zote zina matumaini ya kuandaa michezo mizuri ya Olimpiki. Vifaa vya michezo ni muhimu kwa maandalizi ya michezo ya Olimpiki, hivyo sifa vifaa vya michezo ni muhimu zaidi. Kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing, tumethibitisha uwezo wetu wa kutengeneza vifaa vizuri zaidi duniani. Tena tuna kikundi hodari cha huduma, hatukufanya kosa lolote kwenye michezo ya Olimpiki ya Beijing. Tunafikiri kamati ya maandalizi ya michezo ya Olimpiki ya London itatambua kazi yetu."

Idhaa ya kiswahili 2008-10-07